Kidole Kidogo Cha Allaah

Allaah (Subhanaahu wa Ta´ala) Kasema: فَلَمَّا تَجَلَّىٰ رَبُّهُ لِلْجَبَلِ جَعَلَهُ دَكًّا “Basi Mola wako Aliopojidhihirisha katika jabali, Alilijaalia kuwa lenye kuvurugika vurugika... ” Abu Ja'far at-Twabariy kasema kuhusu Aayah hii: "Ahmad bin Suhayl al-Waasitiy katueleza: Qurrah bin 'Iysa katueleza: al-A'mash katueleza kutoka kwa mtu, kutoka kwa Anas ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kasema: "Hivyo Allaah Akajidhihirisha katika jibali, Akaashiria kwa Kidole Chake na ikavurugika vurugika kuwa kifusi cha ardhi.” Abu Ismaa´iyl alionesha hilo kwa kidole chake kidogo." Katika isnadi hii kuna mpokezi asiejulikana. Kisha akasema at-Twabariy: "al-Muthannah katueleza: Hajjaaj bin Minhaal katueleza: Hammaad katueleza kutoka kwa al-Layth, kutoka kwa Anas." Njia maarufu ni ya Hammaad bin Salamah kutoka kwa Thaabit, kutoka kwa Anas, ambayo Ibn Jariyr amesema: "al-Muthannah kanieleza: Hudbah bin Khaalid katueleza: Hammaad bin Salamah katueleza kutoka kwa Thaabit, kutoka kwa Anas ambaye kasema: "Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) alisoma “Basi Mola Wako Aliopojidhihirisha katika jabali, Alilijaalia kuwa lenye kuvurugika vurugika", akaweka kidole gumba karibu na kidole kidogo na kusema: "Jabali lilididimia (liliangamia)." Humayd alimwambia Thaabit: "Je, kasema namna hii?" Hivyo akanyanyua Thaabit mkono wake, akampiga Humayd kwenye kifua na kusema, "Je, nifiche hilo baada ya kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) na Anas wametusimulia?" Kwa njia hii imepokelewa pia Imaam Ahmad katika "al-Musnad" yake: "Abul-Muthannah Mu'aadh bin Mu'aadh al-'Anbariy katueleza: Hammaad bin Salamah katueleza: Thaabit al-Bunaaniy katueleza kutoka kwa Anas bin Maalik, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) ambaye amesema kuhusiana na Aayah “Basi Mola wako Aliopojidhihirisha katika jabali, Alilijaalia kuwa lenye kuvurugika vurugika", "Namna hii" yaani ni kwamba Alionesha sehemu ya kidole kidogo." Ahmad kasema: "Mu'aadh alituonesha hilo sisi. Hivyo akasema Humayd at-Tawiyl kumwambia: Una maanisha nini kwa hilo?" Akampiga pigo la nguvu kwenye kifua na kusema: "Wewe ni nani, Humayd? Wewe ni nini, Humayd? Anas bin Maalik kanieleza hili kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) na wewe unanambia nini ninachomaanisha kwa hili?" Namna hii pia imepokelewa na at-Tirmidhiy kutoka kwa 'Abdul-Wahhab bin al-Hakam al-Warraaq, kutoka kwa Mu'aadh kwa isnadi iliyobaki. Vilevile alipokea kutoka kwa 'Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan ad-Daarimiy, kutoka kwa Sulaymaan bin Harb, kutoka kwa Hammaad bin Salamah kwa isnadi iliyobaki. Kisha akasema at-Tirmidhiy: "Hii ni Hadiyth Hasan na Swahiyh ambayo tunaijua pekee kaipokea kupitia kwa Hammaad." Vile vile, kapokea al-Haakim katika 'al-Mustadrak' yake kupitia kwa Hammaad bin Salamah kwa isnadi iliyobaki na kusema: "Hii ni Hadiyth Swahiyh inayoeneza masharti, si al-Bukhaariy wala Muslim hawakuipokea." Imepokelewa pia na Abu Muhammad al-Hasan bin Muhammad bin 'Aliy al-Khallaal, kutoka kwa Muhammad bin 'Aliy bin Suwayd, kutoka kwa Abul-Qaasim al-Baghawiy, kutoka kwa Hudbah bin Khaalid, kutoka kwa Hammaad bin Salamah. Kasema: "Ni isnadi Swahiyh isiyokuwa na kasoro yoyote.” Chanzo: Imaam Ismaa´iyl bin Kathiyr ad-Dimashqiy Chanzo: Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhiym (2/326-327) Mu’assasah ar-Risaalah, 1422/2001

Allaah (Subhanaahu wa Ta´ala) Kasema:

فَلَمَّا تَجَلَّىٰ رَبُّهُ لِلْجَبَلِ جَعَلَهُ دَكًّا
“Basi Mola wako Aliopojidhihirisha katika jabali, Alilijaalia kuwa lenye kuvurugika vurugika… ”

Abu Ja’far at-Twabariy kasema kuhusu Aayah hii:
“Ahmad bin Suhayl al-Waasitiy katueleza: Qurrah bin ‘Iysa katueleza: al-A’mash katueleza kutoka kwa mtu, kutoka kwa Anas ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kasema:
“Hivyo Allaah Akajidhihirisha katika jibali, Akaashiria kwa Kidole Chake na ikavurugika vurugika kuwa kifusi cha ardhi.”
Abu Ismaa´iyl alionesha hilo kwa kidole chake kidogo.”

Katika isnadi hii kuna mpokezi asiejulikana. Kisha akasema at-Twabariy:
“al-Muthannah katueleza: Hajjaaj bin Minhaal katueleza: Hammaad katueleza kutoka kwa al-Layth, kutoka kwa Anas.” Njia maarufu ni ya Hammaad bin Salamah kutoka kwa Thaabit, kutoka kwa Anas, ambayo Ibn Jariyr amesema:
“al-Muthannah kanieleza: Hudbah bin Khaalid katueleza: Hammaad bin Salamah katueleza kutoka kwa Thaabit, kutoka kwa Anas ambaye kasema:
“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alisoma “Basi Mola Wako Aliopojidhihirisha katika jabali, Alilijaalia kuwa lenye kuvurugika vurugika”, akaweka kidole gumba karibu na kidole kidogo na kusema:
“Jabali lilididimia (liliangamia).”

Humayd alimwambia Thaabit: “Je, kasema namna hii?” Hivyo akanyanyua Thaabit mkono wake, akampiga Humayd kwenye kifua na kusema, “Je, nifiche hilo baada ya kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na Anas wametusimulia?”

Kwa njia hii imepokelewa pia Imaam Ahmad katika “al-Musnad” yake:
“Abul-Muthannah Mu’aadh bin Mu’aadh al-‘Anbariy katueleza: Hammaad bin Salamah katueleza: Thaabit al-Bunaaniy katueleza kutoka kwa Anas bin Maalik, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) ambaye amesema kuhusiana na Aayah “Basi Mola wako Aliopojidhihirisha katika jabali, Alilijaalia kuwa lenye kuvurugika vurugika”,
“Namna hii” yaani ni kwamba Alionesha sehemu ya kidole kidogo.”
Ahmad kasema:
“Mu’aadh alituonesha hilo sisi. Hivyo akasema Humayd at-Tawiyl kumwambia: Una maanisha nini kwa hilo?” Akampiga pigo la nguvu kwenye kifua na kusema: “Wewe ni nani, Humayd? Wewe ni nini, Humayd? Anas bin Maalik kanieleza hili kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na wewe unanambia nini ninachomaanisha kwa hili?”

Namna hii pia imepokelewa na at-Tirmidhiy kutoka kwa ‘Abdul-Wahhab bin al-Hakam al-Warraaq, kutoka kwa Mu’aadh kwa isnadi iliyobaki. Vilevile alipokea kutoka kwa ‘Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan ad-Daarimiy, kutoka kwa Sulaymaan bin Harb, kutoka kwa Hammaad bin Salamah kwa isnadi iliyobaki. Kisha akasema at-Tirmidhiy:
“Hii ni Hadiyth Hasan na Swahiyh ambayo tunaijua pekee kaipokea kupitia kwa Hammaad.”

Vile vile, kapokea al-Haakim katika ‘al-Mustadrak’ yake kupitia kwa Hammaad bin Salamah kwa isnadi iliyobaki na kusema:
“Hii ni Hadiyth Swahiyh inayoeneza masharti, si al-Bukhaariy wala Muslim hawakuipokea.”

Imepokelewa pia na Abu Muhammad al-Hasan bin Muhammad bin ‘Aliy al-Khallaal, kutoka kwa Muhammad bin ‘Aliy bin Suwayd, kutoka kwa Abul-Qaasim al-Baghawiy, kutoka kwa Hudbah bin Khaalid, kutoka kwa Hammaad bin Salamah. Kasema:
“Ni isnadi Swahiyh isiyokuwa na kasoro yoyote.”

Chanzo: Imaam Ismaa´iyl bin Kathiyr ad-Dimashqiy
Chanzo: Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhiym (2/326-327)
Mu’assasah ar-Risaalah, 1422/2001


  • Kitengo: Uncategorized , Vidole vya Allaah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 27th, October 2013