Je, Binaadamu Anaweza Kuoa Jini La Kike?

´Allaamah al-Waadi´iy: Ama kuoa Majini, wametofautiana wanachuoni. Kuna wanaosema kwamba si Halali, kwa Kauli ya Allaah (´Azza wa Jalla): وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَاجًا لِّتَسْكُنُوا إِلَيْهَا وَجَعَلَ بَيْنَكُم مَّوَدَّةً وَرَحْمَةً "Na katika Aayah Zake ni kwamba Amekuumbieni kutokana na nafsi zenu (jinsi moja) wake ili mpate utulivu kwao; na Amekujaalieni baina yenu mapenzi na Rahmah." (30:21) Na katika wanachuoni kuna waliojuzisha hilo na kusema ya kwamba hakuna dalili inayokataza hilo, na hii ndio kauli ya dhahiri. Hakuna dalili inayokataza. Inajuzu kwa mwanaume kuoa Jini, na inajuzu kwa Jini kuoa binaadamu lakini asimuudhi. Pia ni sharti kujua kama Jini hilo ni Muislamu mwanaume, pia ni sharti kujua kuwa ni Muislamu mwanamke. Asiwe ni Kafiri.

´Allaamah al-Waadi´iy:

Ama kuoa Majini, wametofautiana wanachuoni. Kuna wanaosema kwamba si Halali, kwa Kauli ya Allaah (´Azza wa Jalla):

وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَاجًا لِّتَسْكُنُوا إِلَيْهَا وَجَعَلَ بَيْنَكُم مَّوَدَّةً وَرَحْمَةً
“Na katika Aayah Zake ni kwamba Amekuumbieni kutokana na nafsi zenu (jinsi moja) wake ili mpate utulivu kwao; na Amekujaalieni baina yenu mapenzi na Rahmah.” (30:21)

Na katika wanachuoni kuna waliojuzisha hilo na kusema ya kwamba hakuna dalili inayokataza hilo, na hii ndio kauli ya dhahiri. Hakuna dalili inayokataza. Inajuzu kwa mwanaume kuoa Jini, na inajuzu kwa Jini kuoa binaadamu lakini asimuudhi. Pia ni sharti kujua kama Jini hilo ni Muislamu mwanaume, pia ni sharti kujua kuwa ni Muislamu mwanamke. Asiwe ni Kafiri.