Kuipamba Sauti Wakati Wa Kusoma Qur-aan

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema: “Ipambeni Qur-aan kwa sauti zenu.” Kinachotakikana kwa msomaji ni yeye aipambe sauti yake kwa (kuisoma) Qur-aan. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akipenda sauti nzuri kunaposomwa Qur-aan. Alikuwa anamsikiliza Abu Muusa al-Ash´ariy (Radhiya Allaahu ´anhu) wakati alipokuwa anaswali usiku, kwa kuwa Allaah Alikuwa amempa sauti nzuri. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anamsikiliza. Vilevile akamuamrisha ´Abdullaah bin Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anhu) amsomee na yeye huku anamsikiliza. Akasema: “Mimi napenda kuisikia kwa asiyekuwa mimi.” Akamsomea Suurat-un-Nisaa. Yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anapenda sauti nzuri kwa Qur-aan. Sauti nzuri ni neema kutoka kwa Allaah (´Azza wa Jalla). Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy Chanzo: al-Haaiyyah Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan Chanzo: "Sharh al-Haaiyyah", uk. 78

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema:

“Ipambeni Qur-aan kwa sauti zenu.”

Kinachotakikana kwa msomaji ni yeye aipambe sauti yake kwa (kuisoma) Qur-aan. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akipenda sauti nzuri kunaposomwa Qur-aan. Alikuwa anamsikiliza Abu Muusa al-Ash´ariy (Radhiya Allaahu ´anhu) wakati alipokuwa anaswali usiku, kwa kuwa Allaah Alikuwa amempa sauti nzuri. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anamsikiliza. Vilevile akamuamrisha ´Abdullaah bin Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anhu) amsomee na yeye huku anamsikiliza. Akasema:

“Mimi napenda kuisikia kwa asiyekuwa mimi.”

Akamsomea Suurat-un-Nisaa. Yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anapenda sauti nzuri kwa Qur-aan. Sauti nzuri ni neema kutoka kwa Allaah (´Azza wa Jalla).

Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy
Chanzo: al-Haaiyyah
Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: “Sharh al-Haaiyyah”, uk. 78


  • Kitengo: Uncategorized , Fiqh
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Friday 14th, February 2014