Imaam al-Albaaniy Kuhusu Ujitoleaji Wa Muhanga Unaofanyika Leo

Suala hili linanipelekea katika suala lingine ambalo linatendeka hivi leo. Nimeshaulizwa mara nyingi. Ni yale yanayoitwa kujitoa muhanga. Je, inajuzu? Haya yapo hivi leo na ni lazima kuyajibu. Inajuzu na haijuzu. Yanayopitika hivi leo hayajuzu kwa kuwa ni msukumo wa binafsi. Yanatokana na hisia mbaya ambazo hazitiliwi mpaka na Shari´ah wala akili. Hakuna tofauti kati ya Muislamu huyu anayejiua, m-communist au mjapani mwenye kufanya hivyo, kama ilivyotokea wakati wa vita baina yao na wamarekani. Yote ni sawa. Hakuna yeyote anayefanya hivyo kwa ajili ya Dini yake au kauli za wanachuoni. Haijuzu. Ama lau kungelikuwa mtawala Muislamu, mwanachuoni ambaye anaongoza jeshi lake na akasoma kitovu cha uanaskari, uwanja wa vita na kadhalika... Anayelinganisha baina ya manufaa na madhara. Pindi anapoona kuwa manufaa ya kujitoa muhanga ni makubwa kuliko Muislamu huyu anayekosekana, hapo ndipo tunapoona kuwa inajuzu. Hili limetokea wakati wa vita vya kwanza vya Waislamu na mfano wa hilo ni ushindi wa Damasko. Kulifanyika baadhi ya ujitoleaji wa muhanga. Askari alikuwa anaweza kumuomba kiongozi wao idhini ya kufa shahidi na kushambulia kundi la warumi na wengine. Anawaua mpaka na wao wanamuua. Kiongozi alikuwa anaweza kumpa idhini na mtu huyo anawavamia mpaka anakuwa ni mwenye kufa shahidi katika njia ya Allaah (Ta´ala).

Suala hili linanipelekea katika suala lingine ambalo linatendeka hivi leo. Nimeshaulizwa mara nyingi. Ni yale yanayoitwa kujitoa muhanga. Je, inajuzu? Haya yapo hivi leo na ni lazima kuyajibu. Inajuzu na haijuzu. Yanayopitika hivi leo hayajuzu kwa kuwa ni msukumo wa binafsi. Yanatokana na hisia mbaya ambazo hazitiliwi mpaka na Shari´ah wala akili. Hakuna tofauti kati ya Muislamu huyu anayejiua, m-communist au mjapani mwenye kufanya hivyo, kama ilivyotokea wakati wa vita baina yao na wamarekani. Yote ni sawa. Hakuna yeyote anayefanya hivyo kwa ajili ya Dini yake au kauli za wanachuoni. Haijuzu.

Ama lau kungelikuwa mtawala Muislamu, mwanachuoni ambaye anaongoza jeshi lake na akasoma kitovu cha uanaskari, uwanja wa vita na kadhalika… Anayelinganisha baina ya manufaa na madhara. Pindi anapoona kuwa manufaa ya kujitoa muhanga ni makubwa kuliko Muislamu huyu anayekosekana, hapo ndipo tunapoona kuwa inajuzu.

Hili limetokea wakati wa vita vya kwanza vya Waislamu na mfano wa hilo ni ushindi wa Damasko. Kulifanyika baadhi ya ujitoleaji wa muhanga. Askari alikuwa anaweza kumuomba kiongozi wao idhini ya kufa shahidi na kushambulia kundi la warumi na wengine. Anawaua mpaka na wao wanamuua. Kiongozi alikuwa anaweza kumpa idhini na mtu huyo anawavamia mpaka anakuwa ni mwenye kufa shahidi katika njia ya Allaah (Ta´ala).


  • Author: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy. Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (533)
  • Kitengo: Uncategorized , Fiqh
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 9th, February 2014