Kunyoa Ndevu Ni Kujifananisha Na Wanawake Na Ni Laana

Haijuzu kwa mwanaume kujifananisha na wanawake katika mavazi yao, kutembea kwao, kuongea kwao, kujipendezesha kwao wanawake. Haijuzu kwake hilo kwa kuwa yeye ni mwanamume. Yahitajika kwake nguvu na ukakamavu, hakuhitajiki kwake ulaini na kujiachia achia hivi ilihali ni mwanaume. Asifike kwa sifa za wanaume. Kadhalika katika kujifananisha na wanawake ni kunyoa ndevu, hii ni aina kubwa katika aina za kujifananisha na wanawake, kunyoa ndevu akawa mwanaume kama mwanamke... Kitu kinachomtofautisha mwanaume na mwanamke ni ndevu, hivyo [mwanaume] akinyoa ndevu zake huwezi kutofautisha kati ya uso wa mwanamke na uso wa mwanamume. Inatoweka alama inayowapambanua. Huku ni kujifananisha wanaume kwa wanawake. Allaah Kamuumba nazo mwanaume na kumnyima nazo mwanamke. Hivyo kamlaani Mtume صلي الله عليه وسلم anaelifanya, na laana ni dalili ya kuonesha kuwa ni dhambi kubwa katika madhambi makubwa. Ni wajibu kwa wanaume kujitofautisha na wanawake, na ni wajibu kwa wanawake kujitofautisha na wanaume. Huu ndo wajibu. وَلَيْسَ الذَّكَرُ كَالأُنثَى “Na mwanamume si sawa na mwanamke.” (al-´Imraan 03:36). Ama akiwa mwanamume kama mwanamke au mwanamke kama mwanamume, hali itabadilika - Laa Hawla walaa Quwwata illa biLlaah. Na yeye kajifananisha na sifa ya wanawake. Lakini ukimwambia wewe ni kama mwanamke atakukasirikia au anaweza hata kukuua, ukimwambia [mnyoa ndevu] wewe ni kama mwanamke, atakuua au atakupiga. Ilihali yeye mwenyewe ndo anafanya jambo hili, anakuwa kama mwanamke.

Haijuzu kwa mwanaume kujifananisha na wanawake katika mavazi yao, kutembea kwao, kuongea kwao, kujipendezesha kwao wanawake. Haijuzu kwake hilo kwa kuwa yeye ni mwanamume. Yahitajika kwake nguvu na ukakamavu, hakuhitajiki kwake ulaini na kujiachia achia hivi ilihali ni mwanaume. Asifike kwa sifa za wanaume.
Kadhalika katika kujifananisha na wanawake ni kunyoa ndevu, hii ni aina kubwa katika aina za kujifananisha na wanawake, kunyoa ndevu akawa mwanaume kama mwanamke…

Kitu kinachomtofautisha mwanaume na mwanamke ni ndevu, hivyo [mwanaume] akinyoa ndevu zake huwezi kutofautisha kati ya uso wa mwanamke na uso wa mwanamume. Inatoweka alama inayowapambanua. Huku ni kujifananisha wanaume kwa wanawake.

Allaah Kamuumba nazo mwanaume na kumnyima nazo mwanamke. Hivyo kamlaani Mtume صلي الله عليه وسلم anaelifanya, na laana ni dalili ya kuonesha kuwa ni dhambi kubwa katika madhambi makubwa. Ni wajibu kwa wanaume kujitofautisha na wanawake, na ni wajibu kwa wanawake kujitofautisha na wanaume. Huu ndo wajibu.

وَلَيْسَ الذَّكَرُ كَالأُنثَى
“Na mwanamume si sawa na mwanamke.” (al-´Imraan 03:36).

Ama akiwa mwanamume kama mwanamke au mwanamke kama mwanamume, hali itabadilika – Laa Hawla walaa Quwwata illa biLlaah. Na yeye kajifananisha na sifa ya wanawake.
Lakini ukimwambia wewe ni kama mwanamke atakukasirikia au anaweza hata kukuua, ukimwambia [mnyoa ndevu] wewe ni kama mwanamke, atakuua au atakupiga. Ilihali yeye mwenyewe ndo anafanya jambo hili, anakuwa kama mwanamke.