Kuanza Kwa Chakula Kabla Ya Swalah

Imaam Ibn Baaz: Na yote haya ni dalili kinapotengwa chakula basi aanze nacho, ili asiende katika Swalah na moyo wake ni wenye kushughulishwa na chakula. Lakini asichukulie kama ada, hapana! Hili ni wakati fulani tu inapotokea, hivyo ataanza nacho. Ama kuchukulia kuwa ndio udhuru na anaamrisha ahli wake kutayarisha chakula wakati wanaadhini, huyu makusudio yake ni kukwepa Swalah ya Jamaa´ah. Ama ikitokea kwa bahati mbaya, hivyo ataanza nacho kama ilivyo katika Hadiyth ya ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anha). Ama kuchukulia ikawa kama ada, hili halijuzu. Kwa kuwa maana yake anakusudia kuikwepa [Jamaa´ah]. Muulizaji: Lakini Shaykh, je ale chakula cha kujaza tumbo au ale tu... Imaam Ibn Baaz: Ale kidogo tu [cha kushikiza] kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Muulizaji: Kuna ambao wanakula chakula chote, wanakunywa vinywaji vyote na kila kimechotengwa? Imaam Ibn Baaz: Kama kimeshatengwa hakuna ubaya. Tumesema tu ubora mtu afanye nini.

Imaam Ibn Baaz:
Na yote haya ni dalili kinapotengwa chakula basi aanze nacho, ili asiende katika Swalah na moyo wake ni wenye kushughulishwa na chakula. Lakini asichukulie kama ada, hapana! Hili ni wakati fulani tu inapotokea, hivyo ataanza nacho. Ama kuchukulia kuwa ndio udhuru na anaamrisha ahli wake kutayarisha chakula wakati wanaadhini, huyu makusudio yake ni kukwepa Swalah ya Jamaa´ah. Ama ikitokea kwa bahati mbaya, hivyo ataanza nacho kama ilivyo katika Hadiyth ya ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anha). Ama kuchukulia ikawa kama ada, hili halijuzu. Kwa kuwa maana yake anakusudia kuikwepa [Jamaa´ah].

Muulizaji:
Lakini Shaykh, je ale chakula cha kujaza tumbo au ale tu…

Imaam Ibn Baaz:
Ale kidogo tu [cha kushikiza] kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Muulizaji:
Kuna ambao wanakula chakula chote, wanakunywa vinywaji vyote na kila kimechotengwa?

Imaam Ibn Baaz:
Kama kimeshatengwa hakuna ubaya. Tumesema tu ubora mtu afanye nini.