Kutoka Salafiy Kwenda Salaftiy

'Abdur-Rahmaan ´Abdul-Khaaliq alikuwa mzuri mwanzoni. Ndugu zetu wa Kuwait walinufaika kwake huko Kuwait. Alikuwa ni sababu ya kuenea kwa Sunnah nyingi. Inatakiwa kushukuriwa kwa hilo. Kisha akapinda. Da´wah yake ikawa ni mgawanyiko. Lakini mgawanyiko wake ilikuwa ni mgawanyiko kati ya Sunniy na mtu wa Bid´ah, kati ya Muislamu na kafiri? Kama ni hivyo, ni vizuri bila shaka. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema: "Muhammad amewatenganisha watu." Ina maana pale ambapo mtu ambaye ameoa mwanamke wa kikafiri akiingia katika Uislamu au baba aliyeingia katika Uislamu na ana watoto wa kikafiri. Hapa ndipo kulipoanza tofauti mwanzoni wa kuongoza kwake. Ama kuhusu 'Abdur-Rahmaan ´Abdul-Khaaliq, Da´wah yake inawatenganisha Ahl-us-Sunnah ambao wana haja kubwa ya umoja. Ndugu Abu Dhabi na Sudan wamegawanyika kwa sababu yake. Hivi karibuni nimepata barua ambayo inasema kuwa 'Abdur-Rahmaan ´Abdul-Khaaliq amesababisha uchujaji wa Answaar-us-Sunnah. Mimi ninaona uzito kuwaita "Answaar-us-Sunnah", lakini nataja jina kama lilivyo, kama alivofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati aliposema: Mimi ni Mtume na sio uongo Mimi ni mwana wa ´Abdul-Muttwalib Pamoja na kwamba, haijuzu kuwa na jina linaloashiria kuwa mtu ni mja wa mwingine asiyekuwa Allaah. Hivyo basi, ninaonelea vigumu kuwaita "Answaaar-us-Sunnah" wakati ukweli wa mambo ni kwamba wamekuwa Answaar-ul-Baatwil, wanusuraji wa batili. Isipokuwa tu yule Aliyerehemewa na Allaah. Wameanza kuvikidolea macho vitu vya dunia. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amepatia pale aliposema: "Kila Ummah una mtihani na mtihani wa Ummah wangu ni mali." 'Abdur-Rahmaan ´Abdul-Khaaliq alikuwa ni Salafiy ambaye baadae akageuka kuwa Salaftiy. Kwa sababu wanajuzisha upigaji kura na ni katika demokrasia. Allaah Amesema: أَفَمَن كَانَ مُؤْمِنًا كَمَن كَانَ فَاسِقًا ۚ لَّا يَسْتَوُونَ "Je, aliye Muumini atakuwa sawa na aliye fasiki? Hawalingani sawa!" (32:18) أَمْ نَجْعَلُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ كَالْمُفْسِدِينَ فِي الْأَرْضِ أَمْ نَجْعَلُ الْمُتَّقِينَ كَالْفُجَّارِ "Je, Tuwajaalie wale walioamini na wakatenda mema [walingane sawasawa] kama mafisadi katika ardhi? Au Tuwajaalie wenye taqwa kama [sawa] na waovu?" (38:28) وَلَيْسَ الذَّكَرُ كَالْأُنثَىٰ “Na mwanamme si kama mwanamke." (03:36) تِلْكَ إِذًا قِسْمَةٌ ضِيزَىٰ "Huo ni mgawanyo si wa uadilifu." (53:22) Mzungumzaji: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy Chanzo: Naswaaih wa Fadhwaaih, uk. 50-51 Toleo la: 17-12-2014 Imefasiriwa na: Wanachuoni.com

‘Abdur-Rahmaan ´Abdul-Khaaliq alikuwa mzuri mwanzoni. Ndugu zetu wa Kuwait walinufaika kwake huko Kuwait. Alikuwa ni sababu ya kuenea kwa Sunnah nyingi. Inatakiwa kushukuriwa kwa hilo.

Kisha akapinda. Da´wah yake ikawa ni mgawanyiko. Lakini mgawanyiko wake ilikuwa ni mgawanyiko kati ya Sunniy na mtu wa Bid´ah, kati ya Muislamu na kafiri? Kama ni hivyo, ni vizuri bila shaka. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema:

“Muhammad amewatenganisha watu.”

Ina maana pale ambapo mtu ambaye ameoa mwanamke wa kikafiri akiingia katika Uislamu au baba aliyeingia katika Uislamu na ana watoto wa kikafiri. Hapa ndipo kulipoanza tofauti mwanzoni wa kuongoza kwake.

Ama kuhusu ‘Abdur-Rahmaan ´Abdul-Khaaliq, Da´wah yake inawatenganisha Ahl-us-Sunnah ambao wana haja kubwa ya umoja. Ndugu Abu Dhabi na Sudan wamegawanyika kwa sababu yake. Hivi karibuni nimepata barua ambayo inasema kuwa ‘Abdur-Rahmaan ´Abdul-Khaaliq amesababisha uchujaji wa Answaar-us-Sunnah. Mimi ninaona uzito kuwaita “Answaar-us-Sunnah”, lakini nataja jina kama lilivyo, kama alivofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati aliposema:

Mimi ni Mtume na sio uongo
Mimi ni mwana wa ´Abdul-Muttwalib

Pamoja na kwamba, haijuzu kuwa na jina linaloashiria kuwa mtu ni mja wa mwingine asiyekuwa Allaah.

Hivyo basi, ninaonelea vigumu kuwaita “Answaaar-us-Sunnah” wakati ukweli wa mambo ni kwamba wamekuwa Answaar-ul-Baatwil, wanusuraji wa batili. Isipokuwa tu yule Aliyerehemewa na Allaah. Wameanza kuvikidolea macho vitu vya dunia. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amepatia pale aliposema:

“Kila Ummah una mtihani na mtihani wa Ummah wangu ni mali.”

‘Abdur-Rahmaan ´Abdul-Khaaliq alikuwa ni Salafiy ambaye baadae akageuka kuwa Salaftiy. Kwa sababu wanajuzisha upigaji kura na ni katika demokrasia. Allaah Amesema:

أَفَمَن كَانَ مُؤْمِنًا كَمَن كَانَ فَاسِقًا ۚ لَّا يَسْتَوُونَ
“Je, aliye Muumini atakuwa sawa na aliye fasiki? Hawalingani sawa!” (32:18)

أَمْ نَجْعَلُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ كَالْمُفْسِدِينَ فِي الْأَرْضِ أَمْ نَجْعَلُ الْمُتَّقِينَ كَالْفُجَّارِ
“Je, Tuwajaalie wale walioamini na wakatenda mema [walingane sawasawa] kama mafisadi katika ardhi? Au Tuwajaalie wenye taqwa kama [sawa] na waovu?” (38:28)

وَلَيْسَ الذَّكَرُ كَالْأُنثَىٰ
“Na mwanamme si kama mwanamke.” (03:36)

تِلْكَ إِذًا قِسْمَةٌ ضِيزَىٰ
“Huo ni mgawanyo si wa uadilifu.” (53:22)

Mzungumzaji: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
Chanzo: Naswaaih wa Fadhwaaih, uk. 50-51
Toleo la: 17-12-2014
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com


  • Kitengo: Uncategorized , ´Abdul-Khaaliq, ´Abdur-Rahmaan
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Wednesday 17th, December 2014