Mafukara Wanataka Kula Nyama Zilizochinjwa Makaburini

Swali: Sisi katika mji wetu Eritrea kuna makaburi watu wanayazuru. ´Allaamah al-Fawzaan: Kila mahala siku hizi kuna makaburi. Muulizaji: Baadhi ya watu hawa (wanaozuru) ni mafukara na wanaenda wawasaidie matumizi na njaa walonayo ili wale katika vichinjo hivi vinavyochinjwa huko. Inajuzu kufanya hivyo? ´Allaamah al-Fawzaan: Yaani milango mingine yote ya riziki imefungwa mpaka aende makaburini tu? Tafuta riziki kwa Allaah Allaah (´Azza wa Jala). Na Allaah yu Karibu Mwenye kujibu. Na njia za kutafuta riziki ni nyingi na usende makaburini na kula katika vichinjo vyao ni Haramu kwa kuwa ni maiti hiyo mizoga. Kuchinja kwenye makaburi ni Shirki, vimechinjwa kwa ajili ya asiyekuwa Allaah. وَلاَ تَأْكُلُواْ مِمَّا لَمْ يُذْكَرِ اسْمُ اللّهِ عَلَيْهِ “Wala msile katika wale wasio somewa jina la Allaah.” (06:121) إِنَّمَا حَرَّمَ عَلَيْكُمُ الْمَيْتَةَ وَالدَّمَ وَلَحْمَ الْخِنزِيرِ وَمَا أُهِلَّ بِهِ لِغَيْرِ اللّهِ “Yeye Amekuharimishieni mzoga tu na damu na nyamaya nguruwe na kilicho tajiwa - katika kuchinjwa kwake jina la asiyekuwa Allaah.” (02:173) Zimechinjwa kwa ajili ya asiyekuwa Allaah, hivyo ni Haramu kwenu.

Swali:
Sisi katika mji wetu Eritrea kuna makaburi watu wanayazuru.

´Allaamah al-Fawzaan:
Kila mahala siku hizi kuna makaburi.

Muulizaji:
Baadhi ya watu hawa (wanaozuru) ni mafukara na wanaenda wawasaidie matumizi na njaa walonayo ili wale katika vichinjo hivi vinavyochinjwa huko. Inajuzu kufanya hivyo?

´Allaamah al-Fawzaan:
Yaani milango mingine yote ya riziki imefungwa mpaka aende makaburini tu? Tafuta riziki kwa Allaah Allaah (´Azza wa Jala). Na Allaah yu Karibu Mwenye kujibu. Na njia za kutafuta riziki ni nyingi na usende makaburini na kula katika vichinjo vyao ni Haramu kwa kuwa ni maiti hiyo mizoga. Kuchinja kwenye makaburi ni Shirki, vimechinjwa kwa ajili ya asiyekuwa Allaah.

وَلاَ تَأْكُلُواْ مِمَّا لَمْ يُذْكَرِ اسْمُ اللّهِ عَلَيْهِ
“Wala msile katika wale wasio somewa jina la Allaah.” (06:121)

إِنَّمَا حَرَّمَ عَلَيْكُمُ الْمَيْتَةَ وَالدَّمَ وَلَحْمَ الْخِنزِيرِ وَمَا أُهِلَّ بِهِ لِغَيْرِ اللّهِ
“Yeye Amekuharimishieni mzoga tu na damu na nyamaya nguruwe na kilicho tajiwa – katika kuchinjwa kwake jina la asiyekuwa Allaah.” (02:173)

Zimechinjwa kwa ajili ya asiyekuwa Allaah, hivyo ni Haramu kwenu.