Kauli Za Maimamu Kuhusu Kauli Zao Zinapokwenda Kinyume

Maimamu wanatahadharisha kuchukua kauli zao bila ya kujua dalili: Imaam Maalik (Rahimahu Allaah) anasema: “Sote kauli zetu ni zenye ni zinachukuliwa na kurudishwa isipokuwa mwenye kaburi hili.” yaani Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Imaam ash-Shaafi´iy (Rahimahu Allaah): “Hadiyth itaposihi, basi hayo ndio madhehebu yangu.” Anasema tena: “Kauli yangu ikitofautiana na kauli ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), chukua kauli ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na itupilie mbali kauli yangu.” Anasema tena: “Waislamu wamekubaliana juu ya yule atakayebainikiwa na Sunnah ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) haimpasi kwake kuiacha kwa kuiendea kauli ya yeyote.” Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) anasema: “Ninashangazwa na watu wanaojua Isnaad na usahihi wake wanaenda katika rai ya Sufyaan!.” Sufyaan ath-Thawriy Faqiyh ambaye alikuwa ni Imaam mtukufu. Allaah (Ta´ala) Anasema: فَلْيَحْذَرِ الَّذِينَ يُخَالِفُونَ عَنْ أَمْرِهِ أَن تُصِيبَهُمْ فِتْنَةٌ أَوْ يُصِيبَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ “Basi watahadhari wale wanaokhalifu amri yake, isije kuwasibu fitnah au ikawasibu adhabu iumizayo.” (an-Nuur:63) Mnajua ni ipi fitina? Fitina hapa ni Shirki. Pengine atapoacha baadhi ya kauli yake (Mtume) akaingiwa moyoni mwake na kitu katika upotevu akaangamia”.” Hakuna kauli yoyote pamoja na kauli ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni wajibu kwetu wakati wa tofauti kurejea katika mizani. Hii ni Rahmah ya Allaah kwetu sisi kwa kuwa Hakutuacha juu ya tofauti na kauli za watu, bali Ametuamrisha kuzipima hizo kauli na Kitabu na Sunnah. Hili linakuwa kwa wanachuoni. Ama ´Awwaam ni lazima kwao kuwauliza wanachuoni: فَاسْأَلُوا أَهْلَ الذِّكْرِ إِن كُنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ “Basi ulizeni watu wa Adh-Dhikr (wanazuoni) ikiwa hamjui.” (an-Nahl:43) Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy Chanzo: al-Haaiyyah Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan Chanzo: "Sharh al-Haaiyyah", uk. 195-196

Maimamu wanatahadharisha kuchukua kauli zao bila ya kujua dalili:

Imaam Maalik (Rahimahu Allaah) anasema:

“Sote kauli zetu ni zenye ni zinachukuliwa na kurudishwa isipokuwa mwenye kaburi hili.” yaani Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Imaam ash-Shaafi´iy (Rahimahu Allaah):

“Hadiyth itaposihi, basi hayo ndio madhehebu yangu.”

Anasema tena:

“Kauli yangu ikitofautiana na kauli ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), chukua kauli ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na itupilie mbali kauli yangu.”

Anasema tena:

“Waislamu wamekubaliana juu ya yule atakayebainikiwa na Sunnah ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) haimpasi kwake kuiacha kwa kuiendea kauli ya yeyote.”

Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) anasema: “Ninashangazwa na watu wanaojua Isnaad na usahihi wake wanaenda katika rai ya Sufyaan!.” Sufyaan ath-Thawriy Faqiyh ambaye alikuwa ni Imaam mtukufu. Allaah (Ta´ala) Anasema:

فَلْيَحْذَرِ الَّذِينَ يُخَالِفُونَ عَنْ أَمْرِهِ أَن تُصِيبَهُمْ فِتْنَةٌ أَوْ يُصِيبَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ
“Basi watahadhari wale wanaokhalifu amri yake, isije kuwasibu fitnah au ikawasibu adhabu iumizayo.” (an-Nuur:63)

Mnajua ni ipi fitina? Fitina hapa ni Shirki. Pengine atapoacha baadhi ya kauli yake (Mtume) akaingiwa moyoni mwake na kitu katika upotevu akaangamia”.”

Hakuna kauli yoyote pamoja na kauli ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni wajibu kwetu wakati wa tofauti kurejea katika mizani. Hii ni Rahmah ya Allaah kwetu sisi kwa kuwa Hakutuacha juu ya tofauti na kauli za watu, bali Ametuamrisha kuzipima hizo kauli na Kitabu na Sunnah. Hili linakuwa kwa wanachuoni. Ama ´Awwaam ni lazima kwao kuwauliza wanachuoni:

فَاسْأَلُوا أَهْلَ الذِّكْرِ إِن كُنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ
“Basi ulizeni watu wa Adh-Dhikr (wanazuoni) ikiwa hamjui.” (an-Nahl:43)

Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy
Chanzo: al-Haaiyyah
Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: “Sharh al-Haaiyyah”, uk. 195-196


  • Kitengo: Uncategorized , Manhaj
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Saturday 1st, March 2014