Je, Salafiyyah Ni “Wahhaabiyyah”?

Ahl-us-Sunnah wanajinasibisha na Sunnah, wakati makundi mengine yanajinasibisha na mapote yao ya uongo, kwa mfano Jabriyyah, Qadariyyah, Murji-ah, Imaamiyyah pote la maimamu kumi na mbili au watu maalumu, kwa mfano Jahmiyyah, Zaydiyyah, Ash'ariyyah na Ibaadhiyyah. Hata hivyo, haitakiwi kusema kwamba neno "Wahhaabiyyah" ambalo linanasibishwa na Shaykh Muhammad bin 'Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) ni katika aina hii. Sawa wakati wa Shaykh Muhammad (Rahimahu Allaah) na baada yake Ahl-us-Sunnah hawakujiita kamwe kwa jina hilo, kwa kuwa hakuja na kitu kipya ili waweze kujinasibisha kwalo. Badala yake alikuwa akifuata yale ambayo Salaf-us-Swaalih waliyokuwa wakifuata; alikuwa ameshikamana na Sunnah, kuisambaza na kuipa nguvu. Kinyume chake, ni wale ambao wanachukia Da´wah ya Shaykh Muhammad bin 'Abdil-Wahhaab ndio hutamka unasibisho huu ili kutaka kuwatatiza watu. Vile vile, wanafanya hivyo ili kutaka kuwakimbiza watu kufuata haki na uongofu na kwa ajili hiyo wabaki katika hali yao ya Bid´ah na mambo mengine yaliyozushwa ambayo yanaenda kinyume na Manhaj ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.

Ahl-us-Sunnah wanajinasibisha na Sunnah, wakati makundi mengine yanajinasibisha na mapote yao ya uongo, kwa mfano Jabriyyah, Qadariyyah, Murji-ah, Imaamiyyah pote la maimamu kumi na mbili au watu maalumu, kwa mfano Jahmiyyah, Zaydiyyah, Ash’ariyyah na Ibaadhiyyah. Hata hivyo, haitakiwi kusema kwamba neno “Wahhaabiyyah” ambalo linanasibishwa na Shaykh Muhammad bin ‘Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) ni katika aina hii. Sawa wakati wa Shaykh Muhammad (Rahimahu Allaah) na baada yake Ahl-us-Sunnah hawakujiita kamwe kwa jina hilo, kwa kuwa hakuja na kitu kipya ili waweze kujinasibisha kwalo. Badala yake alikuwa akifuata yale ambayo Salaf-us-Swaalih waliyokuwa wakifuata; alikuwa ameshikamana na Sunnah, kuisambaza na kuipa nguvu. Kinyume chake, ni wale ambao wanachukia Da´wah ya Shaykh Muhammad bin ‘Abdil-Wahhaab ndio hutamka unasibisho huu ili kutaka kuwatatiza watu. Vile vile, wanafanya hivyo ili kutaka kuwakimbiza watu kufuata haki na uongofu na kwa ajili hiyo wabaki katika hali yao ya Bid´ah na mambo mengine yaliyozushwa ambayo yanaenda kinyume na Manhaj ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.


  • Author: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad. "Rifqan Ahl-us-Sunnah bi Ahl-is-Sunnah”, uk. 5-6
  • Kitengo: Uncategorized , Manhaj
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 12th, January 2014