Kutoka Kwenye Mwanga Na Kwenda Kwenye Moto

Mche Allaah na hakikisha unakuja katika duruus. Mche Allaah na hakikisha unashirikiana katika wema na uchaji Allaah. Pateni mafunzo kutoka Dammaaj, msingi wa Maraakiz zote. Pateni mafunzo kutoka Dammaaj, msingi wenu. Vipi ilikuwa wakati wa uhai wa Shaykh Muqbil (Rahimahu Allaah)? Ilikuwa ni mwanga. Haikuwa moto. Kulikuwa urafiki, mapenzi, kupendana, rahmah, uelewa, elimu, matendo, kufunza, wema, kuunga udugu, kulingania katika Dini ya Allaah na mengineyo. Ilikuwa vipi wakati alipokuja al-Hajuuriy? Alifanya nini? Aliichoma, kuirarua na kuiharibu. Dammaaj iliangamia kabla ya kuja Huuthiyyah. Dammaaj ilikuwa imeshaharibiwa kabla ya kuja Huuthiyyah. Watu walikuwa wamegawanyika na wamejigawa wao kwa wao. Kulikuwa matusi, laana, upondaji, kupigana, kususana, utahadharisho, kuwatukana wanachuoni na fatwa pasina dalili au msingi. Alipewa nasaha, lakini hakujali. Huuthiyyah wamekuja kipindi cha mwisho wakati Dammaaj tayari ilikuwa imeshaangamia. Kulikuwa kumebaki wachache sana na walikuwa chini ya ukandamizaji na kutishwa. Tunajiweka mbali kwa Allaah kutokana na aliyosababisha al-Hajuuriy katika Da´wah. Ni tokea lini nimesema kuwa al-Hajuuriy hawakilishi Da´wah, Ahl-us-Sunnah, Uislamu wala wanachuoni? Anajiwakilisha yeye mwenyewe tu. Nilisema hivi tangu Dammaaj ilipokuwa na nguvu na bado ninasema hivi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: “Allaah! Mimi najiweka mbali na matendo ya Khaalid mbele Yako!” (al-Bukhaariy (4339) Ni nani Khaalid! Ni Swahabah mtukufu Khaalid bin al-Waliyd (Radhiya Allaahu ´anhu). Alifanya kosa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawa amesema hivi: “Allaah! Mimi najiweka mbali na matendo ya Khaalid mbele Yako!” Tusisemi sisi hivi kuhusu al-Hajuuriy? Ninaapa kwa Allaah ya kwamba al-Hajuuriy hawezi kulinganishwa na Khaalid (Radhiya Allaahu ´anhu). al-Hajuuriy amefanya mamia ya makosa, ikiwa sio maelfu, wakati Khaalid kosa lake lilikuwa limoja tu. Pamoja na hivyo unajua Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwamba unajiweka mbali na kosa mbele ya Allaah. Haijalishi hata kama mtu huyo unampenda. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anafanyia kazi Aayah Tukufu mwishoni mwa Suurat “ash-Shu´araa”: فَإِنْ عَصَوْكَ فَقُلْ إِنِّي بَرِيءٌ مِّمَّا تَعْمَلُونَ ”Wakikuasi; basi sema: “Hakika mimi niko mbali na hayo mnayoyatenda.” (26:216) Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anatendea kazi Qur-aan. Ni yeye ndiye alisema: “Allaah! Mimi najiweka mbali na matendo ya Khaalid mbele Yako!” Amesema hivo kwa kosa moja. al-Hajuuriy ni makosa mangapi ametumbukia ndani yake na ni masuala mangapi? Haihusiani na Da´wah tu. Amesababisha machukizo baina ya watu, wanafunzi, makabila, wanachuoni, wakuu wa makabila, nchi na wakuu wa nchi na amefanya yakufanya. Wanafunzi! Mcheni Allaah juu ya nafsi zenu. Hatutaki kuwa na mtu al-Hajuuriy wa pili. Zingatieni. Ninaapa kwa Allaah ya kwamba hatutaki kuwa na mtu al-Hajuuriy wa pili anayekuja na hili na lile na kutoa fatwa kutoka kwenye kichwa chake. Mwandishi: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Waswaabiy Chanzo: Dammaaj - Ja´aluuhaa Shu´lah min Naar ba´d an kaanat Shu´lah min Nuur, uk. 8-10 Imefasiriwa na: Wanachuoni.com

Mche Allaah na hakikisha unakuja katika duruus. Mche Allaah na hakikisha unashirikiana katika wema na uchaji Allaah. Pateni mafunzo kutoka Dammaaj, msingi wa Maraakiz zote. Pateni mafunzo kutoka Dammaaj, msingi wenu. Vipi ilikuwa wakati wa uhai wa Shaykh Muqbil (Rahimahu Allaah)? Ilikuwa ni mwanga. Haikuwa moto. Kulikuwa urafiki, mapenzi, kupendana, rahmah, uelewa, elimu, matendo, kufunza, wema, kuunga udugu, kulingania katika Dini ya Allaah na mengineyo.

Ilikuwa vipi wakati alipokuja al-Hajuuriy? Alifanya nini? Aliichoma, kuirarua na kuiharibu. Dammaaj iliangamia kabla ya kuja Huuthiyyah. Dammaaj ilikuwa imeshaharibiwa kabla ya kuja Huuthiyyah. Watu walikuwa wamegawanyika na wamejigawa wao kwa wao. Kulikuwa matusi, laana, upondaji, kupigana, kususana, utahadharisho, kuwatukana wanachuoni na fatwa pasina dalili au msingi. Alipewa nasaha, lakini hakujali. Huuthiyyah wamekuja kipindi cha mwisho wakati Dammaaj tayari ilikuwa imeshaangamia. Kulikuwa kumebaki wachache sana na walikuwa chini ya ukandamizaji na kutishwa.

Tunajiweka mbali kwa Allaah kutokana na aliyosababisha al-Hajuuriy katika Da´wah. Ni tokea lini nimesema kuwa al-Hajuuriy hawakilishi Da´wah, Ahl-us-Sunnah, Uislamu wala wanachuoni? Anajiwakilisha yeye mwenyewe tu. Nilisema hivi tangu Dammaaj ilipokuwa na nguvu na bado ninasema hivi.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah! Mimi najiweka mbali na matendo ya Khaalid mbele Yako!” (al-Bukhaariy (4339)

Ni nani Khaalid! Ni Swahabah mtukufu Khaalid bin al-Waliyd (Radhiya Allaahu ´anhu). Alifanya kosa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawa amesema hivi:

“Allaah! Mimi najiweka mbali na matendo ya Khaalid mbele Yako!”

Tusisemi sisi hivi kuhusu al-Hajuuriy? Ninaapa kwa Allaah ya kwamba al-Hajuuriy hawezi kulinganishwa na Khaalid (Radhiya Allaahu ´anhu). al-Hajuuriy amefanya mamia ya makosa, ikiwa sio maelfu, wakati Khaalid kosa lake lilikuwa limoja tu. Pamoja na hivyo unajua Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwamba unajiweka mbali na kosa mbele ya Allaah. Haijalishi hata kama mtu huyo unampenda. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anafanyia kazi Aayah Tukufu mwishoni mwa Suurat “ash-Shu´araa”:
فَإِنْ عَصَوْكَ فَقُلْ إِنِّي بَرِيءٌ مِّمَّا تَعْمَلُونَ

”Wakikuasi; basi sema: “Hakika mimi niko mbali na hayo mnayoyatenda.” (26:216)
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anatendea kazi Qur-aan. Ni yeye ndiye alisema:

“Allaah! Mimi najiweka mbali na matendo ya Khaalid mbele Yako!”

Amesema hivo kwa kosa moja. al-Hajuuriy ni makosa mangapi ametumbukia ndani yake na ni masuala mangapi? Haihusiani na Da´wah tu. Amesababisha machukizo baina ya watu, wanafunzi, makabila, wanachuoni, wakuu wa makabila, nchi na wakuu wa nchi na amefanya yakufanya.

Wanafunzi! Mcheni Allaah juu ya nafsi zenu. Hatutaki kuwa na mtu al-Hajuuriy wa pili. Zingatieni. Ninaapa kwa Allaah ya kwamba hatutaki kuwa na mtu al-Hajuuriy wa pili anayekuja na hili na lile na kutoa fatwa kutoka kwenye kichwa chake.

Mwandishi: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Waswaabiy
Chanzo: Dammaaj – Ja´aluuhaa Shu´lah min Naar ba´d an kaanat Shu´lah min Nuur, uk. 8-10
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com


  • Kitengo: Uncategorized , al-Hajuuriy, Yahyaa
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Saturday 12th, April 2014