Madhehebu Ya Khawaarij Na Mu´tazilah Kwa Anayetenda Dhambi Kubwa

Moto utaingia makafiri na washirikina kama jinsi anavoweza pia kuingia muumini mpwekeshaji, lakini kafiri na mshirikina watadumishwa Motoni tofauti na mpwekeshaji na muumini hatodumishwa Motoni ikiwa wataingia. Hii ndio ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah tofauti na Khawaarij na Mu´tazilah. Khawaarij wanasema mwenye kutenda dhambi kubwa ni kafiri na ametoka katika Uislamu. Akifa pasina kutubu, atadumishwa Motoni milele kama makafiri. Mu´tazilah wanasema (Muislamu mwenye kutenda dhambi kubwa) anatoka katika Uislamu na wala haingii katika kufuru. Anakuwa kwenye manzilah moja baina ya manzilah mbili. Akifa kabla ya kutubu, atadumishwa Motoni milele kama wasemavo Khawaarij. Madhehebu yote mawili ni batili na potevu na wanaenda kinyume na dalili. Allaah (Jalla wa ´Alaa) Anasema: إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ “Hakika Allaah Hasamehi kushirikishwa; lakini Anasamehe yasiyokuwa hayo kwa Amtakae.” (an-Nisaa:48) Imekuja vilevile katika Hadiyth: “... mtoeni Motoni yule ambaye ndani ya moyo wake kuna chembe ndogo sana sana sana ya imani mfano wa mbegu ya hardali.” Atatolewa hali ya kuwa kishaunguzwa na kuwa kama makaa. Atawekwa katika mto miongoni mwa mito ya Peponi, mwili wake uchipuke kama yanavochipuka majani, kisha aingie Peponi. Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy Chanzo: al-Haaiyyah Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan Chanzo: "Sharh al-Haaiyyah", uk. 170-171

Moto utaingia makafiri na washirikina kama jinsi anavoweza pia kuingia muumini mpwekeshaji, lakini kafiri na mshirikina watadumishwa Motoni tofauti na mpwekeshaji na muumini hatodumishwa Motoni ikiwa wataingia. Hii ndio ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah tofauti na Khawaarij na Mu´tazilah.

Khawaarij wanasema mwenye kutenda dhambi kubwa ni kafiri na ametoka katika Uislamu. Akifa pasina kutubu, atadumishwa Motoni milele kama makafiri.

Mu´tazilah wanasema (Muislamu mwenye kutenda dhambi kubwa) anatoka katika Uislamu na wala haingii katika kufuru. Anakuwa kwenye manzilah moja baina ya manzilah mbili. Akifa kabla ya kutubu, atadumishwa Motoni milele kama wasemavo Khawaarij.

Madhehebu yote mawili ni batili na potevu na wanaenda kinyume na dalili. Allaah (Jalla wa ´Alaa) Anasema:

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ
“Hakika Allaah Hasamehi kushirikishwa; lakini Anasamehe yasiyokuwa hayo kwa Amtakae.” (an-Nisaa:48)
Imekuja vilevile katika Hadiyth:

“… mtoeni Motoni yule ambaye ndani ya moyo wake kuna chembe ndogo sana sana sana ya imani mfano wa mbegu ya hardali.”

Atatolewa hali ya kuwa kishaunguzwa na kuwa kama makaa. Atawekwa katika mto miongoni mwa mito ya Peponi, mwili wake uchipuke kama yanavochipuka majani, kisha aingie Peponi.

Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy
Chanzo: al-Haaiyyah
Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: “Sharh al-Haaiyyah”, uk. 170-171


  • Kitengo: Uncategorized , Aakhirah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Saturday 22nd, February 2014