Kumpiga Mwanamke Ni Katika Tabia Mbaya

Shaykh Muhammad al-Madkhaliy: Enyi ndugu! Kumpiga mwanamke, hata kama imeruhusiwa lakini sio kitu kinachopendwa. Sio kitu kinachopendwa kwa wanaume watukufu, masharifu wao na wabora wao. Na kwa ajili hii, kasema ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anha): "Hajawahi kumpiga Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mwanamke kwa mkono wake wala mtumwa, wala kulipiza kisasi kwa ajili yake mwenyewe, isipokuwa tu kunapovukwa mipaka ya Allaah, hapo hulipiza kisasi kwa ajili ya Allaah." Hakuwahi Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumpiga mwanamke. Kwa hivyo, kuwapiga wanawake ni jambo linalochukiza kwa wanaume wenye akili, watukufu, masharifu, wenye fadhila na waliyo juu katika wao. Hili ni jambo linalochukizwa kwao. Na kwa ajili hii, alisisitiza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) maana hii [ya kutowapiga], pamoja na kwamba imeruhusiwa. Akasema: "Mmoja wenu asimpige mijeledi mwanamke wake kama anavyompiga mijeledi mtumishi wake kisha (akataka) kulala nae." Katika upokezi mwingine: "... mwanzoni mwa siku kisha (akataka) kulala nae mwisho wa siku." Vipi, kwa Jina la Allaah, utampiga na kumpa mijeledi kama unavyompiga mtumwa kisha wataka aje katika kitanda chako? Hili haliwezekani. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katahadharisha tabia kama hii mbaya. Hata kama imeruhusiwa kumpa adabu mwanamke: وَاللَّاتِي تَخَافُونَ نُشُوزَهُنَّ فَعِظُوهُنَّ وَاهْجُرُوهُنَّ فِي الْمَضَاجِعِ وَاضْرِبُوهُنَّ "Na wale (wanawake) ambao mnakhofu uasi wao, basi waonyeni na (wakiendelea uasi) wahameni katika malazi (vitanda) na (mwishowe wakishikilia uasi) wapigeni." (an-Nisaa 04 : 34) [Allaah] Akafanya kupiga ndio iwe dawa ya mwisho. Pamoja na hivyo, kipigo hichi kimefundishwa ni namna gani kwa wanachuoni; ya kwamba iwe ni pigo khafifu ambacho hakitomvunja wala kumuachia jeraha. Usimpige ukamuumiza jicho lake kisha jicho lake likatoka. Au ukampiga kwenye sikio lake kiwambo chake kikaharibika. Hili halijuzu. Na kupiga kwenye uso ni Haramu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kalikataza. Pamoja na hivyo, mahakamani unasikia daima mashtaka ya wanaume kuwapiga wanawake; na hii ni tabia mbaya ambayo katahadharisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa hili mlilosikia: "Mmoja wenu asimpige mijeledi mwanamke wake kama anavyompiga mijeledi mtumishi wake au kama mja kisha (akataka) kulala nae."

Shaykh Muhammad al-Madkhaliy:

Enyi ndugu! Kumpiga mwanamke, hata kama imeruhusiwa lakini sio kitu kinachopendwa. Sio kitu kinachopendwa kwa wanaume watukufu, masharifu wao na wabora wao. Na kwa ajili hii, kasema ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anha):

“Hajawahi kumpiga Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mwanamke kwa mkono wake wala mtumwa, wala kulipiza kisasi kwa ajili yake mwenyewe, isipokuwa tu kunapovukwa mipaka ya Allaah, hapo hulipiza kisasi kwa ajili ya Allaah.”

Hakuwahi Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumpiga mwanamke. Kwa hivyo, kuwapiga wanawake ni jambo linalochukiza kwa wanaume wenye akili, watukufu, masharifu, wenye fadhila na waliyo juu katika wao. Hili ni jambo linalochukizwa kwao. Na kwa ajili hii, alisisitiza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) maana hii [ya kutowapiga], pamoja na kwamba imeruhusiwa. Akasema:

“Mmoja wenu asimpige mijeledi mwanamke wake kama anavyompiga mijeledi mtumishi wake kisha (akataka) kulala nae.”

Katika upokezi mwingine:

“… mwanzoni mwa siku kisha (akataka) kulala nae mwisho wa siku.”

Vipi, kwa Jina la Allaah, utampiga na kumpa mijeledi kama unavyompiga mtumwa kisha wataka aje katika kitanda chako? Hili haliwezekani. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katahadharisha tabia kama hii mbaya. Hata kama imeruhusiwa kumpa adabu mwanamke:

وَاللَّاتِي تَخَافُونَ نُشُوزَهُنَّ فَعِظُوهُنَّ وَاهْجُرُوهُنَّ فِي الْمَضَاجِعِ وَاضْرِبُوهُنَّ
“Na wale (wanawake) ambao mnakhofu uasi wao, basi waonyeni na (wakiendelea uasi) wahameni katika malazi (vitanda) na (mwishowe wakishikilia uasi) wapigeni.” (an-Nisaa 04 : 34)

[Allaah] Akafanya kupiga ndio iwe dawa ya mwisho. Pamoja na hivyo, kipigo hichi kimefundishwa ni namna gani kwa wanachuoni; ya kwamba iwe ni pigo khafifu ambacho hakitomvunja wala kumuachia jeraha. Usimpige ukamuumiza jicho lake kisha jicho lake likatoka. Au ukampiga kwenye sikio lake kiwambo chake kikaharibika. Hili halijuzu. Na kupiga kwenye uso ni Haramu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kalikataza. Pamoja na hivyo, mahakamani unasikia daima mashtaka ya wanaume kuwapiga wanawake; na hii ni tabia mbaya ambayo katahadharisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa hili mlilosikia:

“Mmoja wenu asimpige mijeledi mwanamke wake kama anavyompiga mijeledi mtumishi wake au kama mja kisha (akataka) kulala nae.”


  • Author: Shaykh Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Kitengo: Uncategorized , Jamii
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Saturday 19th, October 2013