Kuwaweka Wazazi Katika Nyumba Ya Wazee

Kulinda udugu kunaleta athari duniani na Akhera. Na ikiwa kuulinda udugu kunapelekea kuishi kwa muda mrefu, na kunapelekea ukunjufu wa ziriki, hivyo wema kwa wazazi itakuwa auli zaidi kwa kuwa wao wako karibu zaidi kuliko vyote. Kuwatendea wema wazazi kunapelekea Allaah Anapanua maisha yako na Anakurefushia umri wako. Na kutowatendea haki kunapelekea kuwa na umri mfupi na ugumu wa kupata riziki. Kama jinsi kuwatendea wema tunapelekea katika upana wa umri na riziki kuongezeka. Na jazaa (malipo) ni katika asli ya kitendo. وَلَا تُجْزَوْنَ إِلَّا مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ "Wala hamtalipwa ila yale mliyokuwa mkiyatenda." (36:54) Unafikiria nini kwa ambacho kimezoeleka leo, kwa masikitiko makubwa katika jamii za Kiislamu wakati wazazi wanapokuwa wazee wanatupwa katika nyumba za ihsaan, au nyumba za wazee kama wanavyoziita. Mtoto ndie anaefanya hivyo anawaweka wazazi wake au mmoja wao katika nyumba za wazee. Utafikiria kana kwamba si watoto wake, au utafikiria ya kwamba ni wazazi wa watu hawa wanaofanya kazi katika nyumba za wazee. Yaa Subhaana Allaah! Je [anaefanya hivi] ni mtu kweli au ni mnyama?! Laa hawlah wala Quwwata illa bi Allaah. Huu ni katika ukosefu mkubwa wa adabu. Hili halifanywi na yule ambae kwenye moyo wake kuna khofu kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Ungelijisikiaje lau mtoto wako angelikufanyia kitendo hiki?! Unapo zeeka na kuwa mgonjwa wanakuchukua na kukuweka katika nyumba ya wazee. Ungelijisikiaje? Ungeliwakasirikiaje? Na dhambi ipi ambayo mtoto wako angeliibeba? Kwanini wewe unaomba haki yako na wewe hutimizi haki ambayo iko juu yako?! Amche Allaah kila Muislamu. Ukosefu wa adabu kwa wazazi umeenea sana katika zama hizi, nyoyo zimekuwa ngumu na wandugu kufarakana. Tumejiwa na maadui wa magharibi na makafiri; ambao hawana familia wala nyumba isipokuwa nyumba zao ni kama nyumba za minyama. Nyumbani kwao wanaishi wenyewe au na mbwa. Ama kukuta anaishi na wazazi wake, na watoto wake, na ndugu zake, hapana! Hili halipo katika miji mingi ya kikafiri. Lenye kinachosikitisha ni kwamba baadhi ya Waislamu leo wanataka kuwaiga. Wanataka kuwatupa wazazi wao au mmoja wao katika manyumba ya wazee na ili wawe zao huru. Na kama ana aina fulani ya hisia huenda akaja siku ya Idi kuwasalimia, kuwazuru tu. Au baada ya siku ndo anawapitia na kuwasalimia. Na anachukulia kuwa eti hii ndo haki kubwa alonayo juu yao. Ni juu ya Muislamu kutanabahi na kumcha Allaah; na ajue kuwa anachofanya [anachotendea mwengine] naye atatendewa. Na atalipwa kwa kitendo chake, na asitangulize kunako haki za wazazi wawili chochote isipokuwa tu utiifu [haki] za Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Ikiwa anataka ujira na anataka thawabu asitangulize chochote katika matendo isipokuwa haki za wazazi, isipokuwa tu haki za Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Na kwa haya, namuomba Allaah (Jalla wa ´Alaa) kwa Majina Yake Mazuri na Sifa Zake kuu Awaongoze watoto na vizazi vya Waislamu. Na tunamuomba Awarudishe Waislamu katika Uislamu wao kwa sura nzuri inayotakikana. Na Awafanye Waislamu wawe ni wenye kupendana na Ayafanye manyumba yao kuwa mazuri. Tunamuomba Allaah vilevile Awaepushe na kujifananisha na makafiri na wanafiki, na wale ambao wamekata na kuvunja udugu wakawa kama minyama au wakapotea zaidi. Wa laa hawla wa Quwwata illa bi Allaah.

Kulinda udugu kunaleta athari duniani na Akhera. Na ikiwa kuulinda udugu kunapelekea kuishi kwa muda mrefu, na kunapelekea ukunjufu wa ziriki, hivyo wema kwa wazazi itakuwa auli zaidi kwa kuwa wao wako karibu zaidi kuliko vyote. Kuwatendea wema wazazi kunapelekea Allaah Anapanua maisha yako na Anakurefushia umri wako. Na kutowatendea haki kunapelekea kuwa na umri mfupi na ugumu wa kupata riziki. Kama jinsi kuwatendea wema tunapelekea katika upana wa umri na riziki kuongezeka. Na jazaa (malipo) ni katika asli ya kitendo.

وَلَا تُجْزَوْنَ إِلَّا مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ
“Wala hamtalipwa ila yale mliyokuwa mkiyatenda.” (36:54)

Unafikiria nini kwa ambacho kimezoeleka leo, kwa masikitiko makubwa katika jamii za Kiislamu wakati wazazi wanapokuwa wazee wanatupwa katika nyumba za ihsaan, au nyumba za wazee kama wanavyoziita. Mtoto ndie anaefanya hivyo anawaweka wazazi wake au mmoja wao katika nyumba za wazee. Utafikiria kana kwamba si watoto wake, au utafikiria ya kwamba ni wazazi wa watu hawa wanaofanya kazi katika nyumba za wazee. Yaa Subhaana Allaah! Je [anaefanya hivi] ni mtu kweli au ni mnyama?! Laa hawlah wala Quwwata illa bi Allaah. Huu ni katika ukosefu mkubwa wa adabu. Hili halifanywi na yule ambae kwenye moyo wake kuna khofu kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Ungelijisikiaje lau mtoto wako angelikufanyia kitendo hiki?! Unapo zeeka na kuwa mgonjwa wanakuchukua na kukuweka katika nyumba ya wazee. Ungelijisikiaje? Ungeliwakasirikiaje? Na dhambi ipi ambayo mtoto wako angeliibeba? Kwanini wewe unaomba haki yako na wewe hutimizi haki ambayo iko juu yako?! Amche Allaah kila Muislamu. Ukosefu wa adabu kwa wazazi umeenea sana katika zama hizi, nyoyo zimekuwa ngumu na wandugu kufarakana. Tumejiwa na maadui wa magharibi na makafiri; ambao hawana familia wala nyumba isipokuwa nyumba zao ni kama nyumba za minyama. Nyumbani kwao wanaishi wenyewe au na mbwa. Ama kukuta anaishi na wazazi wake, na watoto wake, na ndugu zake, hapana! Hili halipo katika miji mingi ya kikafiri.

Lenye kinachosikitisha ni kwamba baadhi ya Waislamu leo wanataka kuwaiga. Wanataka kuwatupa wazazi wao au mmoja wao katika manyumba ya wazee na ili wawe zao huru. Na kama ana aina fulani ya hisia huenda akaja siku ya Idi kuwasalimia, kuwazuru tu. Au baada ya siku ndo anawapitia na kuwasalimia. Na anachukulia kuwa eti hii ndo haki kubwa alonayo juu yao. Ni juu ya Muislamu kutanabahi na kumcha Allaah; na ajue kuwa anachofanya [anachotendea mwengine] naye atatendewa. Na atalipwa kwa kitendo chake, na asitangulize kunako haki za wazazi wawili chochote isipokuwa tu utiifu [haki] za Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Ikiwa anataka ujira na anataka thawabu asitangulize chochote katika matendo isipokuwa haki za wazazi, isipokuwa tu haki za Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

Na kwa haya, namuomba Allaah (Jalla wa ´Alaa) kwa Majina Yake Mazuri na Sifa Zake kuu Awaongoze watoto na vizazi vya Waislamu. Na tunamuomba Awarudishe Waislamu katika Uislamu wao kwa sura nzuri inayotakikana. Na Awafanye Waislamu wawe ni wenye kupendana na Ayafanye manyumba yao kuwa mazuri. Tunamuomba Allaah vilevile Awaepushe na kujifananisha na makafiri na wanafiki, na wale ambao wamekata na kuvunja udugu wakawa kama minyama au wakapotea zaidi. Wa laa hawla wa Quwwata illa bi Allaah.