Kati Yetu Sisi Na Mumayyi´ah Ni Vitabu Vya Salaf

Miongoni mwa utata tunasikia leo kwamba ´wameanza kuwahujumu ndugu zao` na ´hakuna hata mmoja mwenye kusalimika nao´. Hii ni dalili kabisa ya kuonesha kuwa mtu huyu ni mwaminifu. Ahmad (Rahimahu Allaah) alimsusa ´Aliy [al-Madiyniy] na alimsusa Yahyaa bin Ma´iyn pindi walipoingia katika fitina. Yahyaa bin Ma´iyn anaingia kwa Ahmad bin Hanbal, Ahmad akageuza uso kutoka kwake na kuangalia kwenye ukuta. Yahyaa akazungumza na Ahmad amenyamaza kimya. Yahyaa anatoka na kusema: “Hivi kweli ninasuswa baada ya urafiki wote huu wa muda mrefu?” Wako wapi mfano wa Ahmad leo hii? Leo wanasema ´mnawakimbiza watu` na ´msizungumzie mambo haya`. Ninawauliza kwa Jina la Allaah; hivi kweli watu hawa wanamfuata Ahmad na maimamu wa Ahl-us-Sunnah? Ninaapa kwa Allaah hawawafuati hata kama watachukulia hilo kwa ubaya. Wacha tuweke baina yetu sisi na hawa wanaosema namna hii vitabu vya Sunnah na vya Salaf. Yule mwenye kuvikubali tunamkubali kwa furaha na mwenye kuvikataa na sisi tunamkataa. Leo ni wakati wa fitina na zinasababisha vurugu na ghasia. Mnaona wenyewe yanayoendelea. Wanachuoni wanazijua zinapokuwa njiani ziwaja na zinapopita ´Awwaam wanazijua. Mapote haya na propaganda hizi ziko wazi na zinajua kila mtu. Balaa ni kwa yule anayejinasibisha na Salafiyyah na anadai kuwa ni Salafiy na mwenendo wake ni kama huu. Huyu ni mbaya zaidi kwetu kuliko Ahl-us-Sunnah.

Miongoni mwa utata tunasikia leo kwamba ´wameanza kuwahujumu ndugu zao` na ´hakuna hata mmoja mwenye kusalimika nao´. Hii ni dalili kabisa ya kuonesha kuwa mtu huyu ni mwaminifu. Ahmad (Rahimahu Allaah) alimsusa ´Aliy [al-Madiyniy] na alimsusa Yahyaa bin Ma´iyn pindi walipoingia katika fitina. Yahyaa bin Ma´iyn anaingia kwa Ahmad bin Hanbal, Ahmad akageuza uso kutoka kwake na kuangalia kwenye ukuta. Yahyaa akazungumza na Ahmad amenyamaza kimya. Yahyaa anatoka na kusema:

“Hivi kweli ninasuswa baada ya urafiki wote huu wa muda mrefu?”

Wako wapi mfano wa Ahmad leo hii? Leo wanasema ´mnawakimbiza watu` na ´msizungumzie mambo haya`. Ninawauliza kwa Jina la Allaah; hivi kweli watu hawa wanamfuata Ahmad na maimamu wa Ahl-us-Sunnah? Ninaapa kwa Allaah hawawafuati hata kama watachukulia hilo kwa ubaya.

Wacha tuweke baina yetu sisi na hawa wanaosema namna hii vitabu vya Sunnah na vya Salaf. Yule mwenye kuvikubali tunamkubali kwa furaha na mwenye kuvikataa na sisi tunamkataa. Leo ni wakati wa fitina na zinasababisha vurugu na ghasia. Mnaona wenyewe yanayoendelea. Wanachuoni wanazijua zinapokuwa njiani ziwaja na zinapopita ´Awwaam wanazijua. Mapote haya na propaganda hizi ziko wazi na zinajua kila mtu. Balaa ni kwa yule anayejinasibisha na Salafiyyah na anadai kuwa ni Salafiy na mwenendo wake ni kama huu. Huyu ni mbaya zaidi kwetu kuliko Ahl-us-Sunnah.