Kuwapa Mkono Wa Pole Makafiri Wanapofiwa

Swali La Kwanza: Kiongozi wa upotofu kafariki Papa Johanna. Je inajuzu kusema mafikio yake ni Motoni kwa kuwa kafa katika kufuru na ipi hukumu ya kutoa taazia [mkono wa pole]... ´Allaamah al-Fawzaan: Kipi kikujulishacho kwamba kafa katika kufuru? Usilenge. Usilenge moja kwa moja kwamba kafa katika kufuru. Haijuzu kumshuhudia yeyote Pepo wala Moto ila yule aliyemshuhudia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Usilenge moja kwa moja kwamba kafa katika kufuru. Allaah Anajua zaidi. Hivyo ndo maana usilenge kwamba ni katika watu wa Motoni. Hii ndo kanuni kwamba hashuhudiwi mtu maalumu. Ama makafiri, manaswara na mayahudi kwa ujumla ni motoni. Ila kusema Johanna [Paulo] ataingia motoni ni kosa. Watakiwa kusema Kuna uwezekano akaingia motoni. Allaah Anajua zaidi. Unaweza pia kusema ikiwa kafa katika ukafiri basi ataingia motoni na ikiwa alikufa kwa kufanya Tawbah ataingia Peponi. Usilenge kitu ila kwa dalili. Swali La Pili: Na ipi hukumu ya kutoa taazia (mkono wa pole) kwa makafiri wanapokufa? ´Allaamah al-Fawzaan: Mtu (haijuzu) kutoa taazia kwa makafiri. Mtu anatoa taazia kwa kafiri kwa muumini. Ikiwa ndugu yake muumini (muislamu) kafa, unatoa taazia kwa muumini. Ama kutoa taazia kwa kafiri haijuzu kufanya hivyo.

Swali La Kwanza:
Kiongozi wa upotofu kafariki Papa Johanna. Je inajuzu kusema mafikio yake ni Motoni kwa kuwa kafa katika kufuru na ipi hukumu ya kutoa taazia [mkono wa pole]…

´Allaamah al-Fawzaan:
Kipi kikujulishacho kwamba kafa katika kufuru? Usilenge. Usilenge moja kwa moja kwamba kafa katika kufuru. Haijuzu kumshuhudia yeyote Pepo wala Moto ila yule aliyemshuhudia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Usilenge moja kwa moja kwamba kafa katika kufuru. Allaah Anajua zaidi. Hivyo ndo maana usilenge kwamba ni katika watu wa Motoni. Hii ndo kanuni kwamba hashuhudiwi mtu maalumu. Ama makafiri, manaswara na mayahudi kwa ujumla ni motoni. Ila kusema Johanna [Paulo] ataingia motoni ni kosa. Watakiwa kusema Kuna uwezekano akaingia motoni. Allaah Anajua zaidi. Unaweza pia kusema ikiwa kafa katika ukafiri basi ataingia motoni na ikiwa alikufa kwa kufanya Tawbah ataingia Peponi. Usilenge kitu ila kwa dalili.

Swali La Pili:
Na ipi hukumu ya kutoa taazia (mkono wa pole) kwa makafiri wanapokufa?

´Allaamah al-Fawzaan:
Mtu (haijuzu) kutoa taazia kwa makafiri. Mtu anatoa taazia kwa kafiri kwa muumini. Ikiwa ndugu yake muumini (muislamu) kafa, unatoa taazia kwa muumini. Ama kutoa taazia kwa kafiri haijuzu kufanya hivyo.