Madhehebu Ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah Juu Ya Mikono Ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala)

Allaah (Jalla wa ´Alaa) Ana Sifa za Dhati na Ana Sifa za Matendo, kama Kustawaa, Kushuka, Kuumba, Kuruzuku na Kuongea. Zote hizo ni katika Sifa za Matendo Yake (Subhaanahu wa Ta´ala). Miongoni mwa Sifa za Dhati ni Mikono miwili. Kumekuja kinachoithibitisha katika Maneno ya Allaah (´Azza wa Jalla) na katika Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa mfano Kauli Yake: وَالسَّمَاوَاتُ مَطْوِيَّاتٌ بِيَمِينِهِ “Na mbingu zitakunjwa Mkononi Mwake wa kulia.” (az-Zumar:67) قَالَ يَا إِبْلِيسُ مَا مَنَعَكَ أَن تَسْجُدَ لِمَا خَلَقْتُ بِيَدَيَّ “(Allaah) Akasema: “Ee Ibliys! Nini kilichokuzuia usimsujudie Niliyemuumba kwa Mikono Yangu?” (Swaad:75) yaani Aadam (´alayhis-Salaam). Imekuja pia katika Hadiyth: “Mikono ya Allaah ni yenye kujaa. Inatoa usiku na mchana.” Na isiyokuwa hiyo katika Hadiyth zilizothibiti Swahiyh katika kuthibitisha Mikono na Mkono wa (´Azza wa Jalla). Maana yake inajuliana vizuri kilugha. Ni Mikono ya kihakika, lakini hata hivyo sio kama mikono ya viumbe. Bali ni Mikono inayolingana na Utukufu na Ukubwa wa Allaah (´Azza wa Jalla). Hakuna ajuae namna ilivyo isipokuwa Allaah Mwenyewe (´Azza wa Jalla). Sisi tunamthibitishia nayo Allaah kwa maana yake ya kihakika na tunamkanushia ufananisho na ushabihisho (Jalla wa ´Alaa). Sisi tunaithibitisha juu ya maana yake ya kihakika na tunaikanushia (Mikono hiyo Miwili) ufananisho na ushabihisho. Hawaishabihishi na mikono ya viumbe. Haya ndio madhehebu ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Madhehebu yanayotembea juu ya Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Jambo lao katika hilo ni kama jambo lao katika baki ya Majina na Sifa zingine za Allaah (´Azza wa Jalla). Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy Chanzo: al-Haaiyyah Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan Chanzo: "Sharh al-Haaiyyah", uk. 92-93

Allaah (Jalla wa ´Alaa) Ana Sifa za Dhati na Ana Sifa za Matendo, kama Kustawaa, Kushuka, Kuumba, Kuruzuku na Kuongea. Zote hizo ni katika Sifa za Matendo Yake (Subhaanahu wa Ta´ala).

Miongoni mwa Sifa za Dhati ni Mikono miwili. Kumekuja kinachoithibitisha katika Maneno ya Allaah (´Azza wa Jalla) na katika Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa mfano Kauli Yake:

وَالسَّمَاوَاتُ مَطْوِيَّاتٌ بِيَمِينِهِ
“Na mbingu zitakunjwa Mkononi Mwake wa kulia.” (az-Zumar:67)

قَالَ يَا إِبْلِيسُ مَا مَنَعَكَ أَن تَسْجُدَ لِمَا خَلَقْتُ بِيَدَيَّ
“(Allaah) Akasema: “Ee Ibliys! Nini kilichokuzuia usimsujudie Niliyemuumba kwa Mikono Yangu?” (Swaad:75)

yaani Aadam (´alayhis-Salaam).

Imekuja pia katika Hadiyth:

“Mikono ya Allaah ni yenye kujaa. Inatoa usiku na mchana.”

Na isiyokuwa hiyo katika Hadiyth zilizothibiti Swahiyh katika kuthibitisha Mikono na Mkono wa (´Azza wa Jalla). Maana yake inajuliana vizuri kilugha. Ni Mikono ya kihakika, lakini hata hivyo sio kama mikono ya viumbe. Bali ni Mikono inayolingana na Utukufu na Ukubwa wa Allaah (´Azza wa Jalla). Hakuna ajuae namna ilivyo isipokuwa Allaah Mwenyewe (´Azza wa Jalla). Sisi tunamthibitishia nayo Allaah kwa maana yake ya kihakika na tunamkanushia ufananisho na ushabihisho (Jalla wa ´Alaa). Sisi tunaithibitisha juu ya maana yake ya kihakika na tunaikanushia (Mikono hiyo Miwili) ufananisho na ushabihisho. Hawaishabihishi na mikono ya viumbe. Haya ndio madhehebu ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Madhehebu yanayotembea juu ya Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Jambo lao katika hilo ni kama jambo lao katika baki ya Majina na Sifa zingine za Allaah (´Azza wa Jalla).

Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy
Chanzo: al-Haaiyyah
Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: “Sharh al-Haaiyyah”, uk. 92-93


  • Kitengo: Uncategorized , Mikono ya Allaah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Saturday 15th, February 2014