ISIS Ni Maadui Wa Uislamu

Enyi watu! Mcheni Allaah (Ta´ala) ukweli wa kumcha. Enyi waja wa Allaah! Tunasikia na kuona maono mabaya na picha chafu ya jarima hizi kubwa zinazotoka kwa nafsi zenye machukizo na mikono mibaya ambayo ni adui wa Uislamu kwa njia zake zote. Jarima hizi kubwa zinaenezwa kwenye vyombo vya khabari ili watu waweze kuona kipi kinachofanywa na watu wanaojinasibisha na Uislamu katika miji ya Kiislamu. Wanauana wao kwa wao. Wanaangamizana wao kwa wao. Makundi haya yenye jarima na yenye madhambi yanayomwaga damu kwa dhuluma pasina sababu yoyote. Inahusiana tu na dhuluma na uadui na kuwatii maadui. Makundi haya yamezalishwa na huduma za khabari za kidunia ambazo hamu yao kubwa ni kuwatumia Waislamu vibaya na kumwaga damu zao pasina haki. Wanafanya mambo ya jarima. Inahusiana tu na jarima kubwa kubwa na majanga. Jambo lingine ni kuwa Uislamu uko mbali kabisa na tabia hizi chafu. Allaah na Mtume Wake (Swalla Allahu ´alayhi wa sallam) wametakasika na tabia hizi chafu. Kila Muislamu ni mwenye kujitenga mbali na tabia hizi, anazichukia na anaonelea kuwa wale wenye kuhalalisha damu za Waislamu wamepotea. Watu hawa wamewaua watu wenye kuswali na wenye kufunga. Wamewaua watu wenye kusema hapana mola mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah. Wamewaua kwa dhuluma na uadui. Wakati Usaamah bin Zayd alipokuwa anataka kumuua kafiri mmoja, yule kafiri alisema hapana mola mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Allaah. Hata hivyo Usaamah akawa amemuua kwa kufikiria ya kwamba kafiri yule amesema hivo tu kwa sababu ya uoga. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwambia: “Umemuua baada ya kusema hapana mola mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Allaah? Utafanya nini siku ya Qiyaamah lau akija na Shahaadah? Umeufunua moyo wake?” Yote haya ni maonyo ya mauaji. Watu hawa wanafanya machafu haya kwa kutumia jina la Uislamu. Jambo la tatu ni kwamba mauaji haya ni ugaidi ulopangwa na uadui wa kishenzi, dhuluma na upotevu, uharibifu wa mali, uharibifu wa miji na kuivamia [sauti haiko wazi] miji ya Kiislamu. Watu hawa hamu yao kubwa ni kuleta kila aina ya ouvu, shari na janga. Baya zaidi kuliko haya ni kuwa wanasema kuwa ni Ukhaliyfah wa Kiislamu, Jihaad ya Kiislamu na haya na yale. Allaah Ametakasika! Jihaad ya haki iko wapi na Uislamu uko wapi? Watu hawa sio Mujaahiduun. Si lolote isipokuwa ni watu wa dhuluma na uadui na wateka nyara wapotevu ambao hamu yao kubwa ni kuwachochea maadui wa Uislamu ambao wanakuja kuwatumia ili kuvamia miji ya Kiislamu na ili, kwa mujibu wao, kutaka kuwasitisha. Haya ndio wanayotaka watu hawa wapotevu! Haya ndio wanayotaka waasi hawa! Vijana wa Kiislamu! Mcheni Allaah juu ya nafsi zenu! Tahadharini kujiunga na watu hawa! Tahadharini na kuwa na dhana nzuri kwa watu hawa! Ni maadui zenu na ni maadui wa Dini yenu! Msifikirie kuwa matendo yao ni mazuri. Matendo yao yote ni machafu, upotevu na ni makosa. Watu hawa ni waharibifu. Tunamuomba Allaah Aitakase miji ya Kiislamu na wao – Hakika yeye juu ya kila kitu ni Muweza.

Enyi watu! Mcheni Allaah (Ta´ala) ukweli wa kumcha. Enyi waja wa Allaah! Tunasikia na kuona maono mabaya na picha chafu ya jarima hizi kubwa zinazotoka kwa nafsi zenye machukizo na mikono mibaya ambayo ni adui wa Uislamu kwa njia zake zote. Jarima hizi kubwa zinaenezwa kwenye vyombo vya khabari ili watu waweze kuona kipi kinachofanywa na watu wanaojinasibisha na Uislamu katika miji ya Kiislamu. Wanauana wao kwa wao. Wanaangamizana wao kwa wao. Makundi haya yenye jarima na yenye madhambi yanayomwaga damu kwa dhuluma pasina sababu yoyote. Inahusiana tu na dhuluma na uadui na kuwatii maadui. Makundi haya yamezalishwa na huduma za khabari za kidunia ambazo hamu yao kubwa ni kuwatumia Waislamu vibaya na kumwaga damu zao pasina haki. Wanafanya mambo ya jarima. Inahusiana tu na jarima kubwa kubwa na majanga.

Jambo lingine ni kuwa Uislamu uko mbali kabisa na tabia hizi chafu. Allaah na Mtume Wake (Swalla Allahu ´alayhi wa sallam) wametakasika na tabia hizi chafu. Kila Muislamu ni mwenye kujitenga mbali na tabia hizi, anazichukia na anaonelea kuwa wale wenye kuhalalisha damu za Waislamu wamepotea. Watu hawa wamewaua watu wenye kuswali na wenye kufunga. Wamewaua watu wenye kusema hapana mola mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah. Wamewaua kwa dhuluma na uadui. Wakati Usaamah bin Zayd alipokuwa anataka kumuua kafiri mmoja, yule kafiri alisema hapana mola mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Allaah. Hata hivyo Usaamah akawa amemuua kwa kufikiria ya kwamba kafiri yule amesema hivo tu kwa sababu ya uoga. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwambia:

“Umemuua baada ya kusema hapana mola mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Allaah? Utafanya nini siku ya Qiyaamah lau akija na Shahaadah? Umeufunua moyo wake?”

Yote haya ni maonyo ya mauaji. Watu hawa wanafanya machafu haya kwa kutumia jina la Uislamu.

Jambo la tatu ni kwamba mauaji haya ni ugaidi ulopangwa na uadui wa kishenzi, dhuluma na upotevu, uharibifu wa mali, uharibifu wa miji na kuivamia [sauti haiko wazi] miji ya Kiislamu. Watu hawa hamu yao kubwa ni kuleta kila aina ya ouvu, shari na janga. Baya zaidi kuliko haya ni kuwa wanasema kuwa ni Ukhaliyfah wa Kiislamu, Jihaad ya Kiislamu na haya na yale. Allaah Ametakasika! Jihaad ya haki iko wapi na Uislamu uko wapi? Watu hawa sio Mujaahiduun. Si lolote isipokuwa ni watu wa dhuluma na uadui na wateka nyara wapotevu ambao hamu yao kubwa ni kuwachochea maadui wa Uislamu ambao wanakuja kuwatumia ili kuvamia miji ya Kiislamu na ili, kwa mujibu wao, kutaka kuwasitisha. Haya ndio wanayotaka watu hawa wapotevu! Haya ndio wanayotaka waasi hawa!

Vijana wa Kiislamu! Mcheni Allaah juu ya nafsi zenu! Tahadharini kujiunga na watu hawa! Tahadharini na kuwa na dhana nzuri kwa watu hawa! Ni maadui zenu na ni maadui wa Dini yenu! Msifikirie kuwa matendo yao ni mazuri. Matendo yao yote ni machafu, upotevu na ni makosa. Watu hawa ni waharibifu. Tunamuomba Allaah Aitakase miji ya Kiislamu na wao – Hakika yeye juu ya kila kitu ni Muweza.