Kitanda Kikubwa Kwa Mume Na Mke?

Haijuzu kwa mwanamke pindi mume wake atapomwita kukataa isipokuwa ikiwa kama atakuwa na udhuru wa Kishari´ah. Ikiwa kama hana sababu yoyote ya Kishari´ah (kama maradhi) haijuzu kukataa. al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kupitia Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: “Mwanaume akimwita mke wake kitandani na akakataa akamkasirikia usiku, Malaika humlaani mpaka kupambazuke.” Hii ni dalili inayoonesha kuwa ni jambo kubwa kabisa mwanamke kukataa kuja kitandani pindi mume wake atamwita. Hadiyth inatolea dalili vilevile kuonesha kuwa wanandoa wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), hata kwetu pia si kwa muda mrefu uliyopita, kila mmoja alikuwa na godoro lake. Hawakuwa wanalala kwenye kitanda kikubwa mara mbili (double bed). Kila mmoja alikuwa na kitanda chake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: “Godoro lako, godoro la ahli yako na godoro la Shaytwaan.” Hii ni dalili inayoonesha kuwa walikuwa wanalala mbali mbali. Leo inaonekana kama ni kutokuwa na adabu. Kinyume chake. Inepelekea katika mahaba. Mara kwa mara kuwa karibu kunasababisha kuchokana. Mtu akichukua umbali kwa mtu humpenda zaidi. Hili limetujia kutoka umagharibini na nje. Kulala pamoja kwenye chumba kimoja na kwenye kitanda kikubwa mara mbili ni jambo liko hivi na hivi.

Haijuzu kwa mwanamke pindi mume wake atapomwita kukataa isipokuwa ikiwa kama atakuwa na udhuru wa Kishari´ah. Ikiwa kama hana sababu yoyote ya Kishari´ah (kama maradhi) haijuzu kukataa. al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kupitia Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwanaume akimwita mke wake kitandani na akakataa akamkasirikia usiku, Malaika humlaani mpaka kupambazuke.”

Hii ni dalili inayoonesha kuwa ni jambo kubwa kabisa mwanamke kukataa kuja kitandani pindi mume wake atamwita.

Hadiyth inatolea dalili vilevile kuonesha kuwa wanandoa wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), hata kwetu pia si kwa muda mrefu uliyopita, kila mmoja alikuwa na godoro lake. Hawakuwa wanalala kwenye kitanda kikubwa mara mbili (double bed). Kila mmoja alikuwa na kitanda chake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Godoro lako, godoro la ahli yako na godoro la Shaytwaan.”

Hii ni dalili inayoonesha kuwa walikuwa wanalala mbali mbali. Leo inaonekana kama ni kutokuwa na adabu. Kinyume chake. Inepelekea katika mahaba. Mara kwa mara kuwa karibu kunasababisha kuchokana. Mtu akichukua umbali kwa mtu humpenda zaidi. Hili limetujia kutoka umagharibini na nje. Kulala pamoja kwenye chumba kimoja na kwenye kitanda kikubwa mara mbili ni jambo liko hivi na hivi.