Kusoma Suurah Tatu Ambazo Zimezoeleka Na Qunuut Baada Ya Rukuu Katika Swalah Ya Witr

Mmeona tuliyofanya katika Swalah kwa kusoma Suurah ambazo hazikuzoeleka kusomwa na ambazo ndio Sunnah. Tumefanya hivo ili iweze kuwabainikia watu ya kwamba kusoma Suurat-ul-A´laa, Suurat-ul-Kaafiruun na Suurat-ul-Ikhlaasw sio kwa njia ya uwajibu, bali ni kwa njia ya mapendekezo. Kama jinsi sio miongoni mwa masharti ya Witr kusoma Qunuut, yaani kusoma Du´aa baada ya Rukuu. Witr inahusiana na mtu kuswali Swalah ya Witr, Rakaa moja, tatu, tano, saba, tisa au kumi na moja. Qunuut sio sharti ya kusihi kwa Witr. Mtu akisoma Qunuut ni sawa na lakini hata hivyo akiacha ni sawa pia kwa kuwa yote mawili yamethibiti katika Sunnah. Lakini katika Ramadhaan imependekezwa kwa mtu kudumu kuleta Du´aa kwa wingi hapa na hapa kwani ni katika sababu za kuitikiwa Du´aa. Ama nje ya Ramadhaan bora zaidi mtu asidumu kuleta Qunuut, yaani kuleta Du´aa baada ya Rukuu. Mzungumzaji: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn Chanzo: Mkanda "Liqaa´aatu Ramadhwaaniyyah", sehemu ya 01 Toleo la: 19-07-2014 Imefasiriwa na: Wanachuoni.com

Mmeona tuliyofanya katika Swalah kwa kusoma Suurah ambazo hazikuzoeleka kusomwa na ambazo ndio Sunnah. Tumefanya hivo ili iweze kuwabainikia watu ya kwamba kusoma Suurat-ul-A´laa, Suurat-ul-Kaafiruun na Suurat-ul-Ikhlaasw sio kwa njia ya uwajibu, bali ni kwa njia ya mapendekezo. Kama jinsi sio miongoni mwa masharti ya Witr kusoma Qunuut, yaani kusoma Du´aa baada ya Rukuu. Witr inahusiana na mtu kuswali Swalah ya Witr, Rakaa moja, tatu, tano, saba, tisa au kumi na moja. Qunuut sio sharti ya kusihi kwa Witr. Mtu akisoma Qunuut ni sawa na lakini hata hivyo akiacha ni sawa pia kwa kuwa yote mawili yamethibiti katika Sunnah. Lakini katika Ramadhaan imependekezwa kwa mtu kudumu kuleta Du´aa kwa wingi hapa na hapa kwani ni katika sababu za kuitikiwa Du´aa. Ama nje ya Ramadhaan bora zaidi mtu asidumu kuleta Qunuut, yaani kuleta Du´aa baada ya Rukuu.

Mzungumzaji: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Chanzo: Mkanda “Liqaa´aatu Ramadhwaaniyyah”, sehemu ya 01
Toleo la: 19-07-2014
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com


  • Kitengo: Uncategorized , Tahajjud, Tarawiyh, Qiyaam-ul-Layl & Witr
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Saturday 19th, July 2014