Imaam Ibn Muflih Nasaha Ya Huduma Ya Meno

Baada ya kula au kunywa kitu cha moto, haitakikani kula au kunywa kitu cha baridi moja kwa moja baada yake na kinyume chake. Kwa njia hiyo mtu anahifadhi meno yake na nguvu zake jambo ambalo linajulikana. Kadhalika haitakikani kwa mtu kutafuna na kukata vitu vigumu na vitu vitamu na vitu vya kupoa kama barafu na vitu vya kupoa ambavyo ni vikali. Mara nyingi kunakuja kutapika ambako kunaharibu meno. Ikiwa mtu anasikia maumivu wakati anapokula kitu cha baridi, anatakiwa kutafuta kitu cha moto kama mkate na mfano wa hayo. Ikiwa anasikia maumivu kwenye jino wakati anapokula kitu cha moto, anatakiwa kunywa maji ya baridi. Wakati wa maumivu ya meno, ni jambo la manufaa kusukutua kinywa kwa kitu kikali.

Baada ya kula au kunywa kitu cha moto, haitakikani kula au kunywa kitu cha baridi moja kwa moja baada yake na kinyume chake. Kwa njia hiyo mtu anahifadhi meno yake na nguvu zake jambo ambalo linajulikana.

Kadhalika haitakikani kwa mtu kutafuna na kukata vitu vigumu na vitu vitamu na vitu vya kupoa kama barafu na vitu vya kupoa ambavyo ni vikali. Mara nyingi kunakuja kutapika ambako kunaharibu meno.

Ikiwa mtu anasikia maumivu wakati anapokula kitu cha baridi, anatakiwa kutafuta kitu cha moto kama mkate na mfano wa hayo. Ikiwa anasikia maumivu kwenye jino wakati anapokula kitu cha moto, anatakiwa kunywa maji ya baridi. Wakati wa maumivu ya meno, ni jambo la manufaa kusukutua kinywa kwa kitu kikali.


  • Author: Imaam Muhammad bin Muflih al-Maqdisiy (d. 763). al-Aadaab ash-Shar´iyyah (3/22-23)
  • Kitengo: Uncategorized , Dawa
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Monday 20th, January 2014