Kujinasibisha Na Salafiyyah Ni Jambo Lenye Kusifika Na Zuri

Katika ukurasa wa 236 al-Buutwiy ameandika kichwa cha khabari “Salafiyyah kama madhehebu ni Bid´ah". Kauli kama hii inasababisha uchanganyikiwaji na mshangao. Vipi ni Bid´ah kuwa na Salafiyyah kama madhehebu na wakati Bid´ah ni upotevu? Vipi itakuwa ni Bid´ah kufuata madhehebu ya Salaf wakati kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah ni wajibu kuifuata na wakati madhehebu haya kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah ni haki na uongofu? Allaah (Ta´ala) Amesema: وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ “Na wale waliotangulia awali (katika Uislamu) miongoni mwa Muhaajiriyn (waliohajiri kutoka Makkah), na Answaar (wakaazi wa Madiynah waliowasaida na kuwanusuru Muhaajiriyn), na wale waliowafuata kwa ihsaan; Allaah Ameridhika nao, nao wameridhika Naye.” (09:100) Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema: "Shikamaneni na Sunnah zangu na Sunnah za Makhaliyfah wangu waongofu baada yangu.” Hivyo ni Sunnah, na sio Bid´ah, kuwa na Salaf kama madhehebu. Hata hivyo, ni Bid´ah kuwa na mfumo wa mtu mwengine. Ikiwa anamaanisha jina kwa dhati yake ni jipya, kama jinsi alivyosema, na kwamba halikuwa likijulikana hapo mwanzoni, basi ni Bid´ah kwa mtazamo huo. Pamoja na hivyo jina ni kitu sahali. Kosa huko halipelekei katika Bid´ah. Ikiwa anamaanisha wale wanaojinasibisha na jina hili wanafanya kosa linaloenda kinyume na mfumo wa Salaf, basi anatakiwa kubainisha kosa hilo bila ya kuvamia Salafiyyah. Kujiita “Salafiy” ni jambo lenye kusifika na jambo zuri ikiwa ina maana kuwa mtu anafuata mfumo wa Salaf na kukemea Bid´ah na ukhurafi. Mwandishi: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan Chanzo: al-Bayaan li Akhtwaa’ Ba´dhw-il-Kuttaab, uk. 156-157 Toleo la: 01-06-2014 Imefasiriwa na: Wanachuoni.com

Katika ukurasa wa 236 al-Buutwiy ameandika kichwa cha khabari “Salafiyyah kama madhehebu ni Bid´ah”. Kauli kama hii inasababisha uchanganyikiwaji na mshangao. Vipi ni Bid´ah kuwa na Salafiyyah kama madhehebu na wakati Bid´ah ni upotevu? Vipi itakuwa ni Bid´ah kufuata madhehebu ya Salaf wakati kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah ni wajibu kuifuata na wakati madhehebu haya kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah ni haki na uongofu?

Allaah (Ta´ala) Amesema:

وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ
“Na wale waliotangulia awali (katika Uislamu) miongoni mwa Muhaajiriyn (waliohajiri kutoka Makkah), na Answaar (wakaazi wa Madiynah waliowasaida na kuwanusuru Muhaajiriyn), na wale waliowafuata kwa ihsaan; Allaah Ameridhika nao, nao wameridhika Naye.” (09:100)

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:

“Shikamaneni na Sunnah zangu na Sunnah za Makhaliyfah wangu waongofu baada yangu.”

Hivyo ni Sunnah, na sio Bid´ah, kuwa na Salaf kama madhehebu. Hata hivyo, ni Bid´ah kuwa na mfumo wa mtu mwengine.

Ikiwa anamaanisha jina kwa dhati yake ni jipya, kama jinsi alivyosema, na kwamba halikuwa likijulikana hapo mwanzoni, basi ni Bid´ah kwa mtazamo huo. Pamoja na hivyo jina ni kitu sahali. Kosa huko halipelekei katika Bid´ah.

Ikiwa anamaanisha wale wanaojinasibisha na jina hili wanafanya kosa linaloenda kinyume na mfumo wa Salaf, basi anatakiwa kubainisha kosa hilo bila ya kuvamia Salafiyyah.

Kujiita “Salafiy” ni jambo lenye kusifika na jambo zuri ikiwa ina maana kuwa mtu anafuata mfumo wa Salaf na kukemea Bid´ah na ukhurafi.

Mwandishi: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: al-Bayaan li Akhtwaa’ Ba´dhw-il-Kuttaab, uk. 156-157
Toleo la: 01-06-2014
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com


  • Kitengo: Uncategorized , al-Buutwiy, Muhammad Sa´iyd Ramadhaan
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 1st, June 2014