Jihaad Si Wajibu Kwa Waislamu Wote

Imaam Ibn ´Uthaytmiyn: Tunasema bila shaka kutafuta elimu ya Kishari´ah ni katika bora ya matendo mema. Bali linakwenda sambamba na Jihaad katika njia ya Allaah. Kama Alivyosema Allaah (Tabaaka wa Ta´ala): وَمَا كَانَ الْمُؤْمِنُونَ لِيَنفِرُواْ كَآفَّةً فَلَوْلاَ نَفَرَ مِن كُلِّ فِرْقَةٍ مِّنْهُمْ طَآئِفَةٌ لِّيَتَفَقَّهُواْ فِي الدِّينِ وَلِيُنذِرُواْ قَوْمَهُمْ إِذَا رَجَعُواْ إِلَيْهِمْ لَعَلَّهُمْ يَحْذَرُونَ ”Wala haiwafalii Waumini kutoka wote. Lakini kwanini hawatoki baadhi katika kila kundi miongoni mwao, wakajifunze vyema Dini, na kisha waje kuwaonya wenzao watakapo warejea, ili wapate kujihadharisha?” (at-Tawbah 09 : 122) Kabainisha Allaah (´Azza wa Jalla) kuwa waumini haiwezekani wakaenda wote kwenye Jihaad katika njia ya Allaah, kwa kuwa hilo linapelekea mambo mengi muhimu yote husimama ambayo Uislamu inapaswa kusimama nayo. Kutokana na hili tunapata kujua kuwa Jihaad haiwezi kuwa Fardhi ‘Ayn kwa kila Muislamu kama wanavyodai baadhi ya watu leo kuwa Jihaad ni Fardhi ‘Ayn kwa kila Muislamu. Hili ni kosa linakhalifu Qur-aan. Kwa kuwa Allaah Kasema: وَمَا كَانَ الْمُؤْمِنُونَ لِيَنفِرُواْ كَآفَّةً ”Wala haiwafalii Waumini kutoka wote.” (at-Tawbah 09 : 122) Kisha akaamrisha waende baadhi yao na wengine wabaki ili waisome Dini ya Allaah na wawaonye wenzao watakaporejea. Lakini Jihaad inakuwa Fardhi ‘Ayn katika masuala khaswa.

Imaam Ibn ´Uthaytmiyn:

Tunasema bila shaka kutafuta elimu ya Kishari´ah ni katika bora ya matendo mema. Bali linakwenda sambamba na Jihaad katika njia ya Allaah. Kama Alivyosema Allaah (Tabaaka wa Ta´ala):

وَمَا كَانَ الْمُؤْمِنُونَ لِيَنفِرُواْ كَآفَّةً فَلَوْلاَ نَفَرَ مِن كُلِّ فِرْقَةٍ مِّنْهُمْ طَآئِفَةٌ لِّيَتَفَقَّهُواْ فِي الدِّينِ وَلِيُنذِرُواْ قَوْمَهُمْ إِذَا رَجَعُواْ إِلَيْهِمْ لَعَلَّهُمْ يَحْذَرُونَ
”Wala haiwafalii Waumini kutoka wote. Lakini kwanini hawatoki baadhi katika kila kundi miongoni mwao, wakajifunze vyema Dini, na kisha waje kuwaonya wenzao watakapo warejea, ili wapate kujihadharisha?” (at-Tawbah 09 : 122)

Kabainisha Allaah (´Azza wa Jalla) kuwa waumini haiwezekani wakaenda wote kwenye Jihaad katika njia ya Allaah, kwa kuwa hilo linapelekea mambo mengi muhimu yote husimama ambayo Uislamu inapaswa kusimama nayo.
Kutokana na hili tunapata kujua kuwa Jihaad haiwezi kuwa Fardhi ‘Ayn kwa kila Muislamu kama wanavyodai baadhi ya watu leo kuwa Jihaad ni Fardhi ‘Ayn kwa kila Muislamu. Hili ni kosa linakhalifu Qur-aan. Kwa kuwa Allaah Kasema:

وَمَا كَانَ الْمُؤْمِنُونَ لِيَنفِرُواْ كَآفَّةً
”Wala haiwafalii Waumini kutoka wote.” (at-Tawbah 09 : 122)

Kisha akaamrisha waende baadhi yao na wengine wabaki ili waisome Dini ya Allaah na wawaonye wenzao watakaporejea. Lakini Jihaad inakuwa Fardhi ‘Ayn katika masuala khaswa.


  • Author: Imaam Muhammad bin Swaalih Ibn ´Uthaymiyn. Liqaa' al-Baab al-Maftuuh (164 A)
  • Kitengo: Uncategorized , Fiqh
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Friday 18th, October 2013