Imaam al-Albaaniy Kuhusu Mafungamano Ya al-Ghazaaliy Katika Sunnah

Ama kuhusiana na hazina yake ya elimu - al-Ghazaaliy - ni tupu. Wakati mmoja tulikuwa katika mualiko uliofanywa na wafanyakazi wamoja wa wizara ya ´Abdullaah bin Ibraahiym al-Answaariy. Ikaja juu ya kwamba mtu anaswali Rakaa mbili za Tahiyyat-ul-Masjid wakati Imamu anatoa Khutbah Ijumaa. al-Ghazaaliy akakataza Swalah hiyo na kusema: "Sionelei ya kwamba mtu aswali wakati ambapo Imamu anatoa Khutbah." Baadaye nikamwambia haiwezekani kufanya Ijtihaad ikiwa kuna dalili katika Qur-aan na Sunnah: "Nafikiria ya kwamba unajua kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema: "Mmoja wenu anapokuja siku ya Ijumaa na akamkuta Imamu anatoa Khutbah, hatakiwi kukaa mpaka aswali Rakaa mbili khafifu." Akasema: "Ndio, ila Imaam Maalik anaonelea ya kwamba mtu asiswali Rakaa hizi mbili." Allaahu Akbar! Majadiliano yakawa kwa kiasi fulani na baridi, lakini hayakuwa kamwe na moto. Hata hivyo hakujibadili pamoja na kwamba kuna Hadiyth Swahiyh katika suala hili. Ana mafungamano mengi kama haya katika Sunnah.

Ama kuhusiana na hazina yake ya elimu – al-Ghazaaliy – ni tupu. Wakati mmoja tulikuwa katika mualiko uliofanywa na wafanyakazi wamoja wa wizara ya ´Abdullaah bin Ibraahiym al-Answaariy. Ikaja juu ya kwamba mtu anaswali Rakaa mbili za Tahiyyat-ul-Masjid wakati Imamu anatoa Khutbah Ijumaa. al-Ghazaaliy akakataza Swalah hiyo na kusema:

“Sionelei ya kwamba mtu aswali wakati ambapo Imamu anatoa Khutbah.”

Baadaye nikamwambia haiwezekani kufanya Ijtihaad ikiwa kuna dalili katika Qur-aan na Sunnah:

“Nafikiria ya kwamba unajua kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema:

“Mmoja wenu anapokuja siku ya Ijumaa na akamkuta Imamu anatoa Khutbah, hatakiwi kukaa mpaka aswali Rakaa mbili khafifu.”

Akasema:

“Ndio, ila Imaam Maalik anaonelea ya kwamba mtu asiswali Rakaa hizi mbili.”

Allaahu Akbar! Majadiliano yakawa kwa kiasi fulani na baridi, lakini hayakuwa kamwe na moto. Hata hivyo hakujibadili pamoja na kwamba kuna Hadiyth Swahiyh katika suala hili. Ana mafungamano mengi kama haya katika Sunnah.


  • Author: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy. Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (167)
  • Kitengo: Uncategorized , al-Ghazaaliy al-Miswriy, Muhammad
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 12th, January 2014