Kijakazi Alijua Mola Wake Alipo Tofauti Na Watu Wengi Wa Zama Hizi

Imaam al-Albaaniy: Huu ndio upotofu wa wazi, kutokana na dalili zilizo wazi katika Qur-aan zioneshazo ya kwamba Ar-Rahmaan Yuko juu ya ´Arshi Kastawaa. Na Kauli ya Allaah: سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الْأَعْلَى "Sabbih (tukuza) Jina la Mola wako Aliye juu kabisa." (87:01) Na pindi Alipowasifu waja Wake waumini: يَخَافُونَ رَبَّهُم مِّن فَوْقِهِمْ "Wanamkhofu Mola wao Aliye juu yao, na wanafanya yale wanayoamrishwa." (16:50) تَعْرُجُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ إِلَيْهِ “Malaika na Roho (Jibrily) wanapanda Kwake.” (70 : 04) Katakasika Allaah kwa wayasemayo madhalimu kutakasika ambako ni kukubwa. Katika Hadiyth Swahiyh: "Alikuwepo Allaah na hapakuwa kitu pamoja Naye." Ni mahali gani [Alikuwepo Allaah] mahali ambapo wamekusanyika watu hawa walio kila mahali? Na khaswa mahali kama hizi kuna ambazo ni safi, na kuna ambazo ni za najisi na chafu, vyoo, baa, sehemu za taka, sehemu za wafanya uasherati na kadhalika. Vipi basi wasimtakasi Allaah (´Azza wa Jalla) kwa kuwa kila mahali? Pamoja na kuwa Amesema katika Aayah nyingi kama tulivyosema ya kwamba Yeye Yuko juu ya ´Arshi Yake Kastawaa. Na katika Hadiyth Swahiyh ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuuliza kijakazi ambaye bwana wake alikuwa anataka kumwacha huru: Akamuuliza: "Yuko wapi Allaah?". [Kijakazi yule akajibu]: "Mbinguni". Akamuuliza tena: "Ni nani mimi?". Akajibu: "Wewe ni Mtume wa Allaah". Akamgeukia bwana wake na kumwambia: "Muache! Kwani kwa hakika ni muuminah". Kijakazi katika zama za Mtume alikuwa na Fiqh [katika Dini] zaidi kuliko Fuqahaa wengi wa leo. Kwa kuwa ukiwauliza wengi katika watu hawa [Ahl-ul-Bid´ah]: "Yuko wapi Allaah?" Watakujibu: "Yuko kila mahali". Mmoja katika majirani zangu anasema: "Allaah Yuko katika kila kilichopo". Masikini watu hawa. Vilivyopo vimeumbwa, na Alikuwepo Allaah na hapakuwa kiumbe chochote. Hivyo, baada ya Mola Wetu kuumba viumbe, Akageuka kuwa sehemu ya viumbe hawa - pamoja na takataka/uchafuunaopatikana humo! [Kamwe!]. Ametakasika Allaah kwa wasemayo madhalimu kutakasika kukubwa.

Imaam al-Albaaniy:

Huu ndio upotofu wa wazi, kutokana na dalili zilizo wazi katika Qur-aan zioneshazo ya kwamba Ar-Rahmaan Yuko juu ya ´Arshi Kastawaa. Na Kauli ya Allaah:

سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الْأَعْلَى
“Sabbih (tukuza) Jina la Mola wako Aliye juu kabisa.” (87:01)

Na pindi Alipowasifu waja Wake waumini:

يَخَافُونَ رَبَّهُم مِّن فَوْقِهِمْ
“Wanamkhofu Mola wao Aliye juu yao, na wanafanya yale wanayoamrishwa.” (16:50)

تَعْرُجُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ إِلَيْهِ
“Malaika na Roho (Jibrily) wanapanda Kwake.” (70 : 04)

Katakasika Allaah kwa wayasemayo madhalimu kutakasika ambako ni kukubwa.
Katika Hadiyth Swahiyh:

“Alikuwepo Allaah na hapakuwa kitu pamoja Naye.”

Ni mahali gani [Alikuwepo Allaah] mahali ambapo wamekusanyika watu hawa walio kila mahali? Na khaswa mahali kama hizi kuna ambazo ni safi, na kuna ambazo ni za najisi na chafu, vyoo, baa, sehemu za taka, sehemu za wafanya uasherati na kadhalika. Vipi basi wasimtakasi Allaah (´Azza wa Jalla) kwa kuwa kila mahali? Pamoja na kuwa Amesema katika Aayah nyingi kama tulivyosema ya kwamba Yeye Yuko juu ya ´Arshi Yake Kastawaa.

Na katika Hadiyth Swahiyh ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuuliza kijakazi ambaye bwana wake alikuwa anataka kumwacha huru: Akamuuliza: “Yuko wapi Allaah?”. [Kijakazi yule akajibu]: “Mbinguni”. Akamuuliza tena: “Ni nani mimi?”. Akajibu: “Wewe ni Mtume wa Allaah”. Akamgeukia bwana wake na kumwambia: “Muache! Kwani kwa hakika ni muuminah”.

Kijakazi katika zama za Mtume alikuwa na Fiqh [katika Dini] zaidi kuliko Fuqahaa wengi wa leo. Kwa kuwa ukiwauliza wengi katika watu hawa [Ahl-ul-Bid´ah]: “Yuko wapi Allaah?” Watakujibu: “Yuko kila mahali”.

Mmoja katika majirani zangu anasema:

“Allaah Yuko katika kila kilichopo”.

Masikini watu hawa. Vilivyopo vimeumbwa, na Alikuwepo Allaah na hapakuwa kiumbe chochote. Hivyo, baada ya Mola Wetu kuumba viumbe, Akageuka kuwa sehemu ya viumbe hawa – pamoja na takataka/uchafuunaopatikana humo! [Kamwe!]. Ametakasika Allaah kwa wasemayo madhalimu kutakasika kukubwa.


  • Author: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy. Silsilat al-Hudaa wan-Nuur 178
  • Kitengo: Uncategorized , Tawhiyd na ´Aqiydah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Saturday 19th, October 2013