Kurefusha Nywele Kwa Mwanaume

Kurefusha nywele ni katika mambo ya kiada na mubaha, kwa sharti asizifanye zikawa zinafanana na makafiri. Akafanya kichwa chake kama wanavyofanya makafiri. Ama kuzirefusha mpaka mabegani, kama jinsi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyokuwa akifanya au zaidi ya hapo, hakuna ubaya. Lakini asizifanye kwa sifa ambayo zinafanana na makafiri. Kuna tanbihi. Ikishakuwa kuzirefusha nywele kunachukuliwa kama ash-Shuhrah na kuwafanya watu wakapata dhana mbaya kwako, kwa kuwa hivi leo imekuwa wale wanaorefusha nywele - kama mnavyojua - huenda akatuhumiwa. Ewe ndugu! Usijijaalie katika nafsi yako tuhuma. Nyoa kama watu wengine.

Kurefusha nywele ni katika mambo ya kiada na mubaha, kwa sharti asizifanye zikawa zinafanana na makafiri. Akafanya kichwa chake kama wanavyofanya makafiri. Ama kuzirefusha mpaka mabegani, kama jinsi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyokuwa akifanya au zaidi ya hapo, hakuna ubaya. Lakini asizifanye kwa sifa ambayo zinafanana na makafiri.

Kuna tanbihi. Ikishakuwa kuzirefusha nywele kunachukuliwa kama ash-Shuhrah na kuwafanya watu wakapata dhana mbaya kwako, kwa kuwa hivi leo imekuwa wale wanaorefusha nywele – kama mnavyojua – huenda akatuhumiwa. Ewe ndugu! Usijijaalie katika nafsi yako tuhuma. Nyoa kama watu wengine.