Jimaa Sana Inatokana Na Mapenzi Mengi

Alllaah (Tabaarak wa Ta´ala) Anasema: وَلَن تَسْتَطِيعُوا أَن تَعْدِلُوا بَيْنَ النِّسَاءِ وَلَوْ حَرَصْتُمْ "Na wala hamtaweza kufanya uadilifu baina ya wake, hata mkikakamia." (04:129) Ibn-ul-Mundhir kapokea ya kwamba Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anhu) kafasiri Aayah na kusema: "Ina maanisha katika jimaa." Hii ni dalili inaonesha ya kwamba mwanaume ni lazima kuwa na jimaa na wake zake wote. Jambo lisilowezekana ni kuwa na jimaa na wake wote kwa usawa. Allaah Ameliswamehe. Lakini hata hivyo haina maana aache kujamiiana na mmoja katika wake kabisa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aligawa usiku kati ya wake zake na alijiudhuru kwa Allaah kwa kusema: "Ee Allaah! Huu ndio mgawanyo wangu kwa yale ninayomiliki. Usinichukulie kwa yale Unayomiliki na si mimi."1 Imepokelewa na maimamu wanne na Ibn Hibbaan kasema kuwa ni Swahiyh. Ina maanisha mapenzi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akimpenda ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anha) zaidi kuliko wake zake wengine wane. Ni jambo linalojulikana ya kwamba mapenzi zaidi inatokana na kujamiiana zaidi. Pamoja na hivyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa na jimaa na wake zake wote. Wakati mwingine alikuwa na jimaa katika usiku mmoja huo huo na kwa ghusl (kukoga mara) moja. Wakati mwingine alikuwa akifanya ghusl kwa kila mke. Hakuna yeyote ambaye aliweza kumpa kila mmoja haki zake kama (alivyokuwa akifanya) yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Namna hii walikuwa pia Maswahabah zake wema kwa wake zao. Ibn Abiy Shaybah, 'Abd bin Humayd na Ibn-ul-Mundhir wamepokea kwamba Mujaahid kasema: "Wao - yaani Maswahaabah - walikuwa wanapendekeza ya kwamba mtu awe ni msawa kwa wake zake wote. Wakati wanajipulizia manukato kwa mke mmoja walikuwa wakifanya hivyo hivyo kwa mke wa pili." Hao watatu wamepokea pia kwamba Jaabir bin Zayd amesema: "Nilikuwa na wake wawili na nawabusu kwa kiasi sawa." Ibn Abiy Shaybah kapokea ya kwamba Muhammad bin Siyriyn kasema juu ya mwanaume na wake wawili: "Inachukizwa kwake kukoga kwa mke mmoja na kutofanya hivyo kwa mke mwingine." Mwandishi: Imaam Muhammad bin Ismaa´îl as-Swan´aaniy Chanzo: Badhl-ul-Mawjuud fi Hukm-il-A´maar wa Imr'at-il-Mafquud, uk. 278-279 -------------------------------------- (1) at-Tirmidhiy (1140), Abu Daawuud (2134), an-Nasaa'iy (8891), Ibn Maajah (1971), Ahmad (6/144) na ad-Daarimiy (2253). Ibn Abiy Haatim kasema: ”Mursal.” (al-´Ilal (1279))

Alllaah (Tabaarak wa Ta´ala) Anasema:

وَلَن تَسْتَطِيعُوا أَن تَعْدِلُوا بَيْنَ النِّسَاءِ وَلَوْ حَرَصْتُمْ
“Na wala hamtaweza kufanya uadilifu baina ya wake, hata mkikakamia.” (04:129)

Ibn-ul-Mundhir kapokea ya kwamba Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anhu) kafasiri Aayah na kusema:

“Ina maanisha katika jimaa.”

Hii ni dalili inaonesha ya kwamba mwanaume ni lazima kuwa na jimaa na wake zake wote. Jambo lisilowezekana ni kuwa na jimaa na wake wote kwa usawa. Allaah Ameliswamehe. Lakini hata hivyo haina maana aache kujamiiana na mmoja katika wake kabisa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aligawa usiku kati ya wake zake na alijiudhuru kwa Allaah kwa kusema:

“Ee Allaah! Huu ndio mgawanyo wangu kwa yale ninayomiliki. Usinichukulie kwa yale Unayomiliki na si mimi.”1

Imepokelewa na maimamu wanne na Ibn Hibbaan kasema kuwa ni Swahiyh.

Ina maanisha mapenzi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akimpenda ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anha) zaidi kuliko wake zake wengine wane. Ni jambo linalojulikana ya kwamba mapenzi zaidi inatokana na kujamiiana zaidi. Pamoja na hivyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa na jimaa na wake zake wote. Wakati mwingine alikuwa na jimaa katika usiku mmoja huo huo na kwa ghusl (kukoga mara) moja. Wakati mwingine alikuwa akifanya ghusl kwa kila mke. Hakuna yeyote ambaye aliweza kumpa kila mmoja haki zake kama (alivyokuwa akifanya) yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Namna hii walikuwa pia Maswahabah zake wema kwa wake zao. Ibn Abiy Shaybah, ‘Abd bin Humayd na Ibn-ul-Mundhir wamepokea kwamba Mujaahid kasema:

“Wao – yaani Maswahaabah – walikuwa wanapendekeza ya kwamba mtu awe ni msawa kwa wake zake wote. Wakati wanajipulizia manukato kwa mke mmoja walikuwa wakifanya hivyo hivyo kwa mke wa pili.”

Hao watatu wamepokea pia kwamba Jaabir bin Zayd amesema:

“Nilikuwa na wake wawili na nawabusu kwa kiasi sawa.”

Ibn Abiy Shaybah kapokea ya kwamba Muhammad bin Siyriyn kasema juu ya mwanaume na wake wawili:

“Inachukizwa kwake kukoga kwa mke mmoja na kutofanya hivyo kwa mke mwingine.”

Mwandishi: Imaam Muhammad bin Ismaa´îl as-Swan´aaniy
Chanzo: Badhl-ul-Mawjuud fi Hukm-il-A´maar wa Imr’at-il-Mafquud, uk. 278-279

————————————–
(1) at-Tirmidhiy (1140), Abu Daawuud (2134), an-Nasaa’iy (8891), Ibn Maajah (1971), Ahmad (6/144) na ad-Daarimiy (2253). Ibn Abiy Haatim kasema: ”Mursal.” (al-´Ilal (1279))


  • Kitengo: Uncategorized , Fiqh
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Tuesday 24th, December 2013