Kutumia Qadar Na Qadhwaa Kuwa Hoja Juu Ya Misiba

Kumebaki masuala mengine ambayo yametajwa na wanachuoni. Nayo ni “kutumia Qadar kama hoja”. Hilo ni kwa ajili Muusa (´alayhis-Salaam) alipokutana na baba wa watu Aadam (´alayhis-Salaam) alimlaumu na kusema: “Kwa nini umetutolesha Peponi?”Akasema: “Wewe ni Muusa umeongeleshwa na Allaah. Allaah Alikuwa Ameshaniandikia haya katika Lawh al-Mahfuudhw.” Muusa akasema – kwa maana yake – Allaah Aliandika hilo kwako katika Lawh al-Mahfuudhw.” Jabriyyah walichukua hili na wakasema kuwa hii ni dalili ya Jabriyyah na vile Aadam ametumia hoja kumwambia Muusa na kusema kwamba yaliyonifika sio kwa khiyari yangu, bali ni Tendo la Allaah (Jalla wa ´Alaa). Ukweli ni kwamba hawakufahamu Hadiyth. Muusa hakumlaumu Aadam kutokana na Qadhwaa na Qadar, bali alimlaumu juu ya kutolewa Peponi. Akasema: “Kwa nini umetutolesha Peponi?” Aadam Akatumia hoja kwake kwa Qadhwaa na Qadar. Kutumia hoja kwa Qadhwaa na Qadar juu ya misiba inajuzu, kwa kuwa linamsaidia kumsahilishia mtu kutokukata tamaa na kukatika nguvu na kutokasirika. Muusa hakumuuliza kutokana na Qadhwaa na Qadar, hakumwambia “Kwa nini Allaah Amekukadiria hivi?” Bali alisema “Kwa nini umetutolesha?” Amesema hivyo akilinasibisha juu ya msiba ambao ulimpitikia Aadam wa kula kutoka kwenye mti. Muusa hakumlaumu kutokana na dhambi. Hakumwambia “Kwa nini ulikula kutoka kwenye mti?” Kwa kuwa ameshatubia kutokana na dhambi na Allaah Akamsamehe. Mwenye kutubu halaumiwi kwa aloyafanya baada ya Tawbah. Isipokuwa alimlaumu juu ya msiba wa kutolewa Peponi. Huu ni msiba uliomsibu Aadam na watoto wake. Aadam (´alayhis-Salaam) alitumia hoja kwake kwa Qadhwaa na Qadar. Kutumia kuwa hoja Qadhwaa na Qadar juu ya misiba ni jambo limewekwa katika Shari´ah (inajuzu). Kwa ajili hii ndio maana akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Na utapofikwa na jambo usiseme: “Lau ningelifanya kadhaa ingelikuwa kadhaa na kadhaa”, lakini badala yake sema: “Hivi ndivyo Alivyokadiria Allaah na Hufanya Atakavyo.” Ametumia hoja kwa Qadhwaa na Qadar juu ya misiba kwa kuwa wewe katika hilo kuna khiyari yoyote. Maasi ni kitendo chako wewe na wewe hapo hutakiwi kutumia hoja Qadhwaa na Qadar. Kutokana na hili wamesema wanachuoni: “Kunatumiwa hoja kwa Qadhwaa na Qadar juu ya misiba na wala haitumiwi hoja kwa maasi.” Huu ndio ufafanuzi katika masuala haya makubwa. Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy Chanzo: al-Haaiyyah Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan Chanzo: "Sharh al-Haaiyyah", uk. 155-157

Kumebaki masuala mengine ambayo yametajwa na wanachuoni. Nayo ni “kutumia Qadar kama hoja”. Hilo ni kwa ajili Muusa (´alayhis-Salaam) alipokutana na baba wa watu Aadam (´alayhis-Salaam) alimlaumu na kusema:

“Kwa nini umetutolesha Peponi?”Akasema:

“Wewe ni Muusa umeongeleshwa na Allaah. Allaah Alikuwa Ameshaniandikia haya katika Lawh al-Mahfuudhw.” Muusa akasema – kwa maana yake – Allaah Aliandika hilo kwako katika Lawh al-Mahfuudhw.”

Jabriyyah walichukua hili na wakasema kuwa hii ni dalili ya Jabriyyah na vile Aadam ametumia hoja kumwambia Muusa na kusema kwamba yaliyonifika sio kwa khiyari yangu, bali ni Tendo la Allaah (Jalla wa ´Alaa). Ukweli ni kwamba hawakufahamu Hadiyth. Muusa hakumlaumu Aadam kutokana na Qadhwaa na Qadar, bali alimlaumu juu ya kutolewa Peponi. Akasema:

“Kwa nini umetutolesha Peponi?”

Aadam Akatumia hoja kwake kwa Qadhwaa na Qadar. Kutumia hoja kwa Qadhwaa na Qadar juu ya misiba inajuzu, kwa kuwa linamsaidia kumsahilishia mtu kutokukata tamaa na kukatika nguvu na kutokasirika. Muusa hakumuuliza kutokana na Qadhwaa na Qadar, hakumwambia “Kwa nini Allaah Amekukadiria hivi?” Bali alisema “Kwa nini umetutolesha?” Amesema hivyo akilinasibisha juu ya msiba ambao ulimpitikia Aadam wa kula kutoka kwenye mti. Muusa hakumlaumu kutokana na dhambi. Hakumwambia “Kwa nini ulikula kutoka kwenye mti?” Kwa kuwa ameshatubia kutokana na dhambi na Allaah Akamsamehe. Mwenye kutubu halaumiwi kwa aloyafanya baada ya Tawbah. Isipokuwa alimlaumu juu ya msiba wa kutolewa Peponi. Huu ni msiba uliomsibu Aadam na watoto wake.

Aadam (´alayhis-Salaam) alitumia hoja kwake kwa Qadhwaa na Qadar. Kutumia kuwa hoja Qadhwaa na Qadar juu ya misiba ni jambo limewekwa katika Shari´ah (inajuzu). Kwa ajili hii ndio maana akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Na utapofikwa na jambo usiseme: “Lau ningelifanya kadhaa ingelikuwa kadhaa na kadhaa”, lakini badala yake sema: “Hivi ndivyo Alivyokadiria Allaah na Hufanya Atakavyo.”

Ametumia hoja kwa Qadhwaa na Qadar juu ya misiba kwa kuwa wewe katika hilo kuna khiyari yoyote. Maasi ni kitendo chako wewe na wewe hapo hutakiwi kutumia hoja Qadhwaa na Qadar. Kutokana na hili wamesema wanachuoni:

“Kunatumiwa hoja kwa Qadhwaa na Qadar juu ya misiba na wala haitumiwi hoja kwa maasi.”

Huu ndio ufafanuzi katika masuala haya makubwa.

Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy
Chanzo: al-Haaiyyah
Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: “Sharh al-Haaiyyah”, uk. 155-157


  • Kitengo: Uncategorized , Jabriyyah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Friday 21st, February 2014