Imaam Ibn ´Uthaymiyn Kuhusu Mwanamke kufanya Mash Juu Ya Mtandio

Wanachuoni wametofautiana kama inajuzu kwa mwanamke kufanya Mash juu ya mtandio (Khimaar) kichwani au hapana. Baadhi ya wanachuoni wanasema ya kwamba imekatazwa kwa kuwa Allaah (Ta´ala) Ameamrisha mtu kufanya Mash juu ya kichwa: "Na pakeni (panguseni) kwa (maji) vichwa vyenu." (05:06) Ikiwa mtu atafanya Mash juu ya mtandio, hivyo mtu atakuwa hakufanya Mash juu ya kichwa. Wengine wanamaanisha ya kwamba inajuzu. Wanalinganisha mtandio wa mwanamke na kilemba cha mwanaume. Mtandio wa mwanamke una hadhi moja sawa na kilemba cha mwanaume na una uzito wa kuuondoa sawa na kilemba cha mwanaume. Ikiwa kuna uzito [juu ya kufanya Mash juu ya kichwa] kwa sababu ya baridi au kwa sababu kuna uzito kuuvua na kuvaa tena, hivyo itakuwa inajuzu. Vinginevyo ni bora zaidi kutofanya hivyo. Vilevile hakukupokelewa jambo lolote sahihi kuhusiana na suala hili.

Wanachuoni wametofautiana kama inajuzu kwa mwanamke kufanya Mash juu ya mtandio (Khimaar) kichwani au hapana.

Baadhi ya wanachuoni wanasema ya kwamba imekatazwa kwa kuwa Allaah (Ta´ala) Ameamrisha mtu kufanya Mash juu ya kichwa:

“Na pakeni (panguseni) kwa (maji) vichwa vyenu.” (05:06)

Ikiwa mtu atafanya Mash juu ya mtandio, hivyo mtu atakuwa hakufanya Mash juu ya kichwa.

Wengine wanamaanisha ya kwamba inajuzu. Wanalinganisha mtandio wa mwanamke na kilemba cha mwanaume. Mtandio wa mwanamke una hadhi moja sawa na kilemba cha mwanaume na una uzito wa kuuondoa sawa na kilemba cha mwanaume.

Ikiwa kuna uzito [juu ya kufanya Mash juu ya kichwa] kwa sababu ya baridi au kwa sababu kuna uzito kuuvua na kuvaa tena, hivyo itakuwa inajuzu. Vinginevyo ni bora zaidi kutofanya hivyo. Vilevile hakukupokelewa jambo lolote sahihi kuhusiana na suala hili.


  • Author: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn. ash-Sharh al-Mumti´ ´alaa Zaad-il-Mustaqni´ (1/196)
  • Kitengo: Uncategorized , ´Ibaadah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Friday 10th, January 2014