Lini Inaanza Takbiyr Siku Ya Idi al-Fitwr Na Idi Adhwhaa Na Lini Inaisha?

Swali: Lini inaanza Takbiyr kwenye ´Iyd al-Fitwr na lini inaisha? Na kwenye ´Iyd al-Adhwhaa lini inaanza na lini inaisha? ´Allaamah Muqibil al-Waadi´iy: Tumekwishajibia hili. Katika ´Iyd al-Fitwr ni wakati watu wanatoka katika Swalah na kabla ya swalah, ama baada yake hakuna ubaya wakaleta Takbiyr siku ile ile ya ´Iyd. Ama ´Iyd al-Adhwhaa ni katika Ayaamut-Tashriyq (tarehe 11, 12, 13 Dhul-Hijjah) lakini kusiletwe katika Swalah zilizobaki bali kunaletwa adhkaar za kawaida. Muulizaji: Je, kila mtu alete Takbiyr kivyake? ´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy: Kila mtu aleta kivyake na inapasa kuwa namna hii, au mmoja akaleta Takbiyr na wengine wakaitikia au wakaleta kikundi. Lakini lililo bora ni kila mtu kuleta kivyake. Muulizaji: Je, waweke mpaka idadi ya Takbiyr au hapana? ´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy: Takbiyr ni mkusanyiko. Na udogo wake ni Takbiyr tatu [yaani Allaahu Akbar, Allaahu Akbar, Allaahu Akbar... ] na wakizidisha hakuna ubaya.

Swali:
Lini inaanza Takbiyr kwenye ´Iyd al-Fitwr na lini inaisha? Na kwenye ´Iyd al-Adhwhaa lini inaanza na lini inaisha?

´Allaamah Muqibil al-Waadi´iy:
Tumekwishajibia hili. Katika ´Iyd al-Fitwr ni wakati watu wanatoka katika Swalah na kabla ya swalah, ama baada yake hakuna ubaya wakaleta Takbiyr siku ile ile ya ´Iyd. Ama ´Iyd al-Adhwhaa ni katika Ayaamut-Tashriyq (tarehe 11, 12, 13 Dhul-Hijjah) lakini kusiletwe katika Swalah zilizobaki bali kunaletwa adhkaar za kawaida.

Muulizaji:
Je, kila mtu alete Takbiyr kivyake?

´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Kila mtu aleta kivyake na inapasa kuwa namna hii, au mmoja akaleta Takbiyr na wengine wakaitikia au wakaleta kikundi. Lakini lililo bora ni kila mtu kuleta kivyake.

Muulizaji:
Je, waweke mpaka idadi ya Takbiyr au hapana?

´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
Takbiyr ni mkusanyiko. Na udogo wake ni Takbiyr tatu [yaani Allaahu Akbar, Allaahu Akbar, Allaahu Akbar… ] na wakizidisha hakuna ubaya.