Kupita Mbele Ya Mwenye Kuswali Kwa Nguvu

Swali: Mtu anaswali mbele yake kukapita mwanaume akamzuia lakini akapita, je swalah yake inabatilika kwa hilo? ´Allaamah al-Fawzaan: Hapana, swalah yake haibatiliki. Lakini aliepita anapata dhambi kubwa. Na mwenye kuswali hana juu yake kitu kwa kuwa alimzuia lakini akapita. Dhambi ni za yule aliepita. [Anasema Mtume]: "Angelijua yule mwenye kupita mbele ya mwenye kuswali ana nini juu yake, ingekuwa bora kwake kusimama arubaini kuliko kupita mbele yake." Swali La Pili: Akipita mwanamke mbele ya mwanaume katika swalah yake, je swalah yake inabatilika kwa hilo? ´Allaamah al-Fawzaan: Kauli sahihi ni kuwa swalah yake haibatiliki; sawa akipita mwanamke, mbwa wala punda isipokuwa makusudio hapa ni kupungua thawabu na si kubatilika. Madhehebu ya Imaam Ahmad ndio inabatilika kwa kupita vitu hivi vitatu; mwanamke, mbwa mweusi na punda. Lakini jumhuri - na ni moja ya upokezi wa Ahmad, kuwa makusudio kubatilika hapa ni kupungua thawabu. Bali madhehebu ya Ahmad wanaona kuwa swalah inabatilika kwa kupita mbwa mweusi tu. Haibatiliki kwa kupita mwanamke na punda, bali ni mbwa mweusi tu.

Swali:
Mtu anaswali mbele yake kukapita mwanaume akamzuia lakini akapita, je swalah yake inabatilika kwa hilo?

´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana, swalah yake haibatiliki. Lakini aliepita anapata dhambi kubwa. Na mwenye kuswali hana juu yake kitu kwa kuwa alimzuia lakini akapita. Dhambi ni za yule aliepita.
[Anasema Mtume]:
“Angelijua yule mwenye kupita mbele ya mwenye kuswali ana nini juu yake, ingekuwa bora kwake kusimama arubaini kuliko kupita mbele yake.”

Swali La Pili:
Akipita mwanamke mbele ya mwanaume katika swalah yake, je swalah yake inabatilika kwa hilo?

´Allaamah al-Fawzaan:
Kauli sahihi ni kuwa swalah yake haibatiliki; sawa akipita mwanamke, mbwa wala punda isipokuwa makusudio hapa ni kupungua thawabu na si kubatilika. Madhehebu ya Imaam Ahmad ndio inabatilika kwa kupita vitu hivi vitatu; mwanamke, mbwa mweusi na punda. Lakini jumhuri – na ni moja ya upokezi wa Ahmad, kuwa makusudio kubatilika hapa ni kupungua thawabu. Bali madhehebu ya Ahmad wanaona kuwa swalah inabatilika kwa kupita mbwa mweusi tu. Haibatiliki kwa kupita mwanamke na punda, bali ni mbwa mweusi tu.