Je Mtume (´alayhis-Salaam) Anahudhuria Katika Sherehe Ya Maulidi?

Imaam Ibn Baaz: Baadhi ya watu wanaamini ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) anahudhuria wakati wa sherehe ya Maulidi. Hii ndio sababu ya wao kumkaribisha huko. Jambo hili ni katika uongo mkubwa sana na ujinga wa kuchukiza. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) hatotoka nje ya kaburi lake mpaka Siku ya Qiyaamah. Hana mawasiliano na mtu yoyote. Hahudhurii katika mkusanyiko wowote. Bado yuko katika kaburi lake mpaka Siku ya Qiyaamah. Nafsi yake iko kwa Mola katika ngazi ya juu, katika makazi ya maisha ya kupendeza. Allaah (Ta´ala) Kasema katika Suurat "al-Mu'minuun": ثم إنكم بعد ذلك لميتون ثم إنكم يوم القيامة تبعثون “Kisha nyinyi baada ya hayo, ni wenye kufa. Kisha hakika nyinyi Siku ya Qiyaamah mtafufuliwa.”(23:15-16) Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kasema: "Mimi ndio mtu wa kwanza atakayetoka ndani ya kaburi siku ya Qiyaamah. Mimi ndo muombezi wa kwanza. Mimi ndio wa kwanza ambaye Shafaa´ah uombezi wake utakubaliwa. " Ninaomba baraka na salaam za Mola Wake ziwe pamoja naye. Aayah na Hadiyth hii tukufu - na Aayah na Hadiyth zingine – zinatoa dalili ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) na wengine wote wamekufa au watakufa. Watatoka katika makaburi yao siku ya Qiyaamah. Suala hili wamekubaliana juu yake wanachuoni wa Waislamu. Kwa hivyo, Waislamu wote wanatakiwa kuzingatia masuala haya. Aidha, ni lazima watahadhari na Bid´ah na ukhurafi wa watu wajinga na mfano wao waliozusha. Allaah Hakuteremsha dalili yoyote kuhusiana na masuala haya. Mwandishi: Imaam 'Abdul-' Aziyz bin 'Abdillaah bin Baaz Fataawaa Arkan-ul-Islam, uk. 109-110 Daar-ud-Daa'iy, 1420

Imaam Ibn Baaz:

Baadhi ya watu wanaamini ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) anahudhuria wakati wa sherehe ya Maulidi. Hii ndio sababu ya wao kumkaribisha huko. Jambo hili ni katika uongo mkubwa sana na ujinga wa kuchukiza. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) hatotoka nje ya kaburi lake mpaka Siku ya Qiyaamah. Hana mawasiliano na mtu yoyote. Hahudhurii katika mkusanyiko wowote. Bado yuko katika kaburi lake mpaka Siku ya Qiyaamah. Nafsi yake iko kwa Mola katika ngazi ya juu, katika makazi ya maisha ya kupendeza. Allaah (Ta´ala) Kasema katika Suurat “al-Mu’minuun”:

ثم إنكم بعد ذلك لميتون ثم إنكم يوم القيامة تبعثون
“Kisha nyinyi baada ya hayo, ni wenye kufa. Kisha hakika nyinyi Siku ya Qiyaamah mtafufuliwa.”(23:15-16)

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kasema:

“Mimi ndio mtu wa kwanza atakayetoka ndani ya kaburi siku ya Qiyaamah. Mimi ndo muombezi wa kwanza. Mimi ndio wa kwanza ambaye Shafaa´ah uombezi wake utakubaliwa. ”

Ninaomba baraka na salaam za Mola Wake ziwe pamoja naye.

Aayah na Hadiyth hii tukufu – na Aayah na Hadiyth zingine – zinatoa dalili ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na wengine wote wamekufa au watakufa. Watatoka katika makaburi yao siku ya Qiyaamah. Suala hili wamekubaliana juu yake wanachuoni wa Waislamu. Kwa hivyo, Waislamu wote wanatakiwa kuzingatia masuala haya. Aidha, ni lazima watahadhari na Bid´ah na ukhurafi wa watu wajinga na mfano wao waliozusha. Allaah Hakuteremsha dalili yoyote kuhusiana na masuala haya.

Mwandishi: Imaam ‘Abdul-‘ Aziyz bin ‘Abdillaah bin Baaz
Fataawaa Arkan-ul-Islam, uk. 109-110
Daar-ud-Daa’iy, 1420


  • Kitengo: Uncategorized , Manhaj
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Thursday 24th, October 2013