Imaam Ibn ´Uthaymiyn Kuhusu Mtu Aliekuwa Akichinja Kwa Ajili Ya Asiyekuwa Allaah Kurudi Hajj Yake

Muulizaji: Kuna mtu alikuwa na kitu katika ujinga kwenye ´Aqiydah. Akawa anachinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah. Akahiji katikati ya kipindi hichi kisha baada ya muda fulani kutoka katika Hajj, akaacha kufanya hivyo na kutubu kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Je Hajj yake inalipwa kama Muislamu au hapana? Jibu: Mtu huyu anayefanya mambo yanayoivunja ´Aqiydah, kama kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah. Kisha akahiji na yeye yuko katika hali hii. Je Hajj yake imekubaliwa? Tunasema kwanza, je alikuwa ni mjinga ambaye anaonelea hakuna neno juu ya hili? Ikiwa alikuwa ni mjinga hajui kitu, Hajj yake ni sahihi. Ama ikiwa alikuwa anajua kuwa kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah ni Shirki, Hajj yake sio sahihi. Muulizaji: Yeye alikuwa anajua kuwa hilo ni haramu na alikuwa ameshasikia baadhi ya fataawa kuhusu hili. Lakini pengine alikuwa hajui kuwa anatoka katika Uislamu na yeye anaamini kuwa ikiwa hakuchinja, jambo hilo litamletea madhara kwake. Jibu: Katika hali hii bora ni yeye kurudi kufanya Hajj yake. Kwa kuwa alikuwa anajua kuwa ni haramu, lililokuwa la wajibu kwake pale alipojua kuwa ni haramu alitakikana kuachana nalo. Bora zaidi ni yeye kurudi Hajj yake.

Muulizaji: Kuna mtu alikuwa na kitu katika ujinga kwenye ´Aqiydah. Akawa anachinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah. Akahiji katikati ya kipindi hichi kisha baada ya muda fulani kutoka katika Hajj, akaacha kufanya hivyo na kutubu kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Je Hajj yake inalipwa kama Muislamu au hapana?

Jibu: Mtu huyu anayefanya mambo yanayoivunja ´Aqiydah, kama kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah. Kisha akahiji na yeye yuko katika hali hii. Je Hajj yake imekubaliwa? Tunasema kwanza, je alikuwa ni mjinga ambaye anaonelea hakuna neno juu ya hili? Ikiwa alikuwa ni mjinga hajui kitu, Hajj yake ni sahihi. Ama ikiwa alikuwa anajua kuwa kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah ni Shirki, Hajj yake sio sahihi.

Muulizaji: Yeye alikuwa anajua kuwa hilo ni haramu na alikuwa ameshasikia baadhi ya fataawa kuhusu hili. Lakini pengine alikuwa hajui kuwa anatoka katika Uislamu na yeye anaamini kuwa ikiwa hakuchinja, jambo hilo litamletea madhara kwake.

Jibu: Katika hali hii bora ni yeye kurudi kufanya Hajj yake. Kwa kuwa alikuwa anajua kuwa ni haramu, lililokuwa la wajibu kwake pale alipojua kuwa ni haramu alitakikana kuachana nalo. Bora zaidi ni yeye kurudi Hajj yake.


  • Author: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn. Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (02 A)
  • Kitengo: Uncategorized , Hajj na ´Umrah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Saturday 21st, December 2013