Imaam Ibn ´Uthaymiyn Kuhusu Uongo Wa April

Ninawatahadharisha ndugu zangu Waislamu kwa wanayofanya baadhi ya wajinga juu ya uongo wa April, na nadhani iko karibu. Uongo huu ambao wameuchukua kutoka kwa mayahudi, manaswara na majusi [waabudu moto] na watu wa kufuru. Isitoshe, pamoja na kuwa ni uongo, na uongo ni haramu Kishari´ah, na ni kujifananisha na wasiokuwa Waislamu, na kujifananisha na wasiokuwa Waislamu ni haramu. Kasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Yule ambaye atajifananisha na watu, basi yeye ni katika wao.” (Kaipokea Ahmad (5114, 5115)) Kasema Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah): "Isnadi yake ni nzuri, na hali yake ndogo iwezayo kusemwa ni kwamba kuna uharamu (wa kujifananisha nao) hata kama uinje wake inaonena ukafiri kwa yule mwenye kujifananisha nao." Pamoja na kuwa kwa dhambi hizi mbili, kuna kujifedhehesha vile vile kwa Waislamu mbele ya maadui wao. Kwa kuwa ni jambo la maalumu katika tabia ya mtu, ya kwamba, yule mwigwaji hufurahia kwa yule mwenye kumwiga na kuona yeye yuko mbele kuliko huyo [anayemwiga]. Na kwa ajili hii, ndio maana kawa mdhaifu mwigaji mpaka akamwiga. Kuna kujidhalilisha kwa Muumini kwa kule kufuata kwake kichwa mchunga makafiri. Dhambi ya nne ni kuwa, aghlabu uongo huu mchafu kunawepo ndani yake kuchukua mali ya watu kwa batili na kumshtua Muislamu. Huenda akadanganya na kuwaambia watu wa nyumbani ya kwamba wana wageni leo. Jambo ambalo linafanya wanaandaa chakula kingi, nyama nyingi na mfano wa hayo. Na huenda wakawaambia jambo la kuwashtua, kama kwa mfano kuwaambia kuna ndugu ambaye kagongwa na gari na mfano wa hayo. Hili halijuzu.

Ninawatahadharisha ndugu zangu Waislamu kwa wanayofanya baadhi ya wajinga juu ya uongo wa April, na nadhani iko karibu. Uongo huu ambao wameuchukua kutoka kwa mayahudi, manaswara na majusi [waabudu moto] na watu wa kufuru. Isitoshe, pamoja na kuwa ni uongo, na uongo ni haramu Kishari´ah, na ni kujifananisha na wasiokuwa Waislamu, na kujifananisha na wasiokuwa Waislamu ni haramu. Kasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yule ambaye atajifananisha na watu, basi yeye ni katika wao.” (Kaipokea Ahmad (5114, 5115))

Kasema Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah):

“Isnadi yake ni nzuri, na hali yake ndogo iwezayo kusemwa ni kwamba kuna uharamu (wa kujifananisha nao) hata kama uinje wake inaonena ukafiri kwa yule mwenye kujifananisha nao.”

Pamoja na kuwa kwa dhambi hizi mbili, kuna kujifedhehesha vile vile kwa Waislamu mbele ya maadui wao. Kwa kuwa ni jambo la maalumu katika tabia ya mtu, ya kwamba, yule mwigwaji hufurahia kwa yule mwenye kumwiga na kuona yeye yuko mbele kuliko huyo [anayemwiga]. Na kwa ajili hii, ndio maana kawa mdhaifu mwigaji mpaka akamwiga. Kuna kujidhalilisha kwa Muumini kwa kule kufuata kwake kichwa mchunga makafiri.

Dhambi ya nne ni kuwa, aghlabu uongo huu mchafu kunawepo ndani yake kuchukua mali ya watu kwa batili na kumshtua Muislamu. Huenda akadanganya na kuwaambia watu wa nyumbani ya kwamba wana wageni leo. Jambo ambalo linafanya wanaandaa chakula kingi, nyama nyingi na mfano wa hayo. Na huenda wakawaambia jambo la kuwashtua, kama kwa mfano kuwaambia kuna ndugu ambaye kagongwa na gari na mfano wa hayo. Hili halijuzu.