Kuchukua Elimu Kwenye Mikanda Na Vitabu

Usiongee bila ya elimu, usiitafute elimu kinyume na milango yake, usiichukue elimu kwa watu wasiostahiki, usitosheke na kusoma vitabu na unadai kuwa umekuwa mwanachuoni? Unahifadhi tu na wala hufahamu kitu. Haitoshi kuhifadhi tu. Ni lazima ufahamu na uwe na maarifa. Hii ni njia potofu na ni njia ya watu wapotofu. Tunamuomba Allaah afya. Ni juu ya vijana wetu - Allaah Awawafikishe - kulipa umuhimu suala hili, na wakae kwa wanachuoni, na wasikilize kutoka kwao, na wachukue elimu kutoka kwa watu wake. Wasiichukue kutoka katika fahamu zao, vitabu vyao na kwa wenzao katika wale wasiojua. لَوْ هَدَانَا اللّهُ لَهَدَيْنَاكُمْ ”Lau Allaah Angelituongoa basi hapana shaka nasi tungelikuongoeni.” (Ibraahiym 14 : 21) Watasema hivi siku ya Qiyaamah. لَوْ هَدَانَا اللّهُ لَهَدَيْنَاكُمْ ”Lau Allaah Angelituongoa basi hapana shaka nasi tungelikuongoeni.” (Ibraahiym 14 : 21) Enyi ndugu zangu! Mtanabahi hili.

Usiongee bila ya elimu, usiitafute elimu kinyume na milango yake, usiichukue elimu kwa watu wasiostahiki, usitosheke na kusoma vitabu na unadai kuwa umekuwa mwanachuoni? Unahifadhi tu na wala hufahamu kitu. Haitoshi kuhifadhi tu. Ni lazima ufahamu na uwe na maarifa. Hii ni njia potofu na ni njia ya watu wapotofu. Tunamuomba Allaah afya. Ni juu ya vijana wetu – Allaah Awawafikishe – kulipa umuhimu suala hili, na wakae kwa wanachuoni, na wasikilize kutoka kwao, na wachukue elimu kutoka kwa watu wake. Wasiichukue kutoka katika fahamu zao, vitabu vyao na kwa wenzao katika wale wasiojua.

لَوْ هَدَانَا اللّهُ لَهَدَيْنَاكُمْ
”Lau Allaah Angelituongoa basi hapana shaka nasi tungelikuongoeni.” (Ibraahiym 14 : 21)

Watasema hivi siku ya Qiyaamah.

لَوْ هَدَانَا اللّهُ لَهَدَيْنَاكُمْ
”Lau Allaah Angelituongoa basi hapana shaka nasi tungelikuongoeni.” (Ibraahiym 14 : 21)

Enyi ndugu zangu! Mtanabahi hili.