Lini Kuhukumu Kinyume Na Aliyoteremsha Allaah Mtu Anakuwa Kafiri?

Wale wanaowakufurisha watawala wa Kiislamu, na wanawakufurisha wale ambao hawahukumu kwa yale Aliyoteremsha Allaah (Jalla wa ´Alaa), hata hivyo masuala haya yanahitajia ufafanuzi. Kuhusiana na kuhukumu kwa yale Aliyoteremsha Allaah (Jalla wa ´Alaa). Hakimu anaweza kuwa kafiri - ukafiri wa kumtoa katika Uislamu akihukumu kinyume na Aliyoteremsha Allaah huku akiitakidi (akiamini) kuhukumu kinyume na Aliyoteremsha Allaah ni bora zaidi kuliko kuhukumu kwa Aliyoteremsha Allaah (Jalla wa ´Alaa). Huyu ni kafiri! Ataehukumu kinyume na Aliyoteremsha Allaah huku akiitakidi kuwa [hukumu hio] iko sawa na hukumu ya Allaah huyu ni kafiri! Na ataehukumu kinyume na Aliyoteremsha Allaah huku akiamini kuwa inajuzu kuhukumu kinyume na Aliyoteremsha Allaah, huyu pia ni kafiri kufuru kubwa! Ama akihukumu kinyume na Aliyoteremsha Allaah huku akiamini kuhukumu kwa Aliyoteremsha Allaah ndio bora zaidi na (ndio hukumu) iliyo kamili, lakini kwa (kupewa) rushwa, kupenda cheo au kutaka kufikia jambo fulani la kidunia - akahukumu naye ni mwenye kuitakidi kuwa ni dhalimu na aasi kwa hali hii hatoki katika Uislamu na kufuru yake ni kufuru ndogo kama alivyosema Ibnu ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kwa kauli ya Allaah: وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللّهُ فَأُوْلَـئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ “Na wasiohukumu kwa Aliyoteremsha Allaah, basi hao ndio makafiri.” (05:44) Akasema ni kufuru duni ya kufuru (kubwa). Khawaarij wanamwita mtu huyu kafiri, na wanahalalisha damu yake na mali. Hivyo ndio maana walimkufurisha ´Aliy, Mu´aawiyah na Maswahabah wote na wakahalalisha yanayohalalishwa kwa makafiri. Ama Mu´tazilah wanasema mwenye kufanya dhambi kubwa anatoka katika Iymaan (Uislamu) na wala haingii katika kufuru, mtu huyo yuko katika manziylah mbili - mtu hawezi kusema ni kafiri wala kusema ni muumini. Hii ni katika misingi ya Mu´tazilah. Wana misingi mingine kuhusiana na Tawhiyd, makusudio ya Tawhiyd kwao ni kupinga (kuzikanusha) Sifa (za Allaah). Hivyo akiongelea mtu kuhusu Tawhiyd ni juu yake kubainisha uhakika wa Tawhiyd ambayo waliomo. Kuna ambao wanasema Tawhiyd maana yake ni al-Haakimiyyah - maaya ya Laa ilaaha illa Allaah maana yake ni al-Haakimiyyah. Na hii ndio itikadi ya al-Ikhwaan al-Muflisuunn.

Wale wanaowakufurisha watawala wa Kiislamu, na wanawakufurisha wale ambao hawahukumu kwa yale Aliyoteremsha Allaah (Jalla wa ´Alaa), hata hivyo masuala haya yanahitajia ufafanuzi.

Kuhusiana na kuhukumu kwa yale Aliyoteremsha Allaah (Jalla wa ´Alaa). Hakimu anaweza kuwa kafiri – ukafiri wa kumtoa katika Uislamu akihukumu kinyume na Aliyoteremsha Allaah huku akiitakidi (akiamini) kuhukumu kinyume na Aliyoteremsha Allaah ni bora zaidi kuliko kuhukumu kwa Aliyoteremsha Allaah (Jalla wa ´Alaa). Huyu ni kafiri!

Ataehukumu kinyume na Aliyoteremsha Allaah huku akiitakidi kuwa [hukumu hio] iko sawa na hukumu ya Allaah huyu ni kafiri!

Na ataehukumu kinyume na Aliyoteremsha Allaah huku akiamini kuwa inajuzu kuhukumu kinyume na Aliyoteremsha Allaah, huyu pia ni kafiri kufuru kubwa!

Ama akihukumu kinyume na Aliyoteremsha Allaah huku akiamini kuhukumu kwa Aliyoteremsha Allaah ndio bora zaidi na (ndio hukumu) iliyo kamili, lakini kwa (kupewa) rushwa, kupenda cheo au kutaka kufikia jambo fulani la kidunia – akahukumu naye ni mwenye kuitakidi kuwa ni dhalimu na aasi kwa hali hii hatoki katika Uislamu na kufuru yake ni kufuru ndogo kama alivyosema Ibnu ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kwa kauli ya Allaah:

وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللّهُ فَأُوْلَـئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ
“Na wasiohukumu kwa Aliyoteremsha Allaah, basi hao ndio makafiri.” (05:44)

Akasema ni kufuru duni ya kufuru (kubwa).

Khawaarij wanamwita mtu huyu kafiri, na wanahalalisha damu yake na mali. Hivyo ndio maana walimkufurisha ´Aliy, Mu´aawiyah na Maswahabah wote na wakahalalisha yanayohalalishwa kwa makafiri.

Ama Mu´tazilah wanasema mwenye kufanya dhambi kubwa anatoka katika Iymaan (Uislamu) na wala haingii katika kufuru, mtu huyo yuko katika manziylah mbili – mtu hawezi kusema ni kafiri wala kusema ni muumini. Hii ni katika misingi ya Mu´tazilah.

Wana misingi mingine kuhusiana na Tawhiyd, makusudio ya Tawhiyd kwao ni kupinga (kuzikanusha) Sifa (za Allaah).

Hivyo akiongelea mtu kuhusu Tawhiyd ni juu yake kubainisha uhakika wa Tawhiyd ambayo waliomo. Kuna ambao wanasema Tawhiyd maana yake ni al-Haakimiyyah – maaya ya Laa ilaaha illa Allaah maana yake ni al-Haakimiyyah. Na hii ndio itikadi ya al-Ikhwaan al-Muflisuunn.