Kufanya Maulidi Ni Bid´ah

Bila ya shaka, kufanya Maulidi ni Bid´ah. Kwa hakika haya Maulidi hayajulikani kuwepo kwake katika uhai wa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wala katika uhai wa Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum), wala katika uhai wa Taabi´iyn, wala katika uhai wa maimamu wanne na wala uhai wa wanafunzi wao. Hayakujulikana katika ulimwengu wa Uislamu kitu kinachoitwa Maulidi kabisa. Sehemu ya kwanza yalipopatikana ni Misri, yalizusha na Faatwimiyyuun, dola iliokuwa chafu ya maovu: al-Baatwiniyyah. Na yalipoanza kusambaa, katika watu wa Ahl-us-Sunnah mtu wa kwanza alieanza kuyasambaza ni mfalme aitwae Irbil Iraaq kutokana na ujinga wake wa kuwaiga manaswara ambao na wao wanaadhimisha siku ya ´Iysa (´alayhis-Salaam). Wakakataza wanachuoni hilo. Yakaendelea kukua mpaka yakaenea leo katika ulimwengu wa Uislamu. Maulidi yanaingia katika maneno ya Mtume: “Na tahadharini na mambo ya kuzua, kwa hakika kila kitakachozushwa ni Bid´ah na kila Bid´ah ni upotevu." Na yanaingia katika maneno ya Mtume: "Atakayefanya ´amali isiyokuwa humo amri yetu, atarudishiwa." Mtu asijikurubishe kwa kitu anachokizingatia kuwa ni utiifu na kujikurubisha kwa Allaah isipokuwa kwa dalili. La sivyo atarudishiwa mwenyewe. Na kuichukulia siku hii kama ´Iyd, na pengine kukafanywa makubwa zaidi ya yanayofanywa katika ´Iyd. Mtume alipoenda Madiynah na walikuwa Answaar na siku ambazo wanasherehekea, akawaambia: "Allaah Amewapa badala ya sikukuu za Kijaahiliyyah, Amewapa ´Iyd-ul-Fitwr na ´Iyd-ul-Adhhaa."

Bila ya shaka, kufanya Maulidi ni Bid´ah. Kwa hakika haya Maulidi hayajulikani kuwepo kwake katika uhai wa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wala katika uhai wa Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum), wala katika uhai wa Taabi´iyn, wala katika uhai wa maimamu wanne na wala uhai wa wanafunzi wao. Hayakujulikana katika ulimwengu wa Uislamu kitu kinachoitwa Maulidi kabisa.

Sehemu ya kwanza yalipopatikana ni Misri, yalizusha na Faatwimiyyuun, dola iliokuwa chafu ya maovu: al-Baatwiniyyah.

Na yalipoanza kusambaa, katika watu wa Ahl-us-Sunnah mtu wa kwanza alieanza kuyasambaza ni mfalme aitwae Irbil Iraaq kutokana na ujinga wake wa kuwaiga manaswara ambao na wao wanaadhimisha siku ya ´Iysa (´alayhis-Salaam). Wakakataza wanachuoni hilo. Yakaendelea kukua mpaka yakaenea leo katika ulimwengu wa Uislamu. Maulidi yanaingia katika maneno ya Mtume:

“Na tahadharini na mambo ya kuzua, kwa hakika kila kitakachozushwa ni Bid´ah na kila Bid´ah ni upotevu.”
Na yanaingia katika maneno ya Mtume:

“Atakayefanya ´amali isiyokuwa humo amri yetu, atarudishiwa.”

Mtu asijikurubishe kwa kitu anachokizingatia kuwa ni utiifu na kujikurubisha kwa Allaah isipokuwa kwa dalili. La sivyo atarudishiwa mwenyewe. Na kuichukulia siku hii kama ´Iyd, na pengine kukafanywa makubwa zaidi ya yanayofanywa katika ´Iyd. Mtume alipoenda Madiynah na walikuwa Answaar na siku ambazo wanasherehekea, akawaambia:

“Allaah Amewapa badala ya sikukuu za Kijaahiliyyah, Amewapa ´Iyd-ul-Fitwr na ´Iyd-ul-Adhhaa.”