Imaam al-Fawzaan Kuhusu Kubusa Midomoni

al-Mardaawiy anasema: "Inachukizwa kubusu mdomoni." Bi maana ya kwamba ni paja la uso ndio linalobuswa na sio kwenye mdomo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimbusu Ja´far kati ya macho. Hali kadhalika mtu anaweza kubusu kichwa. Ama kuhusu kwenye midomo, inaruhusiwa tu kati ya mume na mke. Haitakiwi mtu kubusu wanawake wengine mdomoni hata kama watakuwa ni ndugu. Hali kadhalika (haitakiwi) kubusu kwenye mashavu ikiwa kunakhofiwa fitina. Hata hivyo ikiwa hakukhofiwi fitina, hakuna neno. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimbusu Faatwimah kwenye mashavu. Hali kadhalika inajuzu kubusu kwenye mikono kwa mtu ambaye anamsalimia.

al-Mardaawiy anasema:

“Inachukizwa kubusu mdomoni.”

Bi maana ya kwamba ni paja la uso ndio linalobuswa na sio kwenye mdomo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimbusu Ja´far kati ya macho. Hali kadhalika mtu anaweza kubusu kichwa.

Ama kuhusu kwenye midomo, inaruhusiwa tu kati ya mume na mke. Haitakiwi mtu kubusu wanawake wengine mdomoni hata kama watakuwa ni ndugu.

Hali kadhalika (haitakiwi) kubusu kwenye mashavu ikiwa kunakhofiwa fitina. Hata hivyo ikiwa hakukhofiwi fitina, hakuna neno. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimbusu Faatwimah kwenye mashavu.

Hali kadhalika inajuzu kubusu kwenye mikono kwa mtu ambaye anamsalimia.


  • Author: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan. Ittihaaf-ut-Tullaab, uk. 215
  • Kitengo: Uncategorized , Familia
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Tuesday 7th, January 2014