Kila Mtu Ni Mwenye Haja Ya Mawaidha Kila Wakati

Watu wa imani pia ambao wamesimama na kufanya mambo ya faradhi, mambo ya wajibu, Sunnah na kujiweka mbali na mambo ya haramu ni wenye kuhitajia vilevile Da´wah ili waweze kuwa nashitu na kubadilika kutoka katika hali nzuri na kwenda katika hali nzuri zaidi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiwapa mawaidha Maswahabah. Na wao ni watu gani? Ni watu walikuwa na: 1- Elimu. 2- Matendo. 3- Kuipa nyongo dunia. 4- Wenye kujiandaa na kukutana na Allaah. Hali yao inajulikana kwa wanafunzi. Pamoja na haya yote Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anawapa mawaidha siku ya Ijumaa na nyakati mbali mbali mawaidha mbali mbali kama ilivyo katika Hadiyth ya ´Irbaadhw bin Saariyah (Radhiya Allaahu ´anhu): “Mtume wa Allaah Alitutolea mawaidha yaliyozitikisa nyoyo zetu na machozi yakatiririka.” Tukamwambia: “Kama kwamba ni mawaidha ya kuaga, tuusie ewe Mtume wa Allaah”. Akawaambia: “Nawausia kumcha Allaah, kusikiliza na kutii hata kama mtatawaliwa na mtumwa wa kihabashi. Hakika yeyote atakayeishi katika nyinyi ataona tofauti nyingi. Hivyo shikamaneni na Sunnah zangu na Sunnah za Makhaliyfah wangu waongofu. Ziumeni kwa magego yenu. Tahadharini na mambo ya kuzua! Hakika kila kitakachozushwa ni Bid´ah na kila Bid´ah ni upotevu”.” Kutokana na khatari ya Bid´ah kwa watu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akabainisha kuwa ni upotevu, bali katika upokezi mwingine: “Kila upotevu ni Motoni.” Kila kinachokwenda kinyume na Sunnah ni Bid´ah. Sisi sote ni wenye haja kubwa ya kusikiliza mawaidha na kusikiliza elimu katika kila wakati. Kwa kuwa kwa kufanya hivyo nyoyo zinakuwa hai na mtu anakuwa na nashitu na anabadilika kutoka hali moja na kwenda nyingine. Mtu kutokufanya hivyo anasibiwa na ughafilikaji. Ni lazima kuendelea kutafuta elimu, kusikiliza mawaidha, kupupia hilo, kusoma vitabu, kuweka Maktabah ya nyumbani ambapo ndani yake kutachaguliwa vitabu ambavyo anaweza kusoma mtoto, mkubwa na mgeni anayekuja kukutembelea chukua sehemu katika wakati kwa ajili ya kukumbushana elimu. Ni uzuri ulioje wa vikao vya elimu (kama hivi).

Watu wa imani pia ambao wamesimama na kufanya mambo ya faradhi, mambo ya wajibu, Sunnah na kujiweka mbali na mambo ya haramu ni wenye kuhitajia vilevile Da´wah ili waweze kuwa nashitu na kubadilika kutoka katika hali nzuri na kwenda katika hali nzuri zaidi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiwapa mawaidha Maswahabah. Na wao ni watu gani? Ni watu walikuwa na:

1- Elimu.
2- Matendo.
3- Kuipa nyongo dunia.
4- Wenye kujiandaa na kukutana na Allaah.

Hali yao inajulikana kwa wanafunzi. Pamoja na haya yote Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anawapa mawaidha siku ya Ijumaa na nyakati mbali mbali mawaidha mbali mbali kama ilivyo katika Hadiyth ya ´Irbaadhw bin Saariyah (Radhiya Allaahu ´anhu):

“Mtume wa Allaah Alitutolea mawaidha yaliyozitikisa nyoyo zetu na machozi yakatiririka.” Tukamwambia: “Kama kwamba ni mawaidha ya kuaga, tuusie ewe Mtume wa Allaah”. Akawaambia: “Nawausia kumcha Allaah, kusikiliza na kutii hata kama mtatawaliwa na mtumwa wa kihabashi. Hakika yeyote atakayeishi katika nyinyi ataona tofauti nyingi. Hivyo shikamaneni na Sunnah zangu na Sunnah za Makhaliyfah wangu waongofu. Ziumeni kwa magego yenu. Tahadharini na mambo ya kuzua! Hakika kila kitakachozushwa ni Bid´ah na kila Bid´ah ni upotevu”.”

Kutokana na khatari ya Bid´ah kwa watu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akabainisha kuwa ni upotevu, bali katika upokezi mwingine:

“Kila upotevu ni Motoni.”

Kila kinachokwenda kinyume na Sunnah ni Bid´ah.

Sisi sote ni wenye haja kubwa ya kusikiliza mawaidha na kusikiliza elimu katika kila wakati. Kwa kuwa kwa kufanya hivyo nyoyo zinakuwa hai na mtu anakuwa na nashitu na anabadilika kutoka hali moja na kwenda nyingine. Mtu kutokufanya hivyo anasibiwa na ughafilikaji. Ni lazima kuendelea kutafuta elimu, kusikiliza mawaidha, kupupia hilo, kusoma vitabu, kuweka Maktabah ya nyumbani ambapo ndani yake kutachaguliwa vitabu ambavyo anaweza kusoma mtoto, mkubwa na mgeni anayekuja kukutembelea chukua sehemu katika wakati kwa ajili ya kukumbushana elimu. Ni uzuri ulioje wa vikao vya elimu (kama hivi).