Kuongea (Kuzungumza) Kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala)

Allaah (Jalla wa ´Alaa) katika Sifa Zake za Kimatendo ni kwamba Anaongea. Kama ambavyo Anaumba, Anaruzuku, Anahuisha, Anafisha, Anayaendesha mambo, Anapenda na Kutaka (Subhaanahu wa Ta´ala). Vilevile Anaongea kwa Maneno yanayolingana na Utukufu na Ukubwa Wake – kama zilivyo Sifa Zake zingine zote – Anaongea pale Anapotaka, kwa yale Anayotaka na Anapotaka. Maneno Yake ni ya tokea zamani, hadiyth-ul-Ahaad, bi maana Anaongea pale Anapotaka. Aliongea kwa Qur-aan wakati ilipoteremka, Akamuongelesha Jibriyl, Akamuongelesha Muusa, Akamuongelesha Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) usiku wa Israa´. Kabla ya hapo Alimuongelesha Aadam (´alayhis-Salaam) na Ataongea siku ya Qiyaamah kwa kuwahesabu watu, Atawaongelesha waumini Peponi na wao watamuongelesha. Hivyo Yeye Anaongea kwa Maneno ya milele yasiyokuwa na mwanzo kama Sifa zingine na Maneno Yake ni hadiyth-ul-Ahaad. Vilevile vitabu vingine vyote vilivyoteremshwa kwa Mitume, vyote ni Maneno ya Allaah (Jalla wa ´Alaa). Katika hivyo ni pamoja na Qur-aan Tukufu ambayo ndio babu kubwa yao na Allaah Akaifanya (Qur-aan) kuyalinda. Hivyo ni Maneno Yake (Jalla wa ´Alaa) ya hakika na sio Majaaz, ya mafumbo, yameteremshwa kutoka Kwake na hayakuumbwa. Haya ndio madhehebu ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah na wanasema hilo wazi wazi. Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy Chanzo: al-Haaiyyah Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan Chanzo: "Sharh al-Haaiyyah", uk. 69

Allaah (Jalla wa ´Alaa) katika Sifa Zake za Kimatendo ni kwamba Anaongea. Kama ambavyo Anaumba, Anaruzuku, Anahuisha, Anafisha, Anayaendesha mambo, Anapenda na Kutaka (Subhaanahu wa Ta´ala). Vilevile Anaongea kwa Maneno yanayolingana na Utukufu na Ukubwa Wake – kama zilivyo Sifa Zake zingine zote – Anaongea pale Anapotaka, kwa yale Anayotaka na Anapotaka. Maneno Yake ni ya tokea zamani, hadiyth-ul-Ahaad, bi maana Anaongea pale Anapotaka. Aliongea kwa Qur-aan wakati ilipoteremka, Akamuongelesha Jibriyl, Akamuongelesha Muusa, Akamuongelesha Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) usiku wa Israa´. Kabla ya hapo Alimuongelesha Aadam (´alayhis-Salaam) na Ataongea siku ya Qiyaamah kwa kuwahesabu watu, Atawaongelesha waumini Peponi na wao watamuongelesha. Hivyo Yeye Anaongea kwa Maneno ya milele yasiyokuwa na mwanzo kama Sifa zingine na Maneno Yake ni hadiyth-ul-Ahaad.

Vilevile vitabu vingine vyote vilivyoteremshwa kwa Mitume, vyote ni Maneno ya Allaah (Jalla wa ´Alaa). Katika hivyo ni pamoja na Qur-aan Tukufu ambayo ndio babu kubwa yao na Allaah Akaifanya (Qur-aan) kuyalinda. Hivyo ni Maneno Yake (Jalla wa ´Alaa) ya hakika na sio Majaaz, ya mafumbo, yameteremshwa kutoka Kwake na hayakuumbwa. Haya ndio madhehebu ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah na wanasema hilo wazi wazi.

Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy
Chanzo: al-Haaiyyah
Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: “Sharh al-Haaiyyah”, uk. 69


  • Kitengo: Uncategorized , Maneno ya Allaah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Thursday 13th, February 2014