Lengo La ISIS

ISIS! Ole wenu! Tahadharini na Allaah! Picha mnazoeneza ili kuwashtua watu na kuwafanya wafahamu kuwa nyinyi ni wamwaga damu, basi ndio mjue kuwa nyinyi hamuuwakilishi Uislamu. Nyinyi ni njama dhidi ya Uislamu. Mna ´Aqiydah ya Khawaarij ambayo Waislamu ni wenye kujitenga nayo mbali. Ninamwambia kila mwenye kusikia haya sawa wale waliohudhuria au wale wenye kusikia kupitia vyombo vya mawasiliano: Ninaapa kwa Allaah ya kwamba yale wanayoyafanya hayawakilishi Dini ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambayo ni Dini ya Rahmah. Imekuja ili kusahihisha ´Aqiydah na ´Ibaadah, kuwafundisha watu na kuwafunza tabia. Uislamu umekuja ili kueneza haki na kuiponda batili. Wamwaga damu kama haya yafanywayo na hawa yamefanywa na kila mtu asiyekuwa wa kawaida ulimwenguni. Huwa wakielezana yaliyopitika baina yao Ulaya na wakati wa kipindi cha kiza na jinsi walivyokuwa wanauana. Vyombo vya mateso vimeenea katika enzi za kati. Kunaelezwa jinsi watu wanavyouana, kukanyagana kufa na kuchokamana hadi kufa. Hili ndio jukwaa lao na hii ndio natija yao. Ni kampeni dhidi ya Uislamu. Wana watu wao nyuma ya migongo yao – Allaah Awafichue na Allaah Asiwape uongozi wowote duniani. Lengo lao limefichuliwa nalo ni kuchafua sura ya Uislamu.

ISIS! Ole wenu! Tahadharini na Allaah! Picha mnazoeneza ili kuwashtua watu na kuwafanya wafahamu kuwa nyinyi ni wamwaga damu, basi ndio mjue kuwa nyinyi hamuuwakilishi Uislamu. Nyinyi ni njama dhidi ya Uislamu. Mna ´Aqiydah ya Khawaarij ambayo Waislamu ni wenye kujitenga nayo mbali.

Ninamwambia kila mwenye kusikia haya sawa wale waliohudhuria au wale wenye kusikia kupitia vyombo vya mawasiliano: Ninaapa kwa Allaah ya kwamba yale wanayoyafanya hayawakilishi Dini ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambayo ni Dini ya Rahmah. Imekuja ili kusahihisha ´Aqiydah na ´Ibaadah, kuwafundisha watu na kuwafunza tabia. Uislamu umekuja ili kueneza haki na kuiponda batili.

Wamwaga damu kama haya yafanywayo na hawa yamefanywa na kila mtu asiyekuwa wa kawaida ulimwenguni. Huwa wakielezana yaliyopitika baina yao Ulaya na wakati wa kipindi cha kiza na jinsi walivyokuwa wanauana. Vyombo vya mateso vimeenea katika enzi za kati. Kunaelezwa jinsi watu wanavyouana, kukanyagana kufa na kuchokamana hadi kufa.

Hili ndio jukwaa lao na hii ndio natija yao. Ni kampeni dhidi ya Uislamu. Wana watu wao nyuma ya migongo yao – Allaah Awafichue na Allaah Asiwape uongozi wowote duniani. Lengo lao limefichuliwa nalo ni kuchafua sura ya Uislamu.