Laana Ya Allaah Iwe Juu Ya Mwanamke Mwenye Kutoa Nyusi Zake

Jambo la tatu [miongoni mwa makatazo yanayopingana na Shari'ah], ni kwamba baadhi ya wanawake wananyoa nyusi zao ili zionekane kama upinde au mwezi mwembamba. Wanafanya namna hii kwa kudai ya kuwa ni kuleta uzuri. Kitendo hichi Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekiharamisha na kuwalaani wanawake wanaonyoa nyusi. "Allaah Amemlaani mwanamke anayefanya tattoo (kuchorwa kwa kuchanjwa) na mwenye kuomba kufanyiwa, mwenye kuunga nywele na mwenye kuungwa nywele, anayetoa nyusi na mwenye kuomba kutolewa nyusi[1] na anayechonga meno kuweka nafasi (mwanya) kwa ajili ya kubadilisha maumbile ya Allaah kwa kutaka kupata uzuri."(2) ----------------- (1) at-Twabariy kasema: "Mwanamke hatakiwi kufanya mabadiliko yoyote katika yale ambayo Allaah Amemuumba nayo kwa kuongeza au kupunguza kwa ajili ya kujipamba. Hatakiwi kufanya hivyo kwa ajili ya mume wake au kwa ajili ya mtu mwingine yeyote. Mfano wa hili ni kama kuwa na nyusi sawa na za watu wazima na kuondosha kile kilicho katikati yazo." (Ufupisho wa "Fath-ul-Baariy") (2) al-Bukhaariy (10/306) na Muslim (06/122)

Jambo la tatu [miongoni mwa makatazo yanayopingana na Shari’ah], ni kwamba baadhi ya wanawake wananyoa nyusi zao ili zionekane kama upinde au mwezi mwembamba. Wanafanya namna hii kwa kudai ya kuwa ni kuleta uzuri. Kitendo hichi Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekiharamisha na kuwalaani wanawake wanaonyoa nyusi.

“Allaah Amemlaani mwanamke anayefanya tattoo (kuchorwa kwa kuchanjwa) na mwenye kuomba kufanyiwa, mwenye kuunga nywele na mwenye kuungwa nywele, anayetoa nyusi na mwenye kuomba kutolewa nyusi[1] na anayechonga meno kuweka nafasi (mwanya) kwa ajili ya kubadilisha maumbile ya Allaah kwa kutaka kupata uzuri.”(2)

—————–
(1) at-Twabariy kasema:

“Mwanamke hatakiwi kufanya mabadiliko yoyote katika yale ambayo Allaah Amemuumba nayo kwa kuongeza au kupunguza kwa ajili ya kujipamba. Hatakiwi kufanya hivyo kwa ajili ya mume wake au kwa ajili ya mtu mwingine yeyote. Mfano wa hili ni kama kuwa na nyusi sawa na za watu wazima na kuondosha kile kilicho katikati yazo.” (Ufupisho wa “Fath-ul-Baariy”)

(2) al-Bukhaariy (10/306) na Muslim (06/122)


  • Author: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy. "´Adaab-uz-Zaffaaf", uk. 201-202
  • Kitengo: Uncategorized , Fiqh
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 5th, January 2014