Imaam al-Fawzaan Kuhusu Chuki Ya al-Buutwiy Kwa Salafiyyah Na Salafiyyuun

Nimesoma kitabu kwa jina "as-Salafiyyah Marhalah Zamaniyyah Mubaarakah” kilichoandikwa na Dr. Muhammad Sa´iyd Ramadhaan al-Buutwiy. Nimeshangazwa na kichwa cha khabari ambacho kinatoa ishara kwamba Salaf haina madhehebu na mfumo wowote ambao tunalazimika kujifunza na kushikamana nao na kujitenga mbali na madhehebu yanayoenda kinyume nayo. Lakini nilipoanza kusoma kitabu, nikaona yaliyomo ndani ni ya ajabu zaidi kuliko kichwa cha khabari. Humo anasema kuwa ni Bid´ah kuchukua Salafiyyah kama madhehebu na kuwavamia Salafiyyuun. Najiuliza kuhusu mashambulizi haya mabaya dhidi ya Salafiyyah na Salafiyyuun - ikiwa ni pamoja na wale wa zamani kama Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah na Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin 'Abdil-Wahhab – yanatokamana na kuchukia kwake Bid´ah na kwa hivyo ufahamu wake kuwa ni Bid´ah kuwa na Salafiyyah kama madhehebu. Katu maishani! Sababu sio kuchukia kwake Bid´ah. Kwa sababu tumemuona akiwanusuru watu wa Bid´ah wengi katika kitabu hiki. Ananusuru Adhkaar za Bid´ah za Suufiyyah, Du´aa za pamoja baada ya Swalah za faradhi, jambo ambalo ni Bid´ah, kusafiri kwenda katika kaburi la Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam), jambo ambalo ni Bid´ah... Imetubainikia – na Allaah ndiye Anajua zaidi – ya kwamba sababu ya mashambulizi haya ni usumbufu kwa maoni ya Salafiyyah ambayo yanapambana na Bid´ah na fikira ambazo Waislamu wengi wa leo wako nazo na ambazo haziafikiana na mfumo wa Salaf. Mwandishi: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan Chanzo: Ta´qiybaat ´alaa Kitaab as-Salafiyyah laysat Madhhaban, uk. 3-4 Toleo la: 01-06-2014 Imefasiriwa na: Wanachuoni.com

Nimesoma kitabu kwa jina “as-Salafiyyah Marhalah Zamaniyyah Mubaarakah” kilichoandikwa na Dr. Muhammad Sa´iyd Ramadhaan al-Buutwiy. Nimeshangazwa na kichwa cha khabari ambacho kinatoa ishara kwamba Salaf haina madhehebu na mfumo wowote ambao tunalazimika kujifunza na kushikamana nao na kujitenga mbali na madhehebu yanayoenda kinyume nayo. Lakini nilipoanza kusoma kitabu, nikaona yaliyomo ndani ni ya ajabu zaidi kuliko kichwa cha khabari. Humo anasema kuwa ni Bid´ah kuchukua Salafiyyah kama madhehebu na kuwavamia Salafiyyuun. Najiuliza kuhusu mashambulizi haya mabaya dhidi ya Salafiyyah na Salafiyyuun – ikiwa ni pamoja na wale wa zamani kama Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah na Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ‘Abdil-Wahhab – yanatokamana na kuchukia kwake Bid´ah na kwa hivyo ufahamu wake kuwa ni Bid´ah kuwa na Salafiyyah kama madhehebu. Katu maishani! Sababu sio kuchukia kwake Bid´ah. Kwa sababu tumemuona akiwanusuru watu wa Bid´ah wengi katika kitabu hiki. Ananusuru Adhkaar za Bid´ah za Suufiyyah, Du´aa za pamoja baada ya Swalah za faradhi, jambo ambalo ni Bid´ah, kusafiri kwenda katika kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam), jambo ambalo ni Bid´ah…

Imetubainikia – na Allaah ndiye Anajua zaidi – ya kwamba sababu ya mashambulizi haya ni usumbufu kwa maoni ya Salafiyyah ambayo yanapambana na Bid´ah na fikira ambazo Waislamu wengi wa leo wako nazo na ambazo haziafikiana na mfumo wa Salaf.

Mwandishi: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: Ta´qiybaat ´alaa Kitaab as-Salafiyyah laysat Madhhaban, uk. 3-4
Toleo la: 01-06-2014
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com


  • Kitengo: Uncategorized , al-Buutwiy, Muhammad Sa´iyd Ramadhaan
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 1st, June 2014