Khatari Ya Kuwa Kiigizo Katika Maovu

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema: “Atakayelingania katika upotevu, basi ana madhambi mfano wa madhambi wa ambaye atakayemfuata, hatopungukiwa na hilo katika madhambi yao na chochote. Na atakayelingania katika uongofu, ana ujira mfano wa ujira wa atakayemfuata, hatopungukiwa na hilo katika ujira wa atakayemfuata na chochote.” Muislamu atahadhari asiwe miongoni mwa Madu´aat wapotevu. Kwa kuwa si kwamba atapata madhambi juu ya na nafsi yake mwenyewe, bali atabeba madhambi ya watakaomfuata. Kwa kuwa yeye ndiye amewadanganya, akawashika mkono na kuwafungulia mlango wa shari. Hivyo akawa ni kiigizo katika shari. Anasema (Ta´ala): لِيَحْمِلُوا أَوْزَارَهُمْ كَامِلَةً يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۙ وَمِنْ أَوْزَارِ الَّذِينَ يُضِلُّونَهُم بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗ أَلَا سَاءَ مَا يَزِرُونَ “Ili wabebe mizigo (ya madhambi) yao kamili Siku ya Qiyaamah, na mizigo (ya madhambi) ya wale waliowapoteza bila ya elimu. Tanabahi! Ubaya ulioje (mizigo ya dhambi) wanayoyabeba.” (an-Nahl:25) Khatari ni kubwa katika hili. Hili ni katika mambo ambayo yanazidi kusisitiza kwa Muislamu awe kiigizo katika mambo ya kheri na alinganie katika kheri. Ajiepushe mbali asiwe mlinganiaji katika shari, kufuata hawaa (matamanio) au uendaji kinyume bila kujali yule atakayekuwa juu ya hilo. Haki ndio yenye haki ya kufuatwa. Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy Chanzo: al-Haaiyyah Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan Chanzo: "Sharh al-Haaiyyah", uk. 107-108

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema:

“Atakayelingania katika upotevu, basi ana madhambi mfano wa madhambi wa ambaye atakayemfuata, hatopungukiwa na hilo katika madhambi yao na chochote. Na atakayelingania katika uongofu, ana ujira mfano wa ujira wa atakayemfuata, hatopungukiwa na hilo katika ujira wa atakayemfuata na chochote.”

Muislamu atahadhari asiwe miongoni mwa Madu´aat wapotevu. Kwa kuwa si kwamba atapata madhambi juu ya na nafsi yake mwenyewe, bali atabeba madhambi ya watakaomfuata. Kwa kuwa yeye ndiye amewadanganya, akawashika mkono na kuwafungulia mlango wa shari. Hivyo akawa ni kiigizo katika shari. Anasema (Ta´ala):

لِيَحْمِلُوا أَوْزَارَهُمْ كَامِلَةً يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۙ وَمِنْ أَوْزَارِ الَّذِينَ يُضِلُّونَهُم بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗ أَلَا سَاءَ مَا يَزِرُونَ
“Ili wabebe mizigo (ya madhambi) yao kamili Siku ya Qiyaamah, na mizigo (ya madhambi) ya wale waliowapoteza bila ya elimu. Tanabahi! Ubaya ulioje (mizigo ya dhambi) wanayoyabeba.” (an-Nahl:25)

Khatari ni kubwa katika hili. Hili ni katika mambo ambayo yanazidi kusisitiza kwa Muislamu awe kiigizo katika mambo ya kheri na alinganie katika kheri. Ajiepushe mbali asiwe mlinganiaji katika shari, kufuata hawaa (matamanio) au uendaji kinyume bila kujali yule atakayekuwa juu ya hilo. Haki ndio yenye haki ya kufuatwa.

Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy
Chanzo: al-Haaiyyah
Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: “Sharh al-Haaiyyah”, uk. 107-108


  • Kitengo: Uncategorized , Da´wah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Monday 17th, February 2014