Imaam al-Albaaniy Kuhusu Sayyid Qutwub Na ´Abdullaah ´Azzaam

Imaam, ´Allaamah na Shaykh Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy amesema katika mjadala mmoja na mtu: Umesikia kukizungumziwa kuhusu ´Abdullaah ´Azzaam? Mtu yule: Ndio! Shaykh: ´Abdullaah ´Azzaam hapa alikuwa na al-Ikhwaan al-Muslimuun. Miaka misaba au minane iliyopita al-Ikhwaan al-Muslimuun walinisusa. Wakasusa duruus zangu na Da´wah yangu na ´Abdullaah ´Azzaam ndio alikuwa mtu pekee katika al-Ikhwaan al-Muslimuun ambaye alikuwa kila siku anakuja katika duruus zangu na daftari dogo na kalamu ndogo sana. Wakati kulitoka maamuzi ya kususa mawaidha yangu, hakutokea tena. Siku moja nikakutana naye katika Msikiti Suhayb nje ya Swalah. Nikamsalimia na yeye akanisalimia kwa aibu kwa sababu alivunja makubaliano. Nikamwambia: Haya ndio Uislamu unaamrisha? Akasema: Mawingu ya majira ya joto yataangaza karibuni. Masiku yakaenda. Siku moja akaja nyumbani kwangu na hakunikuta. Akapata khabari kwamba nilikuwa kwa Nidhaam, akabisha hodi na akaingia. Akasema: Nimeenda nyumbani kwako sikukukuta. Nina hamu ya kustafidi elimu yako. Nikamwambia: Ninayajua, lakini ususaji huu una maana gani? Akasema: Umemkufurisha Sayyid Qutwub! na hii ndio sababu. Nikamuuliza: Kwa nini? Akajibu: Umesema kuwa anazungumza kwa Wahdat-ul-Wujuud katika Suurat-ul-Hadiyd na al-Ikhlaasw. Nikasema: Ndio, ana baadhi ya maneno ya Suufiyyah. Hakuna ambacho mtu anaweza kufahamu zaidi ya kuwa anazungumza kwa mujibu wa Wahdat-ul-Wujuud. Lakini, kwa mujibu wa kanuni zetu ni kuwa hatumkufurishi mtu anayetumbukia katika kufuru kabla ya kumsimamishia hoja. Vipi unaweza kuitikia ususaji huu wakati niko baina yenu? Ikiwa wewe huwezi kuja, unaweza kuagiza mtu akahakikisha kama ni kweli kwamba namkufurisha Sayyid Qutwub au hapana. Sayyid Qutwub anasema haya na yale hapa na pale. Akashika upande mwingine na kusema: Mtu huyu anamwamini Allaah, Mtume Wake na Tawhiyd. Nikawa nimemwambia: Ndugu mpendwa. Hatukatai haki hii aliyosema, lakini tunakemea batili hii aliyosema. Pamoja na kikao hichi, akaeneza makala mbili au tatu katika gazeti la al-Mujtamaa´ Kuwait kwa anwani kubwa: Shaykh al-Albaaniy anamkufurisha Sayyid Qutwub. Ni historia kubwa. Mwenye kusema kuwa al-Albaaniy anamfanyia Takfiyr ni kama yule mwenye kusema kwamba al-Albaaniy anamsifu Sayyid Qutwub katika matukio fulani. Watu hawa ni Ahl-ul-Ahwaa´! Njia moja tu ya kushughulika na watu hawa ni wakuombea kwa Allaah: أَفَأَنتَ تُكْرِهُ النَّاسَ حَتَّىٰ يَكُونُوا مُؤْمِنِينَ “Je, basi wewe unawalazimisha watu mpaka wawe Waumini?” (10:99)

Imaam, ´Allaamah na Shaykh Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy amesema katika mjadala mmoja na mtu:

Umesikia kukizungumziwa kuhusu ´Abdullaah ´Azzaam?

Mtu yule: Ndio!

Shaykh: ´Abdullaah ´Azzaam hapa alikuwa na al-Ikhwaan al-Muslimuun. Miaka misaba au minane iliyopita al-Ikhwaan al-Muslimuun walinisusa. Wakasusa duruus zangu na Da´wah yangu na ´Abdullaah ´Azzaam ndio alikuwa mtu pekee katika al-Ikhwaan al-Muslimuun ambaye alikuwa kila siku anakuja katika duruus zangu na daftari dogo na kalamu ndogo sana. Wakati kulitoka maamuzi ya kususa mawaidha yangu, hakutokea tena. Siku moja nikakutana naye katika Msikiti Suhayb nje ya Swalah. Nikamsalimia na yeye akanisalimia kwa aibu kwa sababu alivunja makubaliano. Nikamwambia:

Haya ndio Uislamu unaamrisha?

Akasema:
Mawingu ya majira ya joto yataangaza karibuni.

Masiku yakaenda. Siku moja akaja nyumbani kwangu na hakunikuta. Akapata khabari kwamba nilikuwa kwa Nidhaam, akabisha hodi na akaingia. Akasema:

Nimeenda nyumbani kwako sikukukuta. Nina hamu ya kustafidi elimu yako. Nikamwambia:

Ninayajua, lakini ususaji huu una maana gani?

Akasema:

Umemkufurisha Sayyid Qutwub! na hii ndio sababu.

Nikamuuliza:

Kwa nini?

Akajibu:

Umesema kuwa anazungumza kwa Wahdat-ul-Wujuud katika Suurat-ul-Hadiyd na al-Ikhlaasw.

Nikasema:

Ndio, ana baadhi ya maneno ya Suufiyyah. Hakuna ambacho mtu anaweza kufahamu zaidi ya kuwa anazungumza kwa mujibu wa Wahdat-ul-Wujuud. Lakini, kwa mujibu wa kanuni zetu ni kuwa hatumkufurishi mtu anayetumbukia katika kufuru kabla ya kumsimamishia hoja. Vipi unaweza kuitikia ususaji huu wakati niko baina yenu? Ikiwa wewe huwezi kuja, unaweza kuagiza mtu akahakikisha kama ni kweli kwamba namkufurisha Sayyid Qutwub au hapana. Sayyid Qutwub anasema haya na yale hapa na pale.

Akashika upande mwingine na kusema:

Mtu huyu anamwamini Allaah, Mtume Wake na Tawhiyd.

Nikawa nimemwambia:

Ndugu mpendwa. Hatukatai haki hii aliyosema, lakini tunakemea batili hii aliyosema. Pamoja na kikao hichi, akaeneza makala mbili au tatu katika gazeti la al-Mujtamaa´ Kuwait kwa anwani kubwa:

Shaykh al-Albaaniy anamkufurisha Sayyid Qutwub.

Ni historia kubwa. Mwenye kusema kuwa al-Albaaniy anamfanyia Takfiyr ni kama yule mwenye kusema kwamba al-Albaaniy anamsifu Sayyid Qutwub katika matukio fulani. Watu hawa ni Ahl-ul-Ahwaa´! Njia moja tu ya kushughulika na watu hawa ni wakuombea kwa Allaah:

أَفَأَنتَ تُكْرِهُ النَّاسَ حَتَّىٰ يَكُونُوا مُؤْمِنِينَ
“Je, basi wewe unawalazimisha watu mpaka wawe Waumini?” (10:99)


  • Author: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy. Mkanda ”Mafaahiym yajib an nuswahhih”
  • Kitengo: Uncategorized , ´Azzaam, ´Abdullaah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Saturday 21st, June 2014