Kutofautiana Kwa Ahl-us-Sunnah Juu Ya Ubora Wa ´Uthmaan Na ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhumaa)

Miongoni mwa Makhaliyfah waongofu wane, mbora zaidi ni Abu Bakr, kisha ´Umar. Hili ni kwa Ijmaa´ ya Waislamu. Wakatofautiana kati ya ´Aliy na ´Uthmaan ni nani mbora zaidi? Kundi la watu likamfadhilisha ´Uthmaan, kundi lingine likamfadhilisha ´Aliy na kundi la tatu likasimama katika ubora (halikusema kitu). Ama katika uongozi Ummah umekubaliana ya kuwa uongozi baada ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni Abu Bakr, kisha ´Umar, kisha ´Uthmaan kisha ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhum). Wamekubaliana kuwa huu ndio mpangilio wa uongozi kwa Ijmaa´. Anasema Shaykh-ul-Islaam (Rahimahu Allaah) katika “al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah”: “Atakayekashifu uongozi wa mmoja katika maimamu hawa, basi ni mpotevu kuliko punda wake.” Kuna tofauti kati ya masuala ya ubora na masuala ya uongozi. Katika masuala ya ubora Waislamu wamekubaliana kwamba mbora wao ni Abu Bakr na halafu ´Umar, wakatofautiana juu ya ´Aliy na ´Uthmaan ni nani mbora zaidi kuliko mwingine. Sahihi ni kwamba ´Uthmaan ni mbora zaidi. Hili halina shaka kuwa ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anhu) ni mbora zaidi. Kwa dalili ya kwamba Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) katika mashauriano walimtanguliza ´Uthmaan juu ya ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhumaa). Masuala ya kufadhilisha baina ya ´Uthmaan na ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ni jambo sahali, lakini kukashifu (kutukana) uongozi ni jambo la upotevu. Kwa kuwa Raafidhwah wanasema kwamba anayestahiki uongozi baada ya Mtume wa Allaah ni ´Aliy na yeye ndiye muusiwa. Wanasema kwamba Maswahabah walimdhulumu na wakampokonya uongozi. Vilevile wanamlaani Abu Bakr na ´Umar na wanawaita kuwa ni masanamu ya ki-Quraysh. Hili bila ya shaka ni upotevu, ukafiri na kwenda kinyume na Ijmaa´. Anayestahiki kuwa Khaliyfah baada ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni Abu Bakr, kisha ´Umar, kisha ´Uthmaan kisha ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhum). Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Abiy Daawuud as-Sijistaaniy Chanzo: al-Haaiyyah Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan Chanzo: "Sharh al-Haaiyyah", uk. 115-116

Miongoni mwa Makhaliyfah waongofu wane, mbora zaidi ni Abu Bakr, kisha ´Umar. Hili ni kwa Ijmaa´ ya Waislamu. Wakatofautiana kati ya ´Aliy na ´Uthmaan ni nani mbora zaidi? Kundi la watu likamfadhilisha ´Uthmaan, kundi lingine likamfadhilisha ´Aliy na kundi la tatu likasimama katika ubora (halikusema kitu).

Ama katika uongozi Ummah umekubaliana ya kuwa uongozi baada ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni Abu Bakr, kisha ´Umar, kisha ´Uthmaan kisha ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhum). Wamekubaliana kuwa huu ndio mpangilio wa uongozi kwa Ijmaa´. Anasema Shaykh-ul-Islaam (Rahimahu Allaah) katika “al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah”:

“Atakayekashifu uongozi wa mmoja katika maimamu hawa, basi ni mpotevu kuliko punda wake.”

Kuna tofauti kati ya masuala ya ubora na masuala ya uongozi. Katika masuala ya ubora Waislamu wamekubaliana kwamba mbora wao ni Abu Bakr na halafu ´Umar, wakatofautiana juu ya ´Aliy na ´Uthmaan ni nani mbora zaidi kuliko mwingine. Sahihi ni kwamba ´Uthmaan ni mbora zaidi. Hili halina shaka kuwa ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anhu) ni mbora zaidi. Kwa dalili ya kwamba Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) katika mashauriano walimtanguliza ´Uthmaan juu ya ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhumaa).

Masuala ya kufadhilisha baina ya ´Uthmaan na ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ni jambo sahali, lakini kukashifu (kutukana) uongozi ni jambo la upotevu. Kwa kuwa Raafidhwah wanasema kwamba anayestahiki uongozi baada ya Mtume wa Allaah ni ´Aliy na yeye ndiye muusiwa. Wanasema kwamba Maswahabah walimdhulumu na wakampokonya uongozi. Vilevile wanamlaani Abu Bakr na ´Umar na wanawaita kuwa ni masanamu ya ki-Quraysh. Hili bila ya shaka ni upotevu, ukafiri na kwenda kinyume na Ijmaa´. Anayestahiki kuwa Khaliyfah baada ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni Abu Bakr, kisha ´Umar, kisha ´Uthmaan kisha ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhum).

Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Abiy Daawuud as-Sijistaaniy
Chanzo: al-Haaiyyah
Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: “Sharh al-Haaiyyah”, uk. 115-116


  • Kitengo: Uncategorized , Salafiyyah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Monday 17th, February 2014