Khatari Ya Madhehebu Ya Qadariyyah Na Jabriyyah

Jambo la sita: Mambo ambayo yanapelekea katika madhehebu ya Jabriyyah na Qadariyyah Madhehebu yao yanapelekea katika mambo ya khatari: 1- Madhehebu ya Qadariyyah yanalazimisha: Kuthibitisha miungu ikiwa ni pamoja na Allaah. Hii ni Shirki katika Rubuubiyyah. Kwa ajili hii ndio maana wakaitwa “Majusi wa Ummah huu.” 2- Madhehebu ya Jabriyyah yanalazimisha: Kumsifu Allaah na dhuluma na kwamba anawaadhibu waja Wake kwa kitu ambacho hawakukifanya wao bali kimefanya Yeye (Allaah). Allaah Anawaadhibu kwa kitu ambacho hawakufanya wao. Wao wanapelekwa tu kama upepo bila ya khiyari na bila ya kutaka kwao. Katika hili kuna kumsifu Allaah (Jalla wa ´Alaa) na dhuluma, kwa kuwa Amewaadhibu waja Wake kwa kitu ambacho hawakufanya wao bali Amewaadhibu kwa kitu Chake Yeye Mwenyewe. Hakufichikani (kwa yeyote) uovu wa madhehebu haya batili. Allaah (Jalla wa ´Alaa) Anasema: وَلَا تُجْزَوْنَ إِلَّا مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ “Na wala hamtalipwa isipokuwa yale mliyokuwa mkiyatenda.” (Yaasiyn:54) Akaambatanisha adhabu na kufuru, maasi na ShirkI. Akaambatanisha vilevile thawabu kwa utiifu na mambo ya kheri. Allaah Hamdhulumu yeyote: إِنَّ اللَّـهَ لَا يَظْلِمُ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ ۖ وَإِن تَكُ حَسَنَةً يُضَاعِفْهَا وَيُؤْتِ مِن لَّدُنْهُ أَجْرًا عَظِيمًا “Hakika Allaah Hadhulumu (viumbe Vyake hata) uzito wa atomu (au sisimizi). Na ikiwa ni ‘amali njema Huizidisha na Hutoa kutoka Kwake ujira mkuu.” (an-Nisaa:40) Huu ndio uadilifu kutoka Kwake (Subhaanahu wa Ta´ala). Kutokana na uadilifu Wake vilevile hazidishi juu ya dhambi moja, bali anamlipa mtu kwa mfano wake tu. Vilevile kutokana na uadilifu wake ni kwamba anamlipa mtu kwa kuzidisha kwa jema lake moja (Subhaanahu wa Ta´ala): إِنَّ اللَّـهَ لَا يَظْلِمُ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ ۖ وَإِن تَكُ حَسَنَةً يُضَاعِفْهَا “Hakika Allaah Hadhulumu (viumbe Vyake hata) uzito wa atomu (au sisimizi). Na ikiwa ni ‘amali njema Huizidisha.” (an-Nisaa:40) Kuzidisha ni fadhila kutoka kwa Allaah mpaka kufikia mara kumi mfano wake, mpaka kufikia mara mia saba na zaidi ya hapo. Ama dhambi Allaah Anamlipa mtu kwa hiyo hiyo dhambi tu na wala haizidishi. Hili ni kutokana na uadilifu Wake (Subhaanahu wa Ta´ala). Pamoja na hivyo, Jabriyyah wanamsifu Allaah na dhuluma na kwamba anawaadhibu waja kwa Matendo Anayofanya Mwenyewe na wao hawakufanya kitu, bali anapelekwa kama mashine. Haya ni madhehebu batili. 3- Yanalazimisha vilevile kukanusha (au kuacha) kufanya sababu na wanasema ya kwamba maadamu Ameshaamua na Kukadiria, basi mimi nakaa na yaliyokadiriwa yatakuwa. Haya ni katika matusi ya madhehebu ya Jabriyayh. 4- Yanalazimisha madhehebu ya Mu´tazilah – kama tulivotangulia kusema – Shirki katika Rubuubiyyah. 5- Yanalazimisha katika madhehebu yao jambo la khatari sana, bali ni kutomuwezesha Allaah (Jalla wa ´Alaa) na kwamba katika Ufalme Wake kunakuwa yale Asiyoyataka. Sifa hii ni kutomuwezesha Allaah (Jalla wa ´Alaa). Madhehebu yote mawili ni madhehebu batili na yanalazimisha makatazo na madhara mengi. Ama madhehebu ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanakuwa kati na kati na (ni madhehebu) ya uadilifu katika kila kitu. Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah daima wanakuwa kati na kati baina ya mapote potevu katika hili na mengineyo. Wao wanamthibitishia Allaah Matendo Yake, Utashi Wake na Matakwa Yake, Qadhwaa na Qadari Yake kama jinsi wanavyowathibitishia waja pia kuwa na matakwa yao na utashi wao. Wanatembea pamoja na Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hawakanushi Qadhwaa na Qadar kama wanavosema Mu´tazilah kama jinsi hawapetuki mipaka katika kuthibitisha Qadhwaa na Qadar na kuwavua waja matakwa na utashi wao kama wanavofanya Jabriyyah. Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy Chanzo: al-Haaiyyah Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan Chanzo: "Sharh al-Haaiyyah", uk. 152-154

Jambo la sita: Mambo ambayo yanapelekea katika madhehebu ya Jabriyyah na Qadariyyah

Madhehebu yao yanapelekea katika mambo ya khatari:

1- Madhehebu ya Qadariyyah yanalazimisha: Kuthibitisha miungu ikiwa ni pamoja na Allaah. Hii ni Shirki katika Rubuubiyyah. Kwa ajili hii ndio maana wakaitwa “Majusi wa Ummah huu.”

2- Madhehebu ya Jabriyyah yanalazimisha: Kumsifu Allaah na dhuluma na kwamba anawaadhibu waja Wake kwa kitu ambacho hawakukifanya wao bali kimefanya Yeye (Allaah). Allaah Anawaadhibu kwa kitu ambacho hawakufanya wao. Wao wanapelekwa tu kama upepo bila ya khiyari na bila ya kutaka kwao. Katika hili kuna kumsifu Allaah (Jalla wa ´Alaa) na dhuluma, kwa kuwa Amewaadhibu waja Wake kwa kitu ambacho hawakufanya wao bali Amewaadhibu kwa kitu Chake Yeye Mwenyewe. Hakufichikani (kwa yeyote) uovu wa madhehebu haya batili. Allaah (Jalla wa ´Alaa) Anasema:

وَلَا تُجْزَوْنَ إِلَّا مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ
“Na wala hamtalipwa isipokuwa yale mliyokuwa mkiyatenda.” (Yaasiyn:54)

Akaambatanisha adhabu na kufuru, maasi na ShirkI. Akaambatanisha vilevile thawabu kwa utiifu na mambo ya kheri. Allaah Hamdhulumu yeyote:

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَظْلِمُ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ ۖ وَإِن تَكُ حَسَنَةً يُضَاعِفْهَا وَيُؤْتِ مِن لَّدُنْهُ أَجْرًا عَظِيمًا
“Hakika Allaah Hadhulumu (viumbe Vyake hata) uzito wa atomu (au sisimizi). Na ikiwa ni ‘amali njema Huizidisha na Hutoa kutoka Kwake ujira mkuu.” (an-Nisaa:40)

Huu ndio uadilifu kutoka Kwake (Subhaanahu wa Ta´ala). Kutokana na uadilifu Wake vilevile hazidishi juu ya dhambi moja, bali anamlipa mtu kwa mfano wake tu. Vilevile kutokana na uadilifu wake ni kwamba anamlipa mtu kwa kuzidisha kwa jema lake moja (Subhaanahu wa Ta´ala):

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَظْلِمُ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ ۖ وَإِن تَكُ حَسَنَةً يُضَاعِفْهَا
“Hakika Allaah Hadhulumu (viumbe Vyake hata) uzito wa atomu (au sisimizi). Na ikiwa ni ‘amali njema Huizidisha.” (an-Nisaa:40)

Kuzidisha ni fadhila kutoka kwa Allaah mpaka kufikia mara kumi mfano wake, mpaka kufikia mara mia saba na zaidi ya hapo. Ama dhambi Allaah Anamlipa mtu kwa hiyo hiyo dhambi tu na wala haizidishi. Hili ni kutokana na uadilifu Wake (Subhaanahu wa Ta´ala).

Pamoja na hivyo, Jabriyyah wanamsifu Allaah na dhuluma na kwamba anawaadhibu waja kwa Matendo Anayofanya Mwenyewe na wao hawakufanya kitu, bali anapelekwa kama mashine. Haya ni madhehebu batili.

3- Yanalazimisha vilevile kukanusha (au kuacha) kufanya sababu na wanasema ya kwamba maadamu Ameshaamua na Kukadiria, basi mimi nakaa na yaliyokadiriwa yatakuwa. Haya ni katika matusi ya madhehebu ya Jabriyayh.

4- Yanalazimisha madhehebu ya Mu´tazilah – kama tulivotangulia kusema – Shirki katika Rubuubiyyah.

5- Yanalazimisha katika madhehebu yao jambo la khatari sana, bali ni kutomuwezesha Allaah (Jalla wa ´Alaa) na kwamba katika Ufalme Wake kunakuwa yale Asiyoyataka. Sifa hii ni kutomuwezesha Allaah (Jalla wa ´Alaa). Madhehebu yote mawili ni madhehebu batili na yanalazimisha makatazo na madhara mengi.

Ama madhehebu ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanakuwa kati na kati na (ni madhehebu) ya uadilifu katika kila kitu. Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah daima wanakuwa kati na kati baina ya mapote potevu katika hili na mengineyo. Wao wanamthibitishia Allaah Matendo Yake, Utashi Wake na Matakwa Yake, Qadhwaa na Qadari Yake kama jinsi wanavyowathibitishia waja pia kuwa na matakwa yao na utashi wao. Wanatembea pamoja na Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hawakanushi Qadhwaa na Qadar kama wanavosema Mu´tazilah kama jinsi hawapetuki mipaka katika kuthibitisha Qadhwaa na Qadar na kuwavua waja matakwa na utashi wao kama wanavofanya Jabriyyah.

Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy
Chanzo: al-Haaiyyah
Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: “Sharh al-Haaiyyah”, uk. 152-154


  • Kitengo: Uncategorized , Jabriyyah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Thursday 20th, February 2014