Imaam ash-Shaafi´iy Nasaha Za Kidaktari

ash-Shaafi´iy (Radhiya Allaahu ´anhu) amesema: "Vitu vine vinaupa nguvu mwili: kula nyama, kunukia manukato, kuoga mara nyingi bila ya kufanya jimaa na kuvaa linseed.[1] Vitu vine vinaudhoofisha mwili: kufanya jimaa mara nyingi, kuwa na maudhiko sana, kunywa maji mengi ilihali tumbo liko tupu na kula vitu vikali mara kwa mara. Vitu vine vinafanya kuona kunakuwa na nguvu: kukaa kwenye Ka´abah, kupaka wanja machoni kabla kwenda kulala, kuangalia rangi ya kijani na kusafisha sehemu za vikao. Vitu vine vinadhoofisha kuona: kutazama najisi, watu waliosulubiwa, tupu ya mwanamke na kukaa na mgongo umeelewa dhidi na Ka´abah. Vitu vine vinafanya jimaa kuwa na nguvu: kula nyama ya ndege, ..., karanga na tango. Vitu vine vinaipa nguvu (kuiiamrisha) akili: kujiepusha na maneno ya kipuuzi, kutumia Siwaak, kukaa na watu wema na kukaa na wanachuoni." ---------- (1) Ni mmea wa uwa la rangi ya bluu ambalo mafuta yake na nyuzi ya nguo hutolewa. Tazama kamusi ya Nordstedts

ash-Shaafi´iy (Radhiya Allaahu ´anhu) amesema:

“Vitu vine vinaupa nguvu mwili: kula nyama, kunukia manukato, kuoga mara nyingi bila ya kufanya jimaa na kuvaa linseed.[1]

Vitu vine vinaudhoofisha mwili: kufanya jimaa mara nyingi, kuwa na maudhiko sana, kunywa maji mengi ilihali tumbo liko tupu na kula vitu vikali mara kwa mara.

Vitu vine vinafanya kuona kunakuwa na nguvu: kukaa kwenye Ka´abah, kupaka wanja machoni kabla kwenda kulala, kuangalia rangi ya kijani na kusafisha sehemu za vikao.

Vitu vine vinadhoofisha kuona: kutazama najisi, watu waliosulubiwa, tupu ya mwanamke na kukaa na mgongo umeelewa dhidi na Ka´abah.

Vitu vine vinafanya jimaa kuwa na nguvu: kula nyama ya ndege, …, karanga na tango.

Vitu vine vinaipa nguvu (kuiiamrisha) akili: kujiepusha na maneno ya kipuuzi, kutumia Siwaak, kukaa na watu wema na kukaa na wanachuoni.”

———-
(1) Ni mmea wa uwa la rangi ya bluu ambalo mafuta yake na nyuzi ya nguo hutolewa. Tazama kamusi ya Nordstedts


  • Author: Imaam Muhammad bin Muflih al-Maqdisiy (d. 763). al-Aadaab ash-Shar´iyyah (3/13-14)
  • Kitengo: Uncategorized , Dawa
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Monday 20th, January 2014