Kafiri Akimfanyia Mema Muislamu Matendo Yake Yatamnufaisha?

Muulizaji: Je, matendo mema ya kafiri kumfanyia Muislamu yatamfaa? Jibu: Hapana. Kafiri hakuna jema lolote litalomfaa maadamu ni kafiri. Kwa kuwa matendo yake mema hayatomfaa. Kwa Kauli ya Allaah (´Azza wa Jalla): وَقَدِمْنَا إِلَىٰ مَا عَمِلُوا مِنْ عَمَلٍ فَجَعَلْنَاهُ هَبَاءً مَّنثُورًا “Na Tutayaendea yale waliyoyatenda ya ‘amali yoyote ile, Tutayafanya vumbi linalotawanyika.” (25:23) Muulizaji: Muislamu akimdhulumu kafiri vipi atalipwa huyu kafiri Aakhirah? Vipi kafiri huyu atachukua haki yake kutoka kwa Muislamu huyu? Jibu: Ni jambo linalojulikana kuwa kafiri hana mema yoyote na wala mema hayatomfaa kitu. Hana mema yatayochukuliwa na wala hana yatakayomfaa na kuchukuliwa mema kutoka kwa mwingine (huyo aliyemdhulumu) na kumpa (yeye). Kwa kuwa ukafiri hauna kitu. Matendo yake yote ni yenye kurudishwa pamoja na ukafiri wake.

Muulizaji: Je, matendo mema ya kafiri kumfanyia Muislamu yatamfaa?

Jibu: Hapana. Kafiri hakuna jema lolote litalomfaa maadamu ni kafiri. Kwa kuwa matendo yake mema hayatomfaa. Kwa Kauli ya Allaah (´Azza wa Jalla):

وَقَدِمْنَا إِلَىٰ مَا عَمِلُوا مِنْ عَمَلٍ فَجَعَلْنَاهُ هَبَاءً مَّنثُورًا
“Na Tutayaendea yale waliyoyatenda ya ‘amali yoyote ile, Tutayafanya vumbi linalotawanyika.” (25:23)

Muulizaji: Muislamu akimdhulumu kafiri vipi atalipwa huyu kafiri Aakhirah? Vipi kafiri huyu atachukua haki yake kutoka kwa Muislamu huyu?

Jibu: Ni jambo linalojulikana kuwa kafiri hana mema yoyote na wala mema hayatomfaa kitu. Hana mema yatayochukuliwa na wala hana yatakayomfaa na kuchukuliwa mema kutoka kwa mwingine (huyo aliyemdhulumu) na kumpa (yeye). Kwa kuwa ukafiri hauna kitu. Matendo yake yote ni yenye kurudishwa pamoja na ukafiri wake.