Kufanya ´Ibaadah Na Da´wah Pasina Elimu

Mtu anatakiwa kuanza kujifunza kabla ya kuzungumza na kutenda. Hii ni dalili inayoonesha hadhi ya elimu na kwamba mwenye kufanya ´ibaadah haijuzu kwake kuanza ´ibaadah isipokuwa baada ya elimu. Kadhalika mlinganizi, mwalimu na mwelekezaji, haijuzu kwake kuanza hilo isipokuwa baada ya elimu. Bi maana ni wajibu kwake kuwalingania watu kwa yale anayoyajua. Awashauri watu yale anayoyajua. Awafundishe watu yale anayoyajua. Kuhusu yale asiyoyajua aombe udhuru. Aseme “Allaah ndiye Anajua zaidi”. Ama kuhusu mfanya ´ibaadah ambaye anataka kumwabudu Allaah kwa ujinga na huku akipuuzia elimu kwa madai ya kwamba anataka kukimbilia kuwa katika safu za mbele na kuwasili Misikitini mapema na huku anapuuza elimu, huyu ametawaliwa na Shaytwaan na amemuweka mbali na elimu. Ni wajibu anasihiwe. Baadhi ya wale ambao wanajitahidi katika ´ibaadah, wakati huo huo wanapuuza kujifunza na wametosheka na yale waliyomo na wanajisifia na wakati huo huo wamedanganyika na kupatwa na ujeuri kwa ´ibaadah zao zilizojengeka juu ya ujinga. Ninasema maneno haya ili waweze kusikia baadhi ya watu wema ambao ni wapenda kufanya ´ibaadah ambao kwa kiasi kikubwa wako katika ujinga. Sivyo tu, bali huenda baadhi ya wageni wanapowaona katika safu za mbele wanafikiria kuwa ni katika wanafunzi. Hivyo wanawauliza maswali. Matokeo yake wanajibu kwa ujinga. Pengine anaweza kusikia aibu kusema “Sijui” na badala yake akatoa Fatwa kwa ujinga. Matokeo yake akapotea yeye na akawapoteza wengine. Kwa ajili hiyo, tunawanasihi ndugu zetu wapenda kufanya ´ibaadah watenge sehemu ya wakati wao katika kusoma na kufanya ´ibaadah. Wakati Allaah Anapowarahisishia mambo yao na wakawa ni wenye kumaliza kufanya ´ibaadah na hawana jambo linalowashughulisha, wagawanye wakati wao kati ya kufanya ´ibaadah na kusoma. Watilie umuhimu mkubwa wa kusoma. Watambue kuwa kusoma elimu ya Dini, kuhusu ´Aqiydah, mambo ya Ahkaam ni katika ´ibaadah pia. Kusoma elimu ya Dini ambayo ni ya Kishari´ah, ni katika ´ibaadah pia. ´Ibaadah ni aina nyingi. ´Ibaadah sio kuswali tu. ´Ibaadah sio kushindikiza jeneza tu. ´Ibaadah sio kukimbilia kuwa safu ya kwanza. Bali ´ibaadah ni aina nyingi. Zigawanye ´ibaadah zako na uanze kwa jambo ambalo ni muhimu zaidi. Jambo ambalo ni muhimu zaidi ni kusoma elimu. Soma elimu na elimu ndio itakuwekea wepesi wa kufanya ´ibaadah. Mwandishi: ´Allaamah Muhammad Amaan al-Jaamiy Chanzo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 11-12 Toleo la: 24-05-2014 Imefasiriwa na: Wanachuoni.com

Mtu anatakiwa kuanza kujifunza kabla ya kuzungumza na kutenda. Hii ni dalili inayoonesha hadhi ya elimu na kwamba mwenye kufanya ´ibaadah haijuzu kwake kuanza ´ibaadah isipokuwa baada ya elimu. Kadhalika mlinganizi, mwalimu na mwelekezaji, haijuzu kwake kuanza hilo isipokuwa baada ya elimu. Bi maana ni wajibu kwake kuwalingania watu kwa yale anayoyajua. Awashauri watu yale anayoyajua. Awafundishe watu yale anayoyajua. Kuhusu yale asiyoyajua aombe udhuru. Aseme “Allaah ndiye Anajua zaidi”.

Ama kuhusu mfanya ´ibaadah ambaye anataka kumwabudu Allaah kwa ujinga na huku akipuuzia elimu kwa madai ya kwamba anataka kukimbilia kuwa katika safu za mbele na kuwasili Misikitini mapema na huku anapuuza elimu, huyu ametawaliwa na Shaytwaan na amemuweka mbali na elimu. Ni wajibu anasihiwe. Baadhi ya wale ambao wanajitahidi katika ´ibaadah, wakati huo huo wanapuuza kujifunza na wametosheka na yale waliyomo na wanajisifia na wakati huo huo wamedanganyika na kupatwa na ujeuri kwa ´ibaadah zao zilizojengeka juu ya ujinga. Ninasema maneno haya ili waweze kusikia baadhi ya watu wema ambao ni wapenda kufanya ´ibaadah ambao kwa kiasi kikubwa wako katika ujinga.

Sivyo tu, bali huenda baadhi ya wageni wanapowaona katika safu za mbele wanafikiria kuwa ni katika wanafunzi. Hivyo wanawauliza maswali. Matokeo yake wanajibu kwa ujinga. Pengine anaweza kusikia aibu kusema “Sijui” na badala yake akatoa Fatwa kwa ujinga. Matokeo yake akapotea yeye na akawapoteza wengine.

Kwa ajili hiyo, tunawanasihi ndugu zetu wapenda kufanya ´ibaadah watenge sehemu ya wakati wao katika kusoma na kufanya ´ibaadah. Wakati Allaah Anapowarahisishia mambo yao na wakawa ni wenye kumaliza kufanya ´ibaadah na hawana jambo linalowashughulisha, wagawanye wakati wao kati ya kufanya ´ibaadah na kusoma. Watilie umuhimu mkubwa wa kusoma. Watambue kuwa kusoma elimu ya Dini, kuhusu ´Aqiydah, mambo ya Ahkaam ni katika ´ibaadah pia. Kusoma elimu ya Dini ambayo ni ya Kishari´ah, ni katika ´ibaadah pia. ´Ibaadah ni aina nyingi. ´Ibaadah sio kuswali tu. ´Ibaadah sio kushindikiza jeneza tu. ´Ibaadah sio kukimbilia kuwa safu ya kwanza. Bali ´ibaadah ni aina nyingi. Zigawanye ´ibaadah zako na uanze kwa jambo ambalo ni muhimu zaidi. Jambo ambalo ni muhimu zaidi ni kusoma elimu. Soma elimu na elimu ndio itakuwekea wepesi wa kufanya ´ibaadah.

Mwandishi: ´Allaamah Muhammad Amaan al-Jaamiy
Chanzo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 11-12
Toleo la: 24-05-2014
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com


  • Kitengo: Uncategorized , Da´wah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Saturday 24th, May 2014